IKULU, DAR: Rais Magufuli awaapisha Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Balozi na Wakuu wa Mikoa aliowateua jana


Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
5,922
Likes
6,683
Points
280
Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
5,922 6,683 280


KUTOKA IKULU, DAR: Rais Magufuli anawaapisha Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Balozi pamoja na Wakuu wa Mikoa aliowateuwa hapo jana. Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mabalozi, Wakuu wa Mikoa, Makatibu & Manaibu Katibu: Wamo Mnyeti, Mangu, Kashilila..

- Ungana nami nikikuletea matangazo haya moja kwa moja.

=======

Ameapishwa Adam Kighoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara

Alexander Mnyeti ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara

Ameapishwa Joachim Leonard Wagabo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Ameapishwa Robert Gabriel Lughumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita

Ameapishwa Gelasius Gasper Byakanwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara

Ameapishwa Bi. Christine Solomoni Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

Rais Magufuli amesema, Christine Mndeme aliyemteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ataanzia kazi Mkoa wa Ruvuma na RC Ruvuma atahamia Dodoma.

Haiwezekani Ukuu wa Wilaya uanzie Dodoma na Ukuu wa Mkoa uanzie Dodoma ambapo ni Makao Makuu ya Nchi. Mndeme atakwenda Ruvuma kwanza- Rais Magufuli

Habari zaidi.....

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuhamisha kituo cha kazi Christina Mndeme ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na sasa atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Mndeme ambaye awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, jana aliteuliwa na Rais Dkt Magufuli ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, alipangiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akichukua nafasi ya Jordan Rugimbana.

Christina Mndeme

Rais ametangaza mabadiliko hayo mapema leo alasiri mara baada ya viongozi mbalimbali walioteuliwa kula kiapo ambapo amesema kuwa Mndeme ataanzia kazi katika Mkoa wa Ruvuma na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Binilith Satano Mahenge atahamia Dodoma.

Akisema sababu ya uamuzi huo, Rais walisema kwamba, haiwezekani mtu akaazia Ukuu wa Wilaya Dodoma, halafu akipandishwa cheo kwenda Ukuu wa Mkoa aanzie tena Dodoma ambapo ni Makao Makuu ya Nchi.

Nataka aendeke kwanza Ruvuma akapate mitikisiko na kuhakikisha barabara zinajengwa, na wakati huko aliyekuwa Ruvuma atakuja Dodoma, alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais amesema kuwa viongozi hao walioapishwa leo wameanza kazi mara moja kwani hakuna suala la kuwa mgeni na yeye endapo atataka taarifa yoyote atampigia mtu simu amueleze licha ya kuwa ameapishwa leo, na hivyo ni lazima wajifunze vitu mbalimbali kuhusu maeneo yao haraka.
 
Z

Zee la kitaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2017
Messages
395
Likes
198
Points
60
Age
44
Z

Zee la kitaa

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2017
395 198 60
KUTOKA IKULU, DAR: Rais Magufuli anawaapisha Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Balozi pamoja na Wakuu wa Mikoa aliowateuwa hapo jana.

- Ungana nami nikikuletea matangazo haya moja kwa moja.
Weka link ya live tuone basi
 
balimar

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
3,715
Likes
4,721
Points
280
balimar

balimar

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
3,715 4,721 280
Mbona mimi sichaguliwi jamani?
 
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
33,428
Likes
73,946
Points
280
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
33,428 73,946 280
Wacha waendelee kuapishana
 
king Davidson

king Davidson

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2017
Messages
252
Likes
1,042
Points
180
king Davidson

king Davidson

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2017
252 1,042 180
Kama anadhani kuwa anaweza kuficha ubovu wa miundombinu ya dar kwa kufurika kwa maji kwa kuteua na kuapisha basi hii serikali ya viwanda mwisho wake nimmbaya sana,, anahamisha mjadala,,, taarifa zilizopo wajeda hawajalipwa na muda wowwote kukinukisha hata CDF huwezi kumuona hapo,,, wanapoteza hali
 
M

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Messages
6,127
Likes
3,616
Points
280
M

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2015
6,127 3,616 280
Rais atumie jukwaa hili LA kuapisha wateuliwa wapya kuwajibu Barrick na upuuzi wao Wa kutupa masharti! Awake siku 14 kutoa hizo 700 bilioni vinginevyo wafunge virago!
 
G Sam

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
6,890
Likes
12,845
Points
280
G Sam

G Sam

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
6,890 12,845 280
Yeye anajiweka live, ila hataki Wabunge tuwaone live. Mzee selfish huyu jamani sijapata kuona. Ila nyie Wabunge hebu rudisheni bunge live why Yeye kila anachofanya anajiweka live ?
Sasa si ni wewe na wenzako mlimuweka hapo juu?....Umenipa madaraka ya kuleeevyaaa oohh baby ooohh baby...
 
Z

Zee la kitaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2017
Messages
395
Likes
198
Points
60
Age
44
Z

Zee la kitaa

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2017
395 198 60
Kama anadhani kuwa anaweza kuficha ubovu wa miundombinu ya dar kwa kufurika kwa maji kwa kuteua na kuapisha basi hii serikali ya viwanda mwisho wake nimmbaya sana,, anahamisha mjadala,,, taarifa zilizopo wajeda hawajalipwa na muda wowwote kukinukisha hata CDF huwezi kumuona hapo,,, wanapoteza hali
Hakuna uhusiano wa ulichoandika na suala la kuapisha walioteuliwa. Jitahidi kuongelea vitu vinavyoshaendana na mada ili tukuelewe.
 
M

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2013
Messages
8,071
Likes
18,436
Points
280
M

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2013
8,071 18,436 280
Sijapata kuona Kiongozi wa ajabu kama huyu..

Bunge hataki kabisa lionekane Live..

Ila matukio haya yeye kwake kuonekana Live ni lazima..

Wabunge wanaofanya Bunge liwe la ovyo ni wa CCM.
 
W

wanaojulikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2017
Messages
577
Likes
859
Points
180
W

wanaojulikana

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2017
577 859 180
Yule mkuu wa mkoa wa geita alimchagua kwa mbwembwe sasa imekuwaje tena
 

Forum statistics

Threads 1,272,900
Members 490,197
Posts 30,463,859