#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,201
4,673
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi

Kamati Corona.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud​

---

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA​

KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA​

MUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA

WA COVID-19 NCHINI​

DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021

Ndugu wanahabari,
mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili,

2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.

Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.

Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.

Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:

1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.

2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga
(interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.

4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.

5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:


a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;

b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;

c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:

i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;
ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;
iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;
iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
v. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.
d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.

e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.

6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.

7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.

8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.

9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.

10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.

11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.

12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.

13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.

14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.

15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.

16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.

17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.

18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.

19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.

Ndugu Wanahabari, Asanteni kwa kunisikiliza.
 
Kwa mujibu wa DPC Gerson Msigwa Kamati maalumu iliyoundwa na Rais wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani kufanya tathmini ya ugonjwa wa corona (Covid-19) itawasilisha taarifa yake leo alasiri mbele ya Rais Ikulu Jijini Dar es salaam.

Matangazo ya moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya habari
Hao tayari walishanunuliwa na mabeberu, hata majina yao yalikuwa Siri.
 
Matumizi mabaya ya kodi za wananchi tu taarifa gani watazitoa zaidi ya porojo tu hv watanzania wanaitaji tume kuja kuambiwa wavae barakoa,wanawe mikono na maji tiririka ,wakae social distance kweli? Maana hakuna jipya watakalokuja nalo zaidi ya porojo hizo.

Dunia nzima inajua Covid ipo. Tanzania tulisema Covid hakuna kwetu na mazingira tunavyoishi mtaani kama ingekuwepo kweli kila siku tungekuwa tunazika watu.

Waje na porojo zao but swala la lockdown na chanjo hatutaki ..maana chanjo imekuwa ni biashara kubwa na inampaka madalali na nina imani hata watu wa tume madalali wameshawafata.

Naona kuna mtu anataka kufungua duka saa 2 usk wakat wenzie wanakaribia kufunga biashara.

Mechi ya Corona inakaribia kuisha mtu ndo anataka kuingiza timu uwanjani kucheza mchezo ambao wenzie wanakaribia kuumaliza.
 
Hao tayari walishanunuliwa na mabeberu, hata majina yao yalikuwa Siri.
Si mlidai CCM huwa inapika viongozu wazalendo na cjui mmeshaandaa succession plan had 2075 na kwamba kila kiongozi kawekwa na kitengo baada ya vetting ya kutosha. Vipi tena aliyeaminiwa na JPM ndio kanunuliwa? Ina maana CCM hamkujua Rais ana makamu atakayenunuliwa.

Nachokiona CCM haikujiandaa na the unexpected. Mpo overrated sana kumbe hamna kitu.
 
Kwa mujibu wa DPC Gerson Msigwa Kamati maalumu iliyoundwa na Rais wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani kufanya tathmini ya ugonjwa wa corona ( Covid-19) itawasilisha taarifa yake leo alasiri mbele ya Rais Ikulu Jijini Dar es salaam...
Kwa kuangalia hii picha, unaweza kuja na dhana Mbili za muhimu;

(1)Ukweli (Truth) (T)
na

(2) Uhalisia (Reality) (R)

Truth is Objective but
Reality is subjective.

Regardless of outcome, the Truth is determinant-- It has finality. It is what it is; unlike Reality which can be interpreted in different ways by the various people it affects".

Kwenye probability; occurrence of Event is always less or equal to 1:Ukweli +Uhalisia =? Dunia tunayoishi ni moja na muingiliano baina ya raia wa Nchi mbali mbali ni lazima
 
Ndo wameandika hayo mavitabu?

Halafu sidhani kama Samia atayasoma 🤣.

Sidhani kama ni mtu wa kusoma mavitabu kama hayo.

Yeye ni mitandao tu 🤣🤣.
Hapa atuna Rais,tuna rais wa tume,eti nchi itangaze kuwa tuna corona, wakati nchi nyingi zimeanza kuondokana na nyimbo hizo, Watu wanaanza kuchapa kazi, Sisi ndio tunaanza kuongopeshana.
 
Back
Top Bottom