Iko wapi thamani ya ndoa tunazofungishwa rasmi ikiwa sheria haiwezi kuzilinda?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,931
49,623
Salamu nyingi kwenu wadau

Nimekuwa najiuliza sipati majibu kuhusu kulazimishana kufunga ndoa rasmi zinazotambulika na Serikali lakini hazipewi thamani inayostahili na sheria.

Utakuta mtu kaingilia ndoa ya mtu na kafumania na ushahidi juu lakini ukienda kushtaki mahakamani mtuhumiwa hapewi adhabu yeyote ya maana kwa kosa la kuingilia ndoa ya mwenzie. Matokeo yake watu wanajichukulia sheria mkonono na kujikuta licha ya kuumizwa kihisia wanaumizwa zaidi kwa kuishia jela.

Mbaya zaidi sheria hizi hizi ambazo hazilitambui kosa la kuingilia ndoa ya mwingine inapokuja kutalikiana sheria inasimamia mgao sawa wa mali hata kama zilichumwa na mmoja wa wanandoa.

Kama sheria/Serikali inakomalia mgao sawa wa mali ilipaswa pia iilinde ndoa husika kwa kutoa adhabu kali kwa mtu atakayeingilia ndoa ya mwenzake.

Karibuni kwa michango
 
Back
Top Bottom