Ikulu, Dar | Rais Magufuli awaapisha Viongozi mbalimbali: Dkt. Abbas kuendelea kuwa Msemaji wa Serikali huku akiwa Katibu wa Wizara ya Habari

Yani Magu alivo mkipiga kelele yeye ndo anakanyagia hapo hapo ili muumie zaidi..... Id fake bana kila mtu anaouwezo wa kupiga kelele

MashineNyeusindefu
 
Hapana mkuu leo tutakuwa bize tunafuatilia hotuba ya Mbowe maana leo ataongea na waandishi wa habari, nyie endeleeni tu sanaa na kick za substandard za kutumbua zimeishatukinai kwa sasa.
Hotuba ya mbowe mida gani?
 
Roving Journalist,

Kwanini na wale Wateuliwa wengine wa Bodi na Mabaraza kama akina Profesa Martha Qorro nao hawakuapishwa pamoja na hawa Wenzao? Je, nao walikuwepo leo hapo Ikulu katika hiyo Hafla?
 
Rais Magufuli anawaapisha leo hii Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna Jenerali wa Zimamoto, Makatibu wakuu na Makatibu tawala wa mikoa saa 3:30 asubuhi.



A. MAKATIBU WAKUU
1. MARY GASPER MAKONDO - kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mary Gasper Makondo alikuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Anachukua nafasi ya Bi. Doroth Mwanyika ambaye amestaafu.

2. Dkt. HASSAN ABBAS - kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Hassan Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo. Anachukua nafasi ya Bi. Suzan Mlawi ambaye amestaafu.

3. Prof. RIZIKI SILAS SHEMDOE - kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huo Prof. Riziki Silas Shemdoe alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Prof. Joseph Buchweishaija ambaye amestaafu.

4. ZENA AHMED SAID - kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huo Bi. Zena Ahmed Said alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga. Anachukua nafasi ya Dkt. Hamis Mwinyimvua ambaye amestaafu.

5. CHRISTOPHER KADIO - kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Christopher Kadio alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Anachukua nafasi ya Mej. Jen Jacob Kingu ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.


B. NAIBU KATIBU MKUU
6. LEONARD MASANJA - kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huo Bw. Leonard R. Masanja alikuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala.


C. MAKATIBU TAWALA WA MIKOA
7. JUDICA HAIKASE OMARI - kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga.

8. STEPHEN MASHAURI - kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.

9. EMMANUEL MPAWE TURUBA - kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Majeshi.


D. WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA
10. Brig. Jen. SULEMAN MUNGIYA MZEE - kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza. Brig. Jen. Suleiman Mungiya Mzee anachukua nafasi ya Phaustine Kasike ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

11. Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) JOHN WILLIAM MASUNGA - kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. DCP John William Hasunga anachukua nafasi ya Thobias Andengenye ambaye uteuzi wake umetenguliwa.


E. KAMISHNA WA ARDHI
12. NATHANIEL MATHEW NHONGE - kuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Nathaniel Mathew Nhonge alikuwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.


F. MSAJILI WA MAHAKAMA
13. WILBERT CHUMA - kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama.

14. KELVIN MHINA - kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.

15. SHAMIRA SARWAT - kuwa Msajili wa Mahakama Kuu.


G. MAKAMISHNA WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
16. Jaji Dkt. GERALD NDIKA - kuwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama

17. Wakili JULIUS KALOLO BUNDALA - kuwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa

18. Wakili GENOVEVA KATO - kuwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.


DKT. ABBAS KUENDELEA KUWA MSEMAJI WA SERIKALI -

Rais Magufuli amesema Dkt. Hassan Abbas aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ataendelea kuwa Msemaji hadi mwingine atakapopatikana - Amesema, "Dkt. Abbas amefanya kazi nzuri kwa kufuata miongozo vizuri"

Huu ukumbi awamu hii umevunja record ya viapo .............!!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom