Ikulu, Dodoma: Makabidhiano ya Ripoti ya CAG - Machi 28, 2021

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
905
1,000
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Edward Kichere leo tarehe 28 Machi, 2021 amemkabidhi Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ripoti za ukaguzi kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2020 katika halfa fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Kwa Mujibu wa Ibara ya 143 kifungu kidogo 2 na 4 cha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (kama ilivyorekebishwa) kinamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukabidhi Ripoti kwa Mheshimiwa Rais kabla au ifikapo tarehe 31 Machi kila mwaka na baada ya hapo Ripoti hizo huwasilishwa Bungeni ndani ya siku saba za mwanzo za kikao cha Bunge kinachofuata.

Fuatilia hapa kitakachokuwa kinaendelea.CAG: Katika ukaguzi wetu wa 2019/2020 tumebaini ATCL imetengeneza hasara ya TZS Bilioni 60

Kwa miaka 5 iliyopita Shirika limekuwa likitengeneza hasara

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amesema amekagua Vyama vya Siasa 17 ambapo Hati zinazoridhisha ni nne, zenye mashaka ni nne, hamna Hati mbaya lakini ameshindwa kutoa maoni kwenye hati tisa
-
Amesema ameshindwa kutoa maoni kwasababu hesabu zao hazikuzingatia utaratibu wa kutengeneza hesabu, na wengine hawakuzileta kabisa ili ziweze kukaguliwa

CAG Charles Kichere: Miradi ambayo nimefanya ukaguzi ni Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka DSM hadi Makutupora

- Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Mradi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka kwa DSM (UDART) Gerezani mpaka Mbagala

CAG Charles Kichere: Pia, tumekagua Mradi wa upanuzi wa barabara ya Morogoro kutoka Kimara hadi Kibaha

- Mradi wa usambazaji maji wa Same, Mwanga na Korogwe pamoja na mradi wa uzalishaji Sukari huko Morogoro

"Tutaendelea kutumia mbinu hii ya ukaguzi kwenye miradi ili kutoa ushauri kwa Serikali mapema ili kama kuna hatua za kuchukuliwa zichukuliwe mapema ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa" - Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Serikali

"Mbinu hii ya ukaguzi inawezesha mapungufu yanayoonekana kufanyiwa kazi kwa wakati badala ya kusubiri mradi umeshatekelezwa ndio tunaenda kutoa mapendekezo" - Charles E. Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Serikali

Nimefanikiwa kufanya ukaguzi wa kitaalamu kwenye miradi sita ya kimkakati. Kwenye kaguzi hizo, ofisi yangu imetumia mbinu mpya ambayo inahakikisha kwamba ukaguzi unafanyika kadri mradi unavyoendelea kutekelezwa - Charles E. Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Serikali

"Mradi wa upanuzi wa barabara ya Morogoro kutoka Kimara hadi Kibaha; mradi wa usambazaji maji wa Same, Mwanga na Korogwe; na mradi wa uzalishaji sukari huko Morogoro" - Charles Edward Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Serikali

Miradi ambayo nimefanya ukaguzi ni Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka DSM hadi Makutupora; mradi wa ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP); mradi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka kwa DSM (UDART) Gerezani mpaka Mbagala - Charles Edward Kichere

"Kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 nimetoa jumla ya hati 900 za ukaguzi ikiwa 243 serikali kuu, hati 185 za serikali za mitaa, hati 165 za mashirika ya umma, hati 290 za miradi ya maendeleo na hati 17 kwa vyama vya siasa” – CAG Kichere

Miradi ambayo nimefanya ukaguzi ni Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka DSM hadi Makutupora; mradi wa ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP); mradi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka kwa DSM (UDART) Gerezani mpaka Mbagala - Charles Edward Kichere

Kati ya hizo 900, hati zinazoridhisha ni 800 sawa na asilimia 89%, hati zenye shaka ni 100 sawa na asilimia 9%, hati mbaya ni 10 sawa na 1% - Charles E. Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Serikali

CAG.jpg

"Vyama vya siasa tisa nimeshindwa kutoa maoni kwa sababu hesabu zao hazikuzingatia utaratibu wa kutengeneza hesabu na wengine hawakuleta kabisa hizo hesabu ili niweze kuzikagua" - Charles E. Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Serikali

CAG Charles Kichere: Kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 nimetoa jumla ya hati 900 za ukaguzi ambapo nimetoa kwa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Miradi ya maendeleo, mashirika binafsi pamoja na vyama vya siasa

- Kati ya hizo, hati zinazoridhisha ni 800 sawa na 89%

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amesema katika mwaka wa fedha 2019/2020 aliahidi kuongeza wigo wa ukaguzi katika mashirika mengine 10 na ahadi hiyo imetekelezwa
-
Ameyataja baadhi ya Mashirika hayo kuwa ni Shirika la Nyumba la Taifa, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Kampuni ya Ndege Tanzania, Chuo Kikuu Ardhi, Mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya Udhibiti ya Manunuzi ya Umma
-
Aidha, amesema miradi ambayo imefanyiwa ukaguzi wa kitaalamu kuwa ni ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere, mradi wa miundombinu wa mabasi yaendayo haraka (Gerezani-Mbagala) na upanuzi wa barabara ya Morogoro kipande cha Kimara hadi Kibaha

CAG Charles Kichere: Katika mamlaka ya Serikali za Mitaa, nimekagua hati 185

- Hati zinazoridhisha ni 124, hati zenye mashaka ni 53, hati mbaya nane. Sikushindwa kutoa maoni kwenye halmashauri yoyote

Mkurugenzi TAKUKURU: Tanzania imeendelea kupata sifa kimataifa katika mapambano dhidi ya rushwa

- Katika ripoti ya Taasisi ya Transparency International inaonesha Tanzania kupanda kwa nafasi 8 na kushika nafasi ya 94 kati ya nchi 180

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU: TAKUKURU ilifanya Operesheni ya Mikopo umiza na kuweza kurejesha Tsh. Bilioni 2.6 mashamba/viwanja 18, Nyumba 27, magari 18 na pikipiki 41

Pia wananchi 904 walioathiriwa na mikopo umiza wamesaidiwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom