Ikulu, Dar: Rais Samia akutana na kufanya mazunguzmo na Tony Blair

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,592
2,000
Hadi sasa naona wameshanyoosha mikono juu, Makamu Mkiti kawaamuru waingie barabarani kumdai Mkiti lakini hamna hata mtu mmoja aliyejitokeza, zimebaki kelele jf na Twitter ambapo impact yake ni ndogo sana.

Barabarani watu hawaiingii ghafla mzee, hata huko Zimbabwe, Sudan, Libya nk hawakuingia ndani ya miaka mitano au kumi. Huko tutafika tu wala usijali.

Unapoona watu wanateswa, kubambikiwa kesi, kutekwa, na bado hawaogopi basi ujue huko kwenye kuingia barabarani hakuko mbali. Tuombe tu wakati huo ukifika nchi ipite hilo jaribu bila kuwa kama Ethiopia. Chukua hiki ninachokuambia utanielewa tu.
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,592
2,000
Mzungu hawajawahi kuwa na upendo na mtu yeyote isipokuwa kwa maslahi yake, tujiulize, wanataka nini hasa kwetu na hayo machanjo yao? Msaada tangu lini mtu akakubembeleza kukupa? Hatutaki huo msaada jamani, mbona hivyo?!

Nimecheka kwa nguvu hiki ulichoandika, inawezekana kweli ukawa na hoja, ila hiyo hofu sio kwenye chanjo au dawa za wazungu, maana kwa sasa hakuna ambaye hajawahi kupata chanjo au dawa ya mzungu. Labda kama hizi hadithi za kugomea chanjo za wazungu ziwe za kufurahishia genge.
 

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
8,162
2,000
Huyo atakua ametumwa agenda zao ni zilizile za kutuzubaisha maendeleo. Aende rwanda kwa kagame ndio mtu wake anamsikiliza. Samia wakija watu kama kina tonny blair wasikilize wapotezee. Kazi yao kulinda ubeberu na uzayuni.
 

kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
4,366
2,000
Marehemu Mugabe ndio alikuwa kiboko ya Tony Blair.
Ungemalizia basi ahaaaa mgabe bwana
Ile kauli Blair hakusubutu tena kumsema mgabe
Ukiona MTU anasema mama yako ndo naweza kuongea nae mwanafunzi mwezangu kuaga makini

Lakini vilevile mama awe makini kwani waziri huyu mkuu mstaafu toka uingereza ndio mshauri wamaswala ya uchumi na rafiki mkubwa wa KAGAMe rais

wa RWanDA

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 

Baraka21

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
1,282
2,000
Ahahahahahah siyo huyu bwana,yule alikuwa David Cameroon..mpaka tukasnzisha kamsemo hapa Katerero ka nitaku-Cameroon ujue ahshsh
Kweli mkuu ni Cameroon ndio alikuwa hakupi msaada bila kuheshimu ndoa za jinsia moja.
 

Hoshea

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
5,272
2,000
Alikuja Obama na Bush tena wakiwa madarakani na hakuna jipya, itakuwa huyo mstaafu wa UK? Mama wa kambo hajatukanwa bali anapewa ukweli wake, mnamjaza ili abebe ajenda zenu nyie sukuma Gang. Katiba mpya ni dai halali, na wapinzani wanafanya mikutano ya ndani hawahitaji hisani ya mama wa kambo. Hao cdm watakuwa ni wajinga kama watasubiri hisani ya ccm wasiotaka katiba mpya.
Bado tu mnapambana na sukuma gang, mnachekesha na kutia huruma
 

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,875
2,000
Tonh Blair bila aibu wala kupepesa macho anasema anafanya biashara ya corona! Atukome!! Hiyo biashara akaifanyie nchini kwao!! Akawapime mabeberu wenzake! Akawachanje mabeberu wenzake!

Mama kamjibu vizuri sana, sisi tuna mpango wetu na vipaumbele vyetu!! Kama ana kiherehere cha kusaidia na atusaidie kukamilisha reli ya standard gauge!! Vinginevyo asitupangie!
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
14,480
2,000
Blair kwa sasa anafanya kazi za kuzisafisha tawala za kidikteta. Anatafuta pesa kwa njia yoyote kutoka kwa yeyote, hakuna lingine.
Ana mikono iliyojaa damu pia ya Wa Iraq.
Hapo anaonywa Udikta hauna nafasi Duniani....
 
Oct 27, 2020
97
400
Jana rais alikutana na waziri mkuu mstaafu wa uingereza Tony Blair. Agenda ni kwamba aisaidie kuishauri serikali maswala mbali mbali, ikiwemo kui-rebrand/safisha serikali kupitia taasisi yake ya Tony Blair Institute for Global Change. Tony Blair kupitia hii taasisi huwashauri viongozi kadhaa wa Afrika kama Kagame n.k

Watu wake wanakuwa attached katika ofisi ya Rais, wizara n.k katika kipindi chote cha ushauri ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

Je huu si ukoloni mambo leo au neo liberalism? Mabeberu sasahivi ndo wamekuwa washauri wa kiongozi wa juu wa nchi. Inamaana hatuna wataalamu nchini au katika wizara, hadi atafutwe mtu wa nje na kupewa access kubwa namna hiyo. Kwamba mtu wa nje ndo anafahamu suluhu ya matatizo yetu kuliko sisi wenyewe tuishio nchini?

Tujitafakari.

20210723_050907.jpg
 

KEROZENE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
6,119
2,000
Samia Suluhu akutana na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair...
Kwahiyo baada ya kuwa Mmoja wa Wazungumzaji katika Kumbukizi ya Hayati Rais Mkapa ndiyo Kaalikwa? Je, na Bill Clinton nae ataalikwa hivi karibuni?
 
  • Thanks
Reactions: Ame

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
4,399
2,000
Hongera sana Rais wetu kwa kuendelea kuipa heshima ya kimataifa nchi yetu.

Mungu azidi kukupa afya njema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom