Ikulu, Dar: Rais Magufuli ataka Lugumi achukuliwe hatua. Kuna hela zimechezewa NIDA, achoka kutoa rambirambi

Matokea ya Push up za Magu kwa watendaji wakuu wa serikali na taasisi zake ikiwemo wabunge wa CCM yafunguliwa rasmi.
Ni knock out kwa raundi ya kwanza hadi ya tatu.Ukiwa mwanamume utajikongoja hadi raundi ya 8 out of 10.
 
Sasa yule dogo Abdul Nondo si alisema alijiteka ili apate kiki kwa mkulu, au amesha sahau?, ningefurahi kusikia comment za dogo baada ya huyu kutumbuliwa
 
Sakata la korosho lililozua mjadala katika mkutano wa Bunge la Bajeti limemuibua mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli aliyesema walipanga kuwatimua uanachama wabunge wa mikoa ya Lindi na Mtwara iwapo wangekwamisha Sheria ya Bajeti 2018.

Rais Magufuli amesema hata kama Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa naye angekuwamo katika kupinga mapendekezo ya Serikali, angetimuliwa.

Mjadala huo ulihusisha zaidi ya Sh200 bilioni za ushuru wa mauzo ghafi ya korosho nje ya nchi na mabadiliko ya sheria yaliyopendekeza fedha zote za ushuru huo kuingia kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

Hatua hiyo iliwafanya wabunge wa mikoa ya Kusini kuungana na wanaotoka mikoa mingine inayolima korosho kuibana Serikali, huku baadhi ya wabunge wa CCM wakisema mabadiliko na kutolipwa kwa fedha hizo kutakiua chama hicho katika mikoa hiyo.

Majimbo ya mikoa ya Kusini yako 18, Mtwara ikiwa nayo 10 na Lindi manane, na CCM inaongoza kwa kuwa na majimbo 11 huku upinzani nayo saba. Ukijumlisha na wabunge wawili wa viti maalumu, mmoja wa Lindi na mwingine wa Mtwara wanakuwa 13 wa CCM.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam jana baada ya kuwaapisha mawaziri na naibu katibu wakuu aliowateua juzi, Rais Magufuli alimpongeza mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba aliyemwapisha kuwa naibu waziri wa Kilimo jinsi alivyochangia akiunga mkono mapendekezo ya Serikali.
 
Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam jana baada ya kuwaapisha mawaziri na naibu katibu wakuu aliowateua juzi, Rais Magufuli alimpongeza mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba aliyemwapisha kuwa naibu waziri wa Kilimo jinsi alivyochangia akiunga mkono mapendekezo ya Serikali.

Haya baba.
 
Inasikitisha sana kuona Mtanzania na ambaye anampenda kweli Rais wake anakosea kuliandika vyema jina lake na badala ya kuandika Magufuli anaandika Magufuri. Ushauri tu tujifunze kuwa makini hasa tunapoandika kwani kuna wengine tumebobea katika Mawasiliano na Uandishi hivyo tunapoona Mtu anafanya Kosa la Kitaaluma lihusulo Uandishi na hasa hasa utajaji wa majina ya Watu huwa tunaumia kama siyo kukereka sana tu.
Mkulya wa kwanza kujua vizuri Kiswahili, wazee wa kubadiri L kua R. Just joke mtani wangu
 
Naam,hayo ndiyo maneno ya Rais kwa waziri mkuu!Kwamba naye angetetea fedha za walima korosho wa kusini naye angefukuzwa!
Namshauri PM ajiuzulu tu,ipo siku atadhalilishwa zaidi ya hapo!
 
Naam,hayo ndiyo maneno ya Rais kwa waziri mkuu!Kwamba naye angetetea fedha za walima korosho wa kusini naye angefukuzwa!
Namshauri PM ajiuzulu tu,ipo siku atadhalilishwa zaidi ya hapo!
 
4. Mhe. Mussa Ramadhani Sima (Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini) anaapa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mazingira.

5. Mhe. Omary Tebwete Mgumba anaapa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

6. Moses Mpogole Kusiluka ameapa kuwa Katibu Mkuu Ikulu

=======


Wa kilimo, nakupongeza kwa mchango wako bungeni, mimi huwa naangalia hasa wa CCM wapo ambao huwa wanajisahau, unakuta mwingine anazungumza tukifanya hivi tutashindwa, kwanini unaendelea kuwa humu, si ondoka.

Wewe nakupongeza, ulisimama, Mwenyekiti alikuwa anajaribu kuzibaziba na kwa sababu mwenyekiti huyo huyo alihusika kuzitengeneza hizo sheria mbaya za wakati ule, alishiriki kuharibu hizo sheria akawa anakukatisha tamaa, nakupongeza, nikasema wewe unastahili hiki ulichokipata.

Wapo waliokuwa wanataka umaarufu kule bungeni wakawa wanasema watafanya fujo, nikamwambia waziri mkuu waache wafanye fujo. Nitaanzia kwenye jimbo lake kama kuna shangazi zake nitaanza kupia hao


Nilimuuluza mtwara na lindi kuna wabunge wangapinwa ccm akasema 17 nikamwambia bora waondoke wote. na nikambigia simu katibu waccm na kuongea nae kwamba tuanze mpango huo. Pampoja na yeye Waziri mKuu angeondoka na yeye si wa huko huko

na wakati wa kupitisha bajeti nilimuambia katibu mkuu nenda kaangalie wabunge wote wa ccm ambao hawatakuwepo bungeni na awatandike barua. " Katibu Mkuu umefanya hivyo?".






 
Ishu ya lugumi ni mtego nyuma ya lugumi kuna wazito......ngoja tuone mchezo ukataochezwa Huo

Ova
 
Tunataka watimize majukumu yao ili tusonge mbele
Kweli mkuu. Miaka 30 ya porojo na ubabaishaji imetufanya watanzania tuamini kwamba hayo mambo ndo uhalisia wa maisha yetu, inasikitisha sana. Watu wanateuliwa kwenye nafasi za uongozi wanaona ni kama wamepewa zaidi binafsi, hakuna kazi zinazofanyika zaidi ya wizi, rushwa, uzembe, ubabaishaji na porojo. JPM anajaribu kutufanya tujione kuwa we can do better than that, and honestly we're better than that.
 
Back
Top Bottom