Iko wapi tanzana mpya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Iko wapi tanzana mpya?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by IsayaMwita, Dec 26, 2010.

 1. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2010
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hakika, Hakika najua kwa wale wapiganaji tumebaki midomo wazi, hatuwi twende wapi! dunia haitutaki tena, Matumaini yamepotea ghafla........, sijui tunatokaje hapa tulipofikishwa na akina Wa 16, Maralia Sugu na wengineo wengi wanao faidika na mfumo huu.

  Ndoto na njozi zetu zinaendelea kufifia kila kukicha, hata wale wapiganaji tuliowaamini nao wameanza kuturuka, kia kukicha ni mchanganyiko mtupu.

  Ndugu
  zangu wapenda mabadiiko vita hii sisi tu washindi ni jambo la muda ukitimu ishallah tutashinda tunaelewa mfumo unalazimisha (CCM) kututawala na hata kuwanunua wale tunaoamini katika mabadiliko.

  Natoa ushauri kwa watanzania wapenda mabadiliko.

  1. Tujiepushe na Mijadala isiyokuwa na tija ndani ya (JF)Jamvi hili.

  2. Tutumie akili sana kama tutaweza kuwatambua wale wanaotaka chama cha CHADEMA kipoteze mwelekeo.

  3. Popote tulipo(wapenda mabadiliko) Tanzania tuwaelimishe bibi, babu, mama zetu, dada zetu, wadogo zetu kuwa wezi wetu ni C**, Kisha tuwaambie wadai Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kwa nguvu zote.

  4.Mwisho tuwaabie kuwa Rais wetu ni Dr. Slaa kama si wizi wa hawa jamaa tungenunua bati kwa sh 5000, cement kwa sh 5000. hivyo basi umasikini wao ni kwa sababu ya .....

  swali la kujiuliza wewe mpiganaji

  Ni kwa jinsi gani utahakikisha kuwa Tanzania mpya inapatikana 2015?

   
 2. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu, vitabu vitakatifu vinasema 'watakao vumilia hadi mwisho ndio watakao okoka', hvyo wapiganaji wanaokata tamaa hao si wapiganaji, kwani kila zuri lina ghalama zake, sasa wao wanataka mazuri siku moja na bila gharama.

  Tusife moyo kwani wokovu unakaribia, CCM watambte kuwa hata kama jogoo hatawika lakini asubuhi lazima itafika.
   
 3. n

  niweze JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wengi Tuna Nguvu Kubwa ya Kuwaeleimisha Watanzania Kuhusu Hii Katiba na Kuhakikisha Haya Mabenki na Nchi Zingine Umoja Wa Mataifa Kulazimisha CCM Kuwapa Wananchi Wake "Katiba ya Kutetea Haki kwa Wananchi" Hakuna cha Negotiate Here. Tukipata Katiba Tutawapa Mahakama na Vyombo Vyetu Nguvu ya Kufuatilia Maovu Yote Kwenda Mbele na Kuondoa Madaraka kwa Viongozi wa Siasa Hasa Mafisadi-CCM. Wananchi Tujue Moja Tunapigania Haki za Familia Zetu na Nchi Nzima na Hasa Wale Wasio Jiweza na Kuonewa Kila Siku. Wananchi Lazima Tuelewe Hili Kwamba Wananchi Wote Waliopoteza Maisha Mahospitalini kwa Sababu ya Kukosa Dawa Kisa Kiongozi Kaiba au Wananchi Ambao Wanakosa Kazi Baada ya Kusoma Vyuoni kwa Sababu Viongozi Hawajui Kutafuta Jinsi ya Kujenga Uchumi au Wale Wananchi Wanaolipa Kodi kwa Kufuata Sheria Wakati Mafisadi Hawalipi na Kuendeleza Utajiri wa Uongo au Wananchi Wanaoshindwa Kwenda Mashuleni au Vyuoni kwa Sababu Mikataba ya Wizi Migodini na Makampuni ya Nchi. Tunataka Kupigana kwa Ajili ya Nchi Yetu Hizi Ndizo Sababu na Wale Wenzangu Wakaa Kimya, Huu Sio Utanzania.

  "Nchi Haiwezi Kujengwa au Kubadilishwa na Wapiganaji Wachache, CCM Wanajua Hili na Wanataka Watanzania Tuwe Wapiganaji Dhaifu Waendelee Kulimaliza Taifa Letu"
   
Loading...