Ikulu, Dar: Yaliyojiri Kuapishwa kwa Mawaziri wateule Hussein Bashe na George Simbachawene

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Leo viongozi Mheshimiwa Bashe pamoja na Simbachawene watakula kiapo cha uaminifu kuziongoza wizara walizoteuliwa kuziongoza.

Rais Magufuli anawaapisha Mawaziri wateule ambao ni Mh. George Simbachawene kuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na Mhe. Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Yanayotarajiwa ni pamoja na sababu za Kumuondoa January Makamba kwani Rais kila akipangua safu yake huwa anatoa sababu.

UPDATES

======

IMG-20190722-WA0004.jpg

Bashe(Kushoto) na Simbachawene wakila kiapo.

Simbachawene: Nachukua nafasi hii kukushukuru Rais kwa kuniamini tena na kunipa nafasi ya kukusaidia tena kama Waziri wa Mazingira

- Nafahamu nchi ina matatizo makubwa sana katika sekta ya mazingira

Simbachawene: Natambua kuna hela nyingi zinaingia nchini na zinaenda kwenye NGOs na hata kwenye sekta ya umma lakini haziendi moja kwa moja kwenye mazingira zinaishia kwenye utawala

Simbachawene: Suala la mazingira linasemwa kwa namna tofauti. Kuna mazingira kimataifa na mazingira kwa sisi wenyewe. Haya lazima tuyaangalie sana

- Tukiangalia mazingira kimataifa zaidi wakati tunaendelea kuharibu mazingira yetu, hatuna sehemu ya kuishi

Simbachawene: Wizara hii ni wizara wezeshi, kwani kilimo kinategemea mazingira na kila kitu kinategemea Wizara hii; nitajitahidi kumshauri Makamu wa Rais

- Sehemu nyingine umenichagua ni Muungano. Sijui sana kuhusu hili ila nitajifunza zaidi ofisini kwa wataalamu

Simbachawene: Mimi na familia yangu tunakushukuru sana kwa kuniamini tena. Nafahamu umuhimu wa kiapo, mimi ni mwanasheria. Ukiapishwa leo unaendelea na kiapo hata nje ya utumishi

- Leo ni kiapo changu cha tano cha Rais, nitaendelea kuheshimu viapo hivi hata nikizeeka

Bashe: Nimshukuru Mungu, nikushukuru wewe Rais kwa imani uliyonionesha na najua jukumu hili si kuitwa Mheshimiwa bali kutumikia

- Nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kuweza kutimiza yaliyo kwenye uwezo wangu kwa ajili ya maendeleo

Bashe: Sekta ya kilimo tumekuwa tunaita tu kilimo cha kujikimu, ila nafahamu kilimo ni biashara na kilimo ni maisha

- Nafahamu uchumi wa nchi hii ambapo ndoto yako ni kujenga uchumi wa viwanda ni lazima wakulima wawe na uwezo, tuwatendee haki

Rais Magufuli: Mengi yamezungumzwa na waliomaliza kuapa. Nichukue nafasi kuwapongeza kwa majukumu haya mapya

Rais Magufuli: Suala la mazingira kasimamie vizuri wewe(Simbachawene) mwenyewe umeeleza hapa kuna fedha nyingi zimekuwa zikipelekwa kule lakini 'impact' yake haionekani

- Kuna idara ya mazingira kule, fedha nyingi zinatolewa na wafadhili lakini hazionekani zikitumika

Rais Magufuli: Kuna miradi hewa, kule Rufiji ikapandwa mikoko. Nataka haya ukayashughulikie. Vibali kama vya NEMC, wasiwe na ucheleweshaji kuvitoa kwa viwanda

- Wawekezaji wasiwekewe vipingamizi kwa visingizio vya NEMC, vibali hivi vitoke. Kwa sababu tunahitaji viwanda

Rais Magufuli: Wawekezaji wasicheleweshwe kuwekeza kwa vibali vya NEMC. Ikiwezekana wawekeze kwanza vibali vitakuja baadaye kwa sababu hivi vitu vyote ni vyetu

- Mpaka uzungumze halafu unasikia kibali kimetoka baada ya siku 5. Unajiuliza kwanini hakikutoka mwaka mzima?

Rais Magufuli: Nakumbuka suala la mifuko ya plastiki lilichukua muda mrefu karibia miaka minne. Nikasaini halikutekelezwa, Makamu wa Rais akazungumza wee halikutekelezwa

- Waziri Mkuu akaongea Bungeni, halikutekelezwa. Mwishoni nilipotoa amri ya lazima ndio likatekelezwa

Rais Magufuli: Usiende ukawe hivyo na wewe(kuchelewa). Utajifunza mengi sana kutoka kwa Makamu wa Rais, ni msimamizi mzuri

- Nimepanga mbeleni nitakutana na wafugaji wote kama nilivyokutana na watu wa madini na wafanyabiashara. Hatuwezi kutozishugulikia changamoto zao

Rais Magufuli: Kwa Naibu Waziri Bashe nakupongeza. Umechaguliwa katika sekta muhimu sana. Nimekuwa nakusikiliza sana Bungeni, michango yako huwa mizuri

- Unatoa 'analysis' ya namna kilimo kinaweza kuleta 'effect' katika uchumi wa nchi yetu. 'Analysis' zile nilizipenda

Rais Magufuli: Ila zile zilikuwa ni za Bungeni nataka sasa ukaziweke kwenye 'practical’, ndio maana nimekuweka kwenye wizara hiyo

- 'Theory' zote ulizokuwa unasema Bungeni na tukafurahia sasa yawe kwenye 'practical’. Nina matumaini makubwa, kayatekeleze

Rais Magufuli: Nafahamu sekta ya Kilimo ina changamoto sana. Mfano Bodi ya Sukari inapigwa vita sana ila inafanya kazi vizuri sana

- Nilikuwa nasubiri Waziri aivunje na yeye angepata cha mtema kuni, ila hajaivunja. Nataka kueleza ukweli

Rais Magufuli: Bodi ile inafanya kazi vizuri kweli ila wafanyabiashara wa sukari waliozoea kuitumia sukari kama ‘white gold’ wanaipiga vita kweli

- Tulisema hapana, kwa sababu 'gap sugar' katika nchi yetu ni ndogo haiwezi kuwa 'exaggerated' na kuletewa sukari za hovyo

Rais Magufuli: Nafahamu sekta ya Kilimo ina changamoto sana. Mfano Bodi ya Sukari inapigwa vita sana ila inafanya kazi vizuri sana

- Nilikuwa nasubiri Waziri aivunje na yeye angepata cha mtema kuni, ila hajaivunja. Nataka kueleza ukweli

Rais Magufuli: Nendeni mkashughulikie changamoto hizo. Nafahamu kule Kagera tumewaambia watu wauze kahawa, wawekezaji waje kununua ila ni kwa Tsh. 1,500 na zaidi

- Wafanyabiashara wachache wameanza kuwadanganya Wananchi. Wafanyabiashara hawa lazima washughulikiwe

Rais Magufuli: Changamoto kwenye pamba, tumeshasema kilo ni kuanzia Tsh. 1,200 ila wapo wanaonunua na kukopa

- Nilishasema wafanyabiashara wakitaka kukopa, mkampata anayetaka kuwalipa iuzeni hiyo pamba mpate pesa ili wakulima wapate fedha zao

Rais Magufuli: Niwapongeze na nendeni mkafanye kazi zenu. Mtapigwa vita, mtazungumzwa ila mengine mwachieni Mungu kwa sababu Mungu ndio ametaka muwe katika nafasi zenu

- Kashirikianeni na wanyonge, mtafanya kazi kubwa sana. Mungu awabariki sana. Asanteni

 
Kwanza nakupa HONGERA sana. Pili kuteuliwa kwako pia kumetokana na mchango wa Wana jamiiforums ambao kila mara wamekuwa wakikupigia debe. Mchango wako Bungeni ulikosha mioyo yetu na umepelekwa kwenye Wizara ambayo inasimamia wakulima wanyonge wa nchi hii. Sasa imefika zamu yako ya kuwasaidia wakulima wa pamba, kahawa, tumbaku nk. Yale uliyokuwa unayasema Bungeni ni nadharia sasa yaweke kwenye matendo. Kila la kheri Mhe. Bashe.
 
Leo viongozi Mheshimiwa Bashe pamoja na Simbachawene watakula kiapo cha uaminifu kuziongoza wizara walizoteuliwa kuziongoza.

Rais Magufuli anawaapisha Mawaziri wateule ambao ni Mh. George Simbachawene kuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na Mhe. Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Yanayotarajiwa ni pamoja na sababu za Kumuondoa January Makamba kwani Rais kila akipangua safu yake huwa anatoa sababu.


Mbona leo utaratibu umebadilika ambapo Siku zote za Uapisho ule muda wa Nasaha za Viongozi ukifika huwa anaanza Kwanza Makamo wa Rais kisha Waziri Mkuu na Jaji Mkuu ila leo nafasi hiyo amepewa tu mwenyewe Mheshimiwa Rais. Kulikoni?
 
Kwanza nakupa HONGERA sana. Pili kuteuliwa kwako pia kumetokana na mchango wa Wana jamiiforums ambao kila mara wamekuwa wakikupigia debe. Mchango wako Bungeni ulikosha mioyo yetu na umepelekwa kwenye Wizara ambayo inasimamia wakulima wanyonge wa nchi hii. Sasa imefika zamu yako ya kuwasaidia wakulima wa pamba, kahawa, tumbaku nk. Yale uliyokuwa unayasema Bungeni ni nadharia sasa yaweke kwenye matendo. Kila la kheri Mhe. Bashe.
Hivi mgawo wa fedha kwa wizara ya Kilimo kwa 2019/2020 ni kiasi gani kwa anayekumbuka tafadhali
 
Back
Top Bottom