Iko wapi ndege ya Rais iliyotulisha nyasi za Mramba?

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,558
25,322
Mnijuze wakuu maana sijaisikia ikikata mawingu wala kuiona angani, natamani kujua ilipo maana nimeiona ya mgeni wetu wa makinikia nikatamani kujua ndege yetu yenye gharama ya uhai wa watu wetu ilipo.
 
Mwache raisi mstaafu apumzike!! Vinginevyo hakikisha post yako haiongelei raisi
 
Sasahivi makinikia ndo habari ya mjini, hayo mengine yalishapita, usifukue makaburi
 
Ndugu wa jamvi, najaribu kuwaza kama naota. Miaka kadhaa iliyopita watanzania tulikula nyasi ili mtukufu Rais wetu anunuliwe ndege bora na ya kisasa kabisa. Tangu inunuliwe mbona hatuoni inatumika kama ilivyokusudiwa.

Kama haina matumizi ikulu Kwanini ATC wasiichukue badala ya kuhangaika na hizi bombadia?
 
Ndugu wa jamvi, najaribu kuwaza kama naota. Miaka kadhaa iliyopita watanzania tulikula nyasi ili mtukufu Rais wetu anunuliwe ndege bora na ya kisasa kabisa. Tangu inunuliwe mbona hatuoni inatumika kama ilivyokusudiwa.
Kama haina matumizi ikulu Kwanini ATC wasiichukue badala ya kuhangaika na hizi bombadia.,??
Unataka kupimwa mkojo na uitwe mchochezi upone haraka Lissu
 
Ile Ndege ipo pale Kijiji cha Makumbusho ya Taifa imekuwa kivutio kwa Watanzania wote wajinga waliokula nyasi.
 
Sina hakika kama ndege hiyo ni nzima waijuao watufahamishe kama inaruka
 
Usalama wa raisi ni muhimu haiwezi kutumika kiraia hakuna nchi duniani inafanya hivo
Iko wapi sasa. Maana kwenye takwimu Haioneshi hata jk aliitumiaje nayeye ndio alikuwa bingwa wa kusafiri. Pili Ile ni ndege kama zingine na imeligharimu taifa mabilioni ya fedha,. Kama haitumiki Kwanini isiuzwe tugawane chenchi, kama ilivyotokea chenchi ya rada???
 
Back
Top Bottom