Odinga ni mtu anaetumia akili sana katika siasa za upinzani, wapinzani wa Tz igeni mfano wake.
 
Tunaomba (mimi na wengine kama mimi) ushahidi wa makabidhiano kati ya Mungu na “mwanaume” juu ya makabidhiano ya mwanaume kwa Eden and after!

Pls Chief....
download biblia kwenye simu ujisomee! achaga kufatilia porno tuuuu kuliko neno la uzima kijanaa!
 
Unamfananisha Odinga na hawa wapinzani wasaka tonge wa TZ? Odinga ni mwanasiasa mashuhuri zaidi A. Mashariki na kati, anahitaji heshima yake!! TZ hamna upinzani serious wa Rais kubother kukutana nao, wapinzani wa TZ ni wa kuwapuuza
Umeongea kama wanaume 10 walioshiba.....hongera
 
Odiga ana maslahi gani na TANZANIA??

Unakutana na mpinzani wa nchi nyingine halafu wako umewapa makosa ya Ugaidi?
Odinga sio tu mpinzani bali Ni waziri mkuu mstaafu wa nchi ya Kenya, in that matter huwezi shangaa yeye kualikwa au kwenda ikulu kuonana. Na raisi yyte wa nchi yoyte...hata EL alipokuwa CDM alienda Kenya mara kadhaa kwene hafla alizoalikwa na raisi Kenyatta Kama waziri mkuu mstaafu ......
 
Kijana, jibu langu kwako ni kwamba angalau Kenya wanajua gharama ya uhuru. Kila walicho nacho Kenya wamekipigania na si kama sisi ambao hata huo uhuru tuliupata bwerere.

Kenya hawakupewa uhuru mezani, hapana, walipigana vita wakidai. Hawakuomba haki, hapana, walipambana kuidai. Katiba yao haikuwa hisani ya watawala, la hasha, waliidai kwa nguvu na vitendo.

Kwa kifupi Kenya wanajua gharama ya uhuru, haki na usawa. Watasahau vipi huku makovu wanayo ya kuwakumbusha muda wote. Hawawezi kumruhusu limbukeni moja kuchezea katiba yao.
Mkuu, natamani ningepata muda wa kutosha kueleza hili lakini bahati mbaya sina. Kifupi tu niseme awali nakubaliana nawe kuwa historia ya Kenya na Tanzania ni tofauti katika namna ya kupata uhuru. Hiki ni kitu cha kawaida kwa kila nchi na hata kwa ngazi za mtu mmoja mmoja. Tuna historia tofauti tofauti na huo siyo udhaifu.

Kwa upande wa Katiba ambayo ilikuwa ndiyo ajenda kubwa, nchi zote Tanzania na Kenya katiba zake zimepatikana kwa processes ndefu na naweza kusema kuwa madai yake yake yamechagizwa zaidi na mabadiliko ya mazingira ya wakati husika kuliko wananchi kuipigania kama unavyoeleza.

Kwa mfano kwa Kenya naweza kusema kifupi sana kuwa wamefika hapa walipo kwa mazingira yaliyowalazimishwa kuwa nayo. 1963 kama sisi walipata uhuru na wakawa na independence constitution ambapo Kenyatta alikuwa PM na Queen Elizabeth aliendelea kuwa Head of State.

Moja ya tatizo kubwa walilorithi kwenye katiba hiyo ni suala la serikali ya majimbo ambapo wakati huo kulikuwa na majimbo 7 na yaligawanywa kwa misingi ya ukabila. Hilo linaendelea kuwala hadi leo.

1964 Kenya ilifanya mabadiliko makubwa na kuitangaza Kenya kuwa Republic wakati huo ikiwa na vyama vingi. Hata hivyo baada ya kufariki kwa Kenyatta 1978 na Moi kuchukua madaraka,Kenya iliingia katika mfumo wa chama kimoja (de jure single party state) kama ilivyokuwa Tanzania.

Kutokana na upepo wa siasa za dunia kubadilika miaka ya 1990. Kama ilivyokuwa kwa Tanzania, Kenya pia waliingia katika vuguvugu za siasa za vyama vingi na madai ya kutaka mabadiliko katiba yao.

Takriban kipindi chote cha kuanzia 1992 hadi 2002 tunaweza kusema kuwa mazingira (siyo kupigana) yalilazimisha Kenya kuwa na reforms nyingi ndani ya katiba yao (clamour reforms) kama ilivyokuwa kwa Tanzania.

Vuguvugu hizo za Reform zilisababisha chama tawala cha Kanu kuondolewa madarakani na Kenya kutawaliwa na chama cha NARC chini ya Mzee Mwai Kibaki (2002-2013)

Wakati wa utawala wa NARC hasa mwaka 2003 Kenya ilianzisha majadiliano makubwa ya kikatiba kutokana na mazingira ya wakati huo ikijulikana kama NCC (the National Constitution Conference )ambayo ilikutana Bomas. NCC ilikuja na rasimu iliyoitwa 'Bomas Draft Constitution' ambayo bahati mbaya au nzuri ilikataliwa na Wakenya kwenye kura ya maoni ya mwaka 2005. Ni kama mchakato huo uliishia hapo kama wa kwetu ulivyotulia.

Bahati mbaya kwa Kenya, uchaguzi mkuu wa 2007 ulileta machafuko makubwa na wengi kuuwawa. Mazingira haya yaliilazimisha Kenya kufanya mazungumzo chini ya jopo lililojumuisha pia Mzee wetu Mkapa (RIP) na kukubaliana kufanya mabadiliko makubwa ndani ya katiba yao na kuingiza NARA (National Accord and Reconciliation Act).

NARA ilimwezesha Raila Odinga kutoka upinzani kuwa Waziri Mkuu na ikaundwa serikali ya pamoja (coalition government). Hatua hii iliipeleka Kenya hadi mwaka 2013 na coalition government hiyo kuvunjika.

Naweza kusema kuwa machafuko ya kisiasa ya 2007 yaliwasukuma wakenya kukubalina na katiba yao mpya ambayo waliipitisha kwenye kura ya maoni ya 2010. Wakupenda waingie kwenye uchaguzi mwingine bila katiba mpya kuepuka uzoefu wa machafuko ya 2007. Sijui ndiyo tafsiri yako ya kupigana lakini mimi naona ni zaidi nguvu ya mazingira waliyokuwamo.

Katiba hiyo imepata tena attempt ya kutaka irekebishwe mwaka jana kupitia mpango wa BBI na ikapitishwa na Bunge. Hata hivyo wiki hii Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali mchakato huo wa marekebisho ya katiba ya BBI. Sijui na huu uamuzi wa mahakama unaitafsiri kuwa ni kupigana?

Niseme tu kifupi kuwa katiba nyingi duniani zinabadilika kutokana na mazingira yanayokuwepo wakati huo zaidi kuliko watu kupigana na kuzidai. Hii ndiyo maana Rais Samia amekuwa akieleza kuwa mazingira ya sasa ambayo aliyekuwa mkuu wa nchi amefariki miezi mitano tu iliyopita siyo mazingira rafiki ya kufanya mabadiliko ya katiba. Ameomba apewe muda lakini bahati mbaya sana CHADEMA wameanza kuleta vurugu ambayo ambayo imetufikisha hapa tulipo.

Naomba tuheshimu kauli ya Rais. Mazingira ya sasa siyo mazingira ya kushinikiza katiba mpya. Wakenya uliowataja kama role model wako, hawajapigana kwa ajili ya kudai katiba yao. Tusipigane wala kuleta vurugu kwa kwa ajili ya kudai katiba mpya.
 
Mkuu, natamani ningepata muda wa kutosha kueleza hili lakini bahati mbaya sina. Kifupi tu niseme awali nakubaliana nawe kuwa historia ya Kenya na Tanzania ni tofauti katika namna ya kupata uhuru. Hiki ni kitu cha kawaida kwa kila nchi na hata kwa ngazi za mtu mmoja mmoja. Tuna historia tofauti tofauti na huo siyo udhaifu.

Kwa upande wa Katiba ambayo ilikuwa ndiyo ajenda kubwa, nchi zote Tanzania na Kenya katiba zake zimepatikana kwa processes ndefu na naweza kusema kuwa madai yake yake yamechagizwa zaidi na mabadiliko ya mazingira ya wakati husika kuliko wananchi kuipigania kama unavyoeleza. Kwa mfano kwa Kenya naweza kusema kifupi sana kuwa wamefika hapa walipo kwa mazingira yaliyowalazimishwa kuwa nayo. 1963 kama sisi walipata uhuru na wakawa na independence constitution ambapo Kenyatta alikuwa PM na Queen Elizabeth aliendelea kuwa Head of State. Moja ya tatizo kubwa walilorithi kwenye katiba hiyo ni suala la serikali ya majimbo ambapo wakati huo kulikuwa na majimbo 7 na yaligawanywa kwa misingi ya ukabila. Hilo linaendelea kuwala hadi leo.

1964 Kenya ilifanya mabadiliko makubwa na kuitangaza Kenya kuwa Republic wakati huo ikiwa na vyama vingi. Hata hivyo baada ya kufariki kwa Kenyatta 1978 na Moi kuchukua madaraka,Kenya iliingia katika mfumo wa chama kimoja (de jure single party state) kama ilivyokuwa Tanzania. Kutokana na upepo wa siasa za dunia kubadilika miaka ya 1990. Kama ilivyokuwa kwa Tanzania, Kenya pia waliingia katika vuguvugu za siasa za vyama vingi na madai ya kutaka mabadiliko katiba yao.

Takriban kipindi chote cha kuanzia 1992 hadi 2002 tunaweza kusema kuwa mazingira (siyo kupigana) yalilazimisha Kenya kuwa na reforms nyingi ndani ya katiba yao (clamour reforms) kama ilivyokuwa kwa Tanzania. Vuguvugu hizo za Reform zilisababisha chama tawala cha Kanu kuondolewa madarakani na Kenya kutawaliwa na chama cha NARC chini ya Mzee Mwai Kibaki (2002-2013)

Wakati wa utawala wa NARC hasa mwaka 2003 Kenya ilianzisha majadiliano makubwa ya kikatiba kutokana na mazingira ya wakati huo ikijulikana kama NCC (the National Constitution Conference )ambayo ilikutana Bomas. NCC ilikuja na rasimu iliyoitwa 'Bomas Draft Constitution' ambayo bahati mbaya au nzuri ilikataliwa na Wakenya kwenye kura ya maoni ya mwaka 2005. Ni kama mchakato huo uliishia hapo kama wa kwetu ulivyotulia. Bahati mbaya kwa Kenya, uchaguzi mkuu wa 2007 ulileta machafuko makubwa na wengi kuuwawa. Mazingira haya yaliilazimisha Kenya kufanya mazungumzo chini ya jopo lililojumuisha pia Mzee wetu Mkapa (RIP) na kukubaliana kufanya mabadiliko makubwa ndani ya katiba yao na kuingiza NARA (National Accord and Reconciliation Act). NARA ilimwezesha Raila Odinga kutoka upinzani kuwa Waziri Mkuu na ikaundwa serikali ya pamoja (coalition government). Hatua hii iliipeleka Kenya hadi mwaka 2013 na coalition government hiyo kuvunjika.

Naweza kusema kuwa machafuko ya kisiasa ya 2007 yaliwasukuma wakenya kukubalina na katiba yao mpya ambayo waliipitisha kwenye kura ya maoni ya 2010. Sijui ndiyo tafsiri yako ya kupigana lakini mimi naona ni zaidi nguvu ya mazingira waliyokuwamo. Katiba hiyo imepata tena attempt ya kutaka irekebishwe mwaka jana kupitia mpango wa BBI na ikapitishwa na Bunge. Hata hivyo wiki hii Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali mchakato huo wa marekebisho ya katiba ya BBI. Sijui na huu uamuzi wa mahakama unaitafsiri kuwa ni kupigana?

Niseme tu kifupi kuwa katiba nyingi duniani zinabadilika kutokana na mazingira yanayokuwepo wakati huo zaidi kuliko watu kupigana na kuzidai. Hii ndiyo maana Rais Samia amekuwa akieleza kuwa mazingira ya sasa ambayo aliyekuwa mkuu wa nchi amefariki miezi mitano tu iliyopita siyo mazingira rafiki ya kufanya mabadiliko ya katiba. Ameomba apewe muda lakini bahati mbaya sana CHADEMA wameanza kuleta vurugu ambayo ambayo imetufikisha hapa tulipo. Naomba tuheshimu kauli ya Rais. Mazingira ya sasa siyo mazingira ya kushinikiza katiba mpya. Wakenya uliowataja kama role model wako, hawajapigana kwa ajili ya kudai katiba yao. Tusipikane wala kuleta vurugu kwa kwa ajili ya kudai katiba mpya.
Naona na wewe ni katika wale ambao walikunywa damu ya kijani, unaamini unajua kumbe hujui kitu. Matokeo yake unayoyajua ni ya kukariri tu na historia unayodai kuijua inaeleaelea tu na kuungwaungwa mradi iendane na kile ulichosimuliwa. Na mimi natamani ningekuwa na muda nikupe somo kidogo ila kwa bahati mbaya huo muda sina kwa wakati huu.

Nilishuhudia kuasisiwa kwa TANU mwaka 1954 na pia nilishuhudia kuanzishwa kwa CCM miaka zaidi ya ishirini baadaye. Hivyo nakuomba ukijadiliana na mimi utilie hilo maanani. Siku nikipata muda nitakuelimisha kidogo si niliyosimuliwa bali niliyoshuhudia kwani nilikuwepo yakitokea na jinsi CCM inavyotumia mtaji wa ujinga kung'ang'ania madaraka.
 
Pamoja na mengine ya siasa za EA jamaa kuna albaki yake aluomuazima jiwe wakati kampeni zake sijui kama amemalizia kumlipa kupitua vi tender tender hivi......ìkiwemo parking za kinondoni 2016/7 ......muda mwalim mzuri
 
Seriously hawa jamaa wa mamlaka ya teuzi waanze kuwaangalia diaspora kwenye nafasi serikalini.

Yaani nchi imepatwa na ‘major incident’ polisi watatu wamepoteza maisha, mlinzi mmoja na gaidi (or some crazy gunman) alieuliwa.

Jambo limetokea mchana kweupe, kiongozi wa nchi badala ya kulifariji jeshi la polisi na kutoa pole kwa wafiwa, habari muhimu kutoka Ikulu ni raisi kukutana na Kiongozi wa upinzani kutoka Kenya.

Hivi viazi wengine wanafikaje kuwa mpaka washauri wa raisi wa maswala ya siasa.

Muda wa ku comfort wafiwa na kutoa assurance this is an isolated incident wanatuambia wakati watu wanatupiana risasi mbele ya kadamnasi raisi alikuwa ana chat someone who is a nobody na hiyo ndio habari muhimu kwao.
Walipokufa Askari 4 Benki Mbagala baada ya kuvamiwa na magaidi wa Kibiti Magufuli alienda kuwafariji polisi au familia zao?

Walipokufa Askari 9 Kibiti baada ya kushambuliwa na Magaidi Magufuli alienda kuwaona Askari Au kuzifariji familia zao?

Mbona hukulalamika hapa? Kwa nini ilikuwa sawa kwako kwa upande wa Magufuli na isiwe sawa kwako kwa upande wa Samia?

Acheni chuki na Samia nyie chato gang!
 
Walipokufa Askari 4 Benki Mbagala baada ya kuvamiwa na magaidi wa Kibiti Magufuli alienda kuwafariji polisi au familia zao?

Walipokufa Askari 9 Kibiti baada ya kushambuliwa na Magaidi Magufuli alienda kuwaona Askari Au kuzifariji familia zao?

Mbona hukulalamika hapa? Kwa nini ilikuwa sawa kwako kwa upande wa Magufuli na isiwe sawa kwako kwa upande wa Samia?

Acheni chuki na Samia nyie chato gang!
Chato gang wanatamani nchi hii iongozwe na lile kaburi kuliko mtu mwingine yeyote yule
 
Kweli Dr lowasa anatutesa ni mateso kuazia kuta za ikulu hadi mtaani

Yeye ndie alikua president Leo hii tunaungua
 
Nchi kuongozwa na ubavu... Hapana asee Mungu hakuumba mwanamke ili kutawala bali kumsaidia mwanaume!! Bustani ya Eden hakukabidhiwa mwanamke ni mwanaume na sikwamba Mungu alijisahau.
Nakuunga mkono mkuu, kumbuka dunia haiwezi kwenda sawa na imani yako.

Yaani toka mambo yalipo haribika pale Eden shuguli ndiyo hii unayoiona ya kumpandisha mwanamke kuwa head of anycast..!.
 
Odiga ana maslahi gani na TANZANIA??

Unakutana na mpinzani wa nchi nyingine halafu wako umewapa makosa ya Ugaidi?
1630071172252.png
 
CCM mmechoka kwakweli.

CHADEMA mtwawazushia kila jambo ili mtaishia kushindwa tu.

Bora Mods wamefuta ule upotoshaji na propaganda zenu.
Waliandika ujinga gani mkuu? Wengine hatukupata fursa ya kuuona
 
Unamfananisha Odinga na hawa wapinzani wasaka tonge wa TZ? Odinga ni mwanasiasa mashuhuri zaidi A. Mashariki na kati, anahitaji heshima yake!! TZ hamna upinzani serious wa Rais kubother kukutana nao, wapinzani wa TZ ni wa kuwapuuza
Nani kakudanganya? Hata Roma haikujengwa kwa siku moja. Muda una majibu
 
Walipokufa Askari 4 Benki Mbagala baada ya kuvamiwa na magaidi wa Kibiti Magufuli alienda kuwafariji polisi au familia zao?

Walipokufa Askari 9 Kibiti baada ya kushambuliwa na Magaidi Magufuli alienda kuwaona Askari Au kuzifariji familia zao?

Mbona hukulalamika hapa? Kwa nini ilikuwa sawa kwako kwa upande wa Magufuli na isiwe sawa kwako kwa upande wa Samia?

Acheni chuki na Samia nyie chato gang!

Kwanza hakuna sehemu nimemtaja raisi, nimelaumu washauri wakee.

Pili matukio ya Kibiti hayakutokea mchana wa saa sita tena kwenye moja ya barabara kuu na mashuhuda luluki.

Tatu timing ya tukio na mkutano wa raisi; yaani pole inatolewa kupitia Twitter, Ikulu mawasiliano inaona habari muhimu ya siku ni mkutano wa raisi, TBC aioni umuhimu wa kumpa raisi kutoa neno.

Anyway sie ‘wale twaruka, priiii’ sasa hivi sijui tuko wapi.
 
Back
Top Bottom