South
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,514
- 5,139
Nimesikitishwa sana na taarifa za kuvamiwa kwa wanachama wa CUF na kujeruhiwa kwa baadhi ya waandishi na wanachama waliokuwepo ktk mkutano huo. Siku kadhaa nyuma mkuu wa mkoa alimhakikiashia mh rais kwamba hali ya usalama na utulivu ktk jiji la Dar es Salaam kwa ujumla ni nzuri. Swali la kujiuliza hao wavamizi wamepitaje na kufanya tukio la kikatili kama hilo ikiwa hali ya ulinzi na usalama wa jiji upo? Je kuna baraka za utawala kwa tukio hili? Sidhani kama tukio kama hili linaweza kutokea ktk mkutano wa chama tawala, tuliona hali ya ulinzi ilivyokuwepo Dodoma. Tusifarijiane kwamba kwa sasa usalama upo kama mnavyotaka kutuaminisha, hali sio nzuri na itakua mbaya matukio ya ajabu aina kama yakiendelea na ninyi kuja haraka ktk media na kutudanganya.
South
South