Iko wapi CHADEMA ya Operesheni Sangara na M4C?

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,312
Siioni kabisa, ile Chadema iliyoenda kupiga kambi Kanda ya pwani zaidi ya wiki moja.

Ile Chadema iliyosambaa Kanda zote kuelemisha Wananchi kuhusu Ufisadi na maovu ya ccm kwa ujumla.

Ile ya Lema, Mnyika, Mdee, kwa upande mmoja Sugu,Silinde,Msigwa kwa upande mwingine. Lissu, wenje na wengineo.

Ile ya viongozi wenye upeo toka makao makuu,Pr.Safari, Pr.Baregu na wengineo.

Ile ya vijana makamanda tofauti toka idara tofauti makao makuu.

Kweli leo Chadema ni ya kupelekwa ikulu na akina Sumaye, Masha, Msindayi na Mahanga?

Wako wapi makamanda wa ukweli tuliowazoea wananchi, waliokipaginia chama kwenye jua na mvua usiku na mchana.?

Najua mtasema wengi wapo bize na kampeni kwenye majimbo yao.

Lakini binafsi naamini Lema, Lissu alieashinda asilimia tisini ya serikali Za mitaa, Silinde ambae wananchi wake wanaimba Chadema hadi usingizini, Sugu ambaye ni Rahisi wa Mbeya, Mdee mwanamke shujaa wa siasa za upinzani Tanzania na wengineo.

Hawawezi kushindwa kupoteza siku mbili kwenye majimbo yao na kumnadi Lowassa kwenye mbio za urais.

Poleni makamanda najua wengi wenu mnamadukuduku mioyoni mwenu ila ni ngumu kusema kwa kuogopa kuitwa wasaliti.

Kwa hatua ilipofikia Chadema, kilikuwa sio chama cha kutegemea Sumaye awapeleke ikulu wala Masha wala Msindayi hata Lowassa Mwenyewe.!

Bado naililia Chadema yangu ya ukweli na mtetezi halisi wa watanzania sio hawa wasaka madaraka tu.!

Tukutane October 25
 
Nilitokea kuipenda sana Chadema kama chama cha upinzani kilichokuwa mstari wa mbele kupiga vita RUSHWA na UFISADI.
Kilijipambanua vizuri sana ktk harakati zake.
Leo hii sisikii tena kwenye kampeni za Urais za Lowasa namna gani watapambana kudhibiti RUSHWA na UFISADI, kwenye vipaumbele vya lowasa hakuna!!
 
Usijaribu kuonyesha hisia zako mbele ya wenzetu Usishangae wakikuita wewe ni gamba.

Ukweli ndio huo Chadema imehama mstari, makamanda ni kama wamekata tamaa kila mtu anawaza mstakabali wake sio wa chama tena.!
 
Chadema wanasema tatizo si mtu bali ni mfumo,lakini mfumo ni watu,mbowe kauza chama hajakanusha na lowassa hajakanusha kuuziwa demokrasia ndani ya cdm,ikiwa chama ni taasisi ya wananchi aliyeuza hiyo taasisi SIO FISADI? CHADEMA NI CHAMA CHA DEALS NA MAFISADI. KAMA WEWE NI CDM JIBU SWALI HAPO JUU.PUMBAVU NA LOFA WEWE!!!!
 
Kwanini tunaamini Lowasa atasimamia kile tulichopigania kwa miaka mingi ...... Akiwageuka mtalia na nani ..... Hivi kama swala ni Uchadema .....Chadema ni nini .....tukiamua Leo CCM kuiita Chadema na Chadema kuwa CCM bado utaichagua Chadema ..... nini kimetuingia hadi tunamsaliti jemedari wetu aliyesimama na sisi wakati wa jua na mvua ...
 
Huyo jemadari kafukuzwa?
 
Ipo wapi ccm ile. Iliyojinasibu kuvua gamba. Ipo wapi ccm ile ya mangula iliyojitanabaisha kuwafuta uongozi wale wrote waloshinda kwa rushwa.
 
Nakwambia tutamkumbuka dr Slaa daima.mtazungumka weeeee lakkni mwisho wa siku mtarudi kwa Dr Slaa. Na nasema Mbowe atakuwa wa kwanza kupiga magoti kwa Slaa pale Chadema itakapokuwa imepasuka na kusambaratika, na wafuasi sasa kuanza kudai haki zao
 
Yaani pumba tupu ...hao uliowataja wote ni wagombea ubunge na wana kazi maalumu ya kuzunguka na chopa kwenye msjimbo kadhaa kumnadi mgombea urais hata ratiba ya chama hamuijui then mnaajiita chadema......hamjalazimishwa c muondokee
 
Kwanini tunaamini Lowasa atasimamia kile tulichopigania kwa miaka mingi ...... Akiwageuka mtalia na nani ..... Hivi kama swala ni Uchadema .....Chadema ni nini .....tukiamua Leo CCM kuiita Chadema na Chadema kuwa CCM bado utaichagua Chadema ..... nini kimetuingia hadi tunamsaliti jemedari wetu aliyesimama na sisi wakati wa jua na mvua ...

Lowasa hawezi geuka maana sio mwenyekiti wa chama. Hakigeuka tunamvua uanachama. Kama alivyofanyiwa aboud jumbe pale chimwaga.
 
Very painful ... Watu hawajitambui tena .... Kama wengi wape kwa mtindo huu Muumba wangu anisamehe .....

Huyo dk mihogo alikuwa wapi siku zote za mchakato wa kuchukua fomu. Ulitaka tuendelee kumsubiri. Wacha aongozwe na mkewe.
 
Very painful ... Watu hawajitambui tena .... Kama wengi wape kwa mtindo huu Muumba wangu anisamehe .....
Kifupi kama nchi tumepoteana, hatuhoji wala kujenga hoja tena ila ni mwendo wa ushabiki tu.!
 
Huyo dk mihogo alikuwa wapi siku zote za mchakato wa kuchukua fomu. Ulitaka tuendelee kumsubiri. Wacha aongozwe na mkewe.
Wenye akili wanajua umuhimu wake, punguza ushabiki changanua mambo kwa hoja.
 
Nakwambia tutamkumbuka dr Slaa daima.mtazungumka weeeee lakkni mwisho wa siku mtarudi kwa Dr Slaa. Na nasema Mbowe atakuwa wa kwanza kupiga magoti kwa Slaa pale Chadema itakapokuwa imepasuka na kusambaratika, na wafuasi sasa kuanza kudai haki zao
Hawawezi kukuelewa zaidi watakuita wewe gamba.
 
Back
Top Bottom