IKULU, DAR: Rais Magufuli awaapisha Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Balozi na Wakuu wa Mikoa aliowateua jana

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397



KUTOKA IKULU, DAR: Rais Magufuli anawaapisha Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Balozi pamoja na Wakuu wa Mikoa aliowateuwa hapo jana. Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mabalozi, Wakuu wa Mikoa, Makatibu & Manaibu Katibu: Wamo Mnyeti, Mangu, Kashilila..

- Ungana nami nikikuletea matangazo haya moja kwa moja.

=======

Ameapishwa Adam Kighoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara

Alexander Mnyeti ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara

Ameapishwa Joachim Leonard Wagabo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Ameapishwa Robert Gabriel Lughumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita

Ameapishwa Gelasius Gasper Byakanwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara

Ameapishwa Bi. Christine Solomoni Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

Rais Magufuli amesema, Christine Mndeme aliyemteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ataanzia kazi Mkoa wa Ruvuma na RC Ruvuma atahamia Dodoma.

Haiwezekani Ukuu wa Wilaya uanzie Dodoma na Ukuu wa Mkoa uanzie Dodoma ambapo ni Makao Makuu ya Nchi. Mndeme atakwenda Ruvuma kwanza- Rais Magufuli

Habari zaidi.....

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuhamisha kituo cha kazi Christina Mndeme ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na sasa atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Mndeme ambaye awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, jana aliteuliwa na Rais Dkt Magufuli ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, alipangiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akichukua nafasi ya Jordan Rugimbana.

Mndeme.JPG
Christina Mndeme

Rais ametangaza mabadiliko hayo mapema leo alasiri mara baada ya viongozi mbalimbali walioteuliwa kula kiapo ambapo amesema kuwa Mndeme ataanzia kazi katika Mkoa wa Ruvuma na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Binilith Satano Mahenge atahamia Dodoma.

Akisema sababu ya uamuzi huo, Rais walisema kwamba, haiwezekani mtu akaazia Ukuu wa Wilaya Dodoma, halafu akipandishwa cheo kwenda Ukuu wa Mkoa aanzie tena Dodoma ambapo ni Makao Makuu ya Nchi.

Nataka aendeke kwanza Ruvuma akapate mitikisiko na kuhakikisha barabara zinajengwa, na wakati huko aliyekuwa Ruvuma atakuja Dodoma, alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais amesema kuwa viongozi hao walioapishwa leo wameanza kazi mara moja kwani hakuna suala la kuwa mgeni na yeye endapo atataka taarifa yoyote atampigia mtu simu amueleze licha ya kuwa ameapishwa leo, na hivyo ni lazima wajifunze vitu mbalimbali kuhusu maeneo yao haraka.
 
KUTOKA IKULU, DAR: Rais Magufuli anawaapisha Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Balozi pamoja na Wakuu wa Mikoa aliowateuwa hapo jana.

- Ungana nami nikikuletea matangazo haya moja kwa moja.
Weka link ya live tuone basi
 
Kama anadhani kuwa anaweza kuficha ubovu wa miundombinu ya dar kwa kufurika kwa maji kwa kuteua na kuapisha basi hii serikali ya viwanda mwisho wake nimmbaya sana,, anahamisha mjadala,,, taarifa zilizopo wajeda hawajalipwa na muda wowwote kukinukisha hata CDF huwezi kumuona hapo,,, wanapoteza hali
 
Rais atumie jukwaa hili LA kuapisha wateuliwa wapya kuwajibu Barrick na upuuzi wao Wa kutupa masharti! Awake siku 14 kutoa hizo 700 bilioni vinginevyo wafunge virago!
 
Kama anadhani kuwa anaweza kuficha ubovu wa miundombinu ya dar kwa kufurika kwa maji kwa kuteua na kuapisha basi hii serikali ya viwanda mwisho wake nimmbaya sana,, anahamisha mjadala,,, taarifa zilizopo wajeda hawajalipwa na muda wowwote kukinukisha hata CDF huwezi kumuona hapo,,, wanapoteza hali
Hakuna uhusiano wa ulichoandika na suala la kuapisha walioteuliwa. Jitahidi kuongelea vitu vinavyoshaendana na mada ili tukuelewe.
 
Back
Top Bottom