Iko wapi SIRI NZITO ya upinzani iliyopasuliwa jana na CCM pale Jangwani?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Labda mie mzembe, na uzembe huu umechukua sura mpya hasa kukengeuka katikati ya mambo makuu yanayohitaji umakini mkubwa!

Niliambiwa na kuona kwa macho mabango mengi kila pembe ya jiji la Daslamu mfano (feri kigamboni) yasemayo kuwa Mkutano wa CCM jana pale jangwani ungepasua kile kinachoitwa SIRI NZITO ya UPINZANI (CHADEMA)

Ikanilazimu niweke kampi Jangwani japo sikuvaa nguo ya rangi ya mkoloni huyu mweusi,

Mda ulipowadia nikatega sikio kwa minajiri ileile ya kusikia SIRI NZITO ya upinzani, badala yake nilisikia taariza za mawaziri juu ya utendaji wao na ahadi za kipuuzi za eti "barabara za juu zitaanza kujenzi siku si nyingi" na "mabomba ya maji yatatoa maziwa"

Kwa ujumla sikusikia chamaana kwa mwananchi wa Tanzania zaidi ya wanasiasa hawa kuzidi kuwadhihaki wa tz tu!

Inawezekana siri nzito zenyewe ni ule upokeaji wa kadi feki na wanachama feki wanaojiita wa CHADEMA

Naomba kufahamishwa SIRI NZITO za Upinzani zilizopasuliwa na CCM pale jangwani ni zipi?
 
Wameishiwa. Walilazimishwa kwenda Jangwani kuwadanganya Watanzania. Wameshindwa kudanganya kwa sababu Watanzania wa leo siyo wale wa jana au juzi.
 
Chadema ni kama jina la---lipitalo yote hivyo ccm na kikao chao kile bila kutanguliza jina hilo kuu CDM! wanajua hamna kitu ndiyo maana nao wanaanza kupiga nduru,za kitoto eti kupimana ubavu na umma!
 
Viongozi wa ndani ya ccm walikuwa wanaiita hiyo ni operation jaza uwanja na wengine ni movement for jaza uwanja na hii operation ilikuwa na fungu kubwa zaidi ya shs milioni 100 na ndio maana wanasema magufuli na mwakembe wapo kwasababu wanajua wananchi wanawapenda kidogo kwahiyo watakuwa chachu kwenye hiyo operation
 
Labda mie mzembe, na uzembe huu umechukua sura mpya hasa kukengeuka katikati ya mambo makuu yanayohitaji umakini mkubwa!

Niliambiwa na kuona kwa macho mabango mengi kila pembe ya jiji la Daslamu mfano (feri kigamboni) yasemayo kuwa Mkutano wa CCM jana pale jangwani ungepasua kile kinachoitwa SIRI NZITO ya UPINZANI (CHADEMA)

Ikanilazimu niweke kampi Jangwani japo sikuvaa nguo ya rangi ya mkoloni huyu mweusi,

Mda ulipowadia nikatega sikio kwa minajiri ileile ya kusikia SIRI NZITO ya upinzani, badala yake nilisikia taariza za mawaziri juu ya utendaji wao na ahadi za kipuuzi za eti "barabara za juu zitaanza kujenzi siku si nyingi" na "mabomba ya maji yatatoa maziwa"

Kwa ujumla sikusikia chamaana kwa mwananchi wa Tanzania zaidi ya wanasiasa hawa kuzidi kuwadhihaki wa tz tu!

Inawezekana siri nzito zenyewe ni ule upokeaji wa kadi feki na wanachama feki wanaojiita wa CHADEMA

Naomba kufahamishwa SIRI NZITO za Upinzani zilizopasuliwa na CCM pale jangwani ni zipi?

Naona toka jana unahangaika kutafuta cha kuandika usikipate.

Baadhi ya siri tulizozisikia jana ni hizi hapa, ni kuwa wapinzani hususan chadema ni waongo, wanadanganya wananchi kuwa wao ndio wenye hoja ya CAG kumbe ni Kikwete aliyepeleka hiyo hoja bungeni. Tukasikia kuhusu wazee wa Mbowe walivyo "shirikiana" na Mbowe ana wakufuru. Tukasikia kuhusu chadema wanavyoiba hoja mpaka za kamati zinazotolewa na CCM na wao wanakimbilia kuwaita waandishi wa habari zionekanae ni zao.

Duh, tukasikia kuwa sasa chadema mnafanya maandamano kwenye barabara za lami (mkutano mwingine basi mkafanye sehemu hamna lami ili mumuweze Magufuli).

Isitoshe tukasikia kuwa mnapewa fedha na wazungu na huku mnawachangisha fedha wananchi kwenye mikutano yenu. Jee, mnawaambia kuwa mnaletewa fedha ngapi na wazungu? kwi kwi kwi teh teh teh.
 
Angel mzima, ccm bila kuitaja chadema kwa kila jambo habari yao haina mshiko lakini ukiweka neno chadema angalau inajadiliwa...
Ni kweli mkuu ndio maana wakina mafilili zomba ritz rejao au Tume ya katiba wakileta thread lazima wataje CDM kwa namna moja au nyingine ili thread zao zichangiwe lasivyo zitaishia hewani
 
Kwani hujawajua kuwa ccm hawana tena chakuwambia wananchi?manake wamemaliza maneno yote na yote mwananchi mwenye akili na utashi wa kupambanua mambo hawezi kamwe shawishika na ccm. Wanaoshawisha ni wale wajinga au wale wenye maslai huko. WAMEBAKIA KUKOPY KILA KITU KINACHOFANYWA AU KUONGELEWA NA CHADEMA YA WATANZANIA.
 
ccm wamejaa ghiliba na ulaghai
547539_3704741529886_1253515703_n.jpg
 
Wameishiwa. Walilazimishwa kwenda Jangwani kuwadanganya Watanzania. Wameshindwa kudanganya kwa sababu Watanzania wa leo siyo wale wa jana au juzi.

Kilomita zaidi ya 11,000 za lami wakati wa Kikwete tu.

Wanafunzi zaidi ya million 8 wanaosoma wakati wa Kikwete tu.

Vyuo vikuu wanafunzi zaidi ya 130,000 wakati wa Kikwete tu, kabla yake hawafiki hata 50,000.

Barabara za Dar, mkaoneshwa hapo hapo Jangwani ukitazama kulia ji highway la 8 lanes linajengwa, ukitazama kule ya Yanga jibarabara jipya linaenda mpaka Ubungo.

Treni za mjini kuanza mwaka huu huu, Mwakyembe.

Huko kusini mlikokwenda, hamjawahi kuonekana kwa ajili ilikuwa hakuna barabara, sasa hivi lami bado kilomita 20 tu kumalizika.

Jana umewashuka magwanda ya khaki.
 
Naona toka jana unahangaika kutafuta cha kuandika usikipate.

Baadhi ya siri tulizozisikia jana ni hizi hapa, ni kuwa wapinzani hususan chadema ni waongo, wanadanganya wananchi kuwa wao ndio wenye hoja ya CAG kumbe ni Kikwete aliyepeleka hiyo hoja bungeni. Tukasikia kuhusu wazee wa Mbowe walivyo "shirikiana" na Mbowe ana wakufuru. Tukasikia kuhusu chadema wanavyoiba hoja mpaka za kamati zinazotolewa na CCM na wao wanakimbilia kuwaita waandishi wa habari zionekanae ni zao.

Duh, tukasikia kuwa sasa chadema mnafanya maandamano kwenye barabara za lami (mkutano mwingine basi mkafanye sehemu hamna lami ili mumuweze Magufuli).

Isitoshe tukasikia kuwa mnapewa fedha na wazungu na huku mnawachangisha fedha wananchi kwenye mikutano yenu. Jee, mnawaambia kuwa mnaletewa fedha ngapi na wazungu? kwi kwi kwi teh teh teh.

Ulichokiandika ni kipi?manake ingekuta nakuona labda nafkiri your sound is like zile wanawake wakiwa saloon wanaongea mwishoni utaskia wakicheka sasa wewe unachekaje kwenye serious matters?acha umbea na kwa miaka 50 ya uhuru barabara tunazoziona hazifanani ni bora tusingepataga uhuru manake wakoloni weupe waliacha lami na wangendelea mpaka vijijina pamoja na miji yote tungejengewa barabara maana wangetujali zaidi si kutu exploit to the maximum kama mkolon huyu mweusi tuliyenaye sasa hivi. EMBU ACHA UBWEGE MKUU.
 
Mbona Chadema mmekuwa waoga? Ni haki ya watazania kusikiliza sera za vyama vyote waachieni wenyewe waamue pumba ni ipi na mchele ni upi. Mara ooh wameleta watu kwa malori mmeishiwa sasa semeni wameleta watu kutoka Kenya

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Sasa hata ukimuuliza mwananchi wa kawaida magufuli Tibaijuka na mwakembe walikuja kufanya nini pale wala haijulikani au kusema barabara zitatengenezwa wakati lazima zitaonekana ndege na reli zitafanya kazi wala Hilo halihitaji lielezewe pale CDM square(zamani jangwani ) kwasababu litaonekana na nimoja ya ahadi zilizotolewa na magamba walichokuwa wanafanya ni ushambenga
 
Ulichokiandika ni kipi?manake ingekuta nakuona labda nafkiri your sound is like zile wanawake wakiwa saloon wanaongea mwishoni utaskia wakicheka sasa wewe unachekaje kwenye serious matters?acha umbea na kwa miaka 50 ya uhuru barabara tunazoziona hazifanani ni bora tusingepataga uhuru manake wakoloni weupe waliacha lami na wangendelea mpaka vijijina pamoja na miji yote tungejengewa barabara maana wangetujali zaidi si kutu exploit to the maximum kama mkolon huyu mweusi tuliyenaye sasa hivi. EMBU ACHA UBWEGE MKUU.

Kilomita zaidi ya 11,000 ni wakati wa Kikwete tu. Sasa jiulize Nyerere na Baba'ke Mbowe wakishirikiana awamu ya kwanza walifanya nini kwenye barabara? na waliomfata wote walifanya nini, akiwemo na Slaa CCM? iweje Kikwete tu kwa miaka 7 aweze kilomita zaidi ya 11,000 ambazo ni zaidi ya zote zilizokuwepo kabla yake?
 
Mimi naomba kuuliza. Hivi nini maana ya "waziri wa uratibu na sera"? Nachanganywa sana na cheo cha Waziri Wassira. Kwanini asiitwe wa waziri wa kupambana na Chadema? Maana sioni sera wala uratibu katika yote anayoyasema.
Mfano kwenye kupindi cha dk 45 ITV tarehe 3/6/012 alitumia muda mwingu kuisema CDM badala ya kujibu maswali aliyoulizwa. Jana Jangwani badala ya kuelezea mambo ya sera na uratibu kaongea mambo ya baba yake na Freeman Mbowe alivyopigania uhuru na jinsi Freeman anavyo "kufuru"(sikuelewa mantiki ya neno hilo mahali pale), au inawezekana hizo ndio SIRI tulizoambiwa zitapasuliwa?
 
Mbona Chadema mmekuwa waoga? Ni haki ya watazania kusikiliza sera za vyama vyote waachieni wenyewe waamue pumba ni ipi na mchele ni upi. Mara ooh wameleta watu kwa malori mmeishiwa sasa semeni wameleta watu kutoka Kenya

Chama
Gongo la Mboto DSM

Hawana hoja, hoja zao ndio hizo.

Badala ya kuwaambia watu kama Kikwete kajenga KM 11,000 za lami sisi mpango wetu huu hapa wa kujenga KM 24,000 za lami kwa miaka 5. Hawana. Na Slaa alipojaribu aliwaambia atawapa simenti ya bure. Tazama pumba hizo.
 
ccm haina sera bali wanawsiwasi na M4C kwa kifupi wamelowana ile mbaya hawana kitu kipya kila wakati CDM ni aibu kwa cham kikongwe kama ccm kuhangaika na chama changa kisichokuwa na dola.
 
Back
Top Bottom