Iko Siku Tutaamka na Kusikia Wananchi Wameamua Kujichukulia Ikulu na Kuiongoza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Iko Siku Tutaamka na Kusikia Wananchi Wameamua Kujichukulia Ikulu na Kuiongoza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Nov 11, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Leo hii, nimesoma habari kuwa Wafanyakazi wa TRL, wameamua kujichukukulia majukumu ya kuendesha na kuongoza TRL baada ya Rites kutoa notisi ya siku 60 kujitoa na Serikali kukaa kimya bila kutoa kauli inayoeleweka.

  Ukimya wa Serikali ya Tanzania katika mambo ya msingi na kutatua kero za Wananchi unatisha!

  Uongozi wa Serikali ya Tanzania inaelekea umelala usingizi wa Pono kama si kuamua kuwa haujali yule mpiga kura aliyeipa Serikali hii dhamana ya kuliongoza Taifa la Tanzania.

  Anzia Ajira, Elimu, Afya, Usalama wa Wananchi, Maji Safi, Umeme, Msongamano wa Magari, kukosekana kwa Uwajibikaji, kuongezeka kwa Uhujumu na Ufisadi, ni kero kila kona na napenda kukataa na kuipinga kauli yangu ya wiki tatu zilizopita kuwa Tumeridhika na dhiki, tabu na mateso.

  Ujasiri wa wafanyakazi wa TRL, hata kama tutadai eti haukuwa wa halali, naupongeza kwa kuwa tangu awali, Serikali yetu ambayo ni mbia mkubwa wa mkataba huu wa Shirika la Reli, imefumbia macho malalamiko ya Wananchi na hata mradi wenyewe wa Uwekezaji TRL haukufanyika kwa unyoofu pamoja na Serikali kuelezwa.

  Wakati unaanza wadia ambapo Wananchi wanaamua kujichukulia hatua mkononi. Wanaamua kufanya kazi na kuchukua dhamana ya kuongoza na kuendesha nchi yetu kutokana na kukosa uaminifu na uvumilivu kutoka kwenye kauli hasi za Viongozi na Serikali.

  Inasikitisha, inatisha na inadhalilisha, lakini itakapobidi, sitashangaa kusikia siku moja asubuhi kuwa Wananchi wamejitwalia Ikulu na Bunge na kuamua kujiongoza kwa matakwa yao wenyewe kutokana na kuchoshwa na Viongozi wazembe na Serikali isiyojituma wala kuthamini dhamana iliyopewa kuongoza Taifa la Tanzania!

  Sichochei machafuko au watu kuvunja sheria, lakini ikiwa leo haki ya Mtanzania inawekwa majaribu kutokana na kiburi, uvivu na dharau kutoka kwa wale walioaminiwa kuongoza na kulipeleka Taifa letu katika njia iliyo sahihi, Mchungaji hatashangaa, wala kuwasikitikia wale watakaoondolewa madarakani kutokana na uzembe wao!
   
 2. 911

  911 Platinum Member

  #2
  Nov 11, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Mkulu Rev,heshima mbele.Kile unachokiona/kifikiri kwa Tanzania ya leo ni ndoto,tena ya mchana.I mean wananchi wepi wa kuamua hayo?Hao waliowapokea kina Lowasa na Chenge kama mashujaa.Majority ni kwamba wapo usingizini na huenda wasiamke in a near future.Umenikumbusha wimbo flan tulikuwa tunauimba kwenye mchakamchaka kuwa'...jua lile literemke mama....'.
   
 3. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  kwakweli kwa bongo ni kazi, ila hakuna marefu yasio na ..........ipo siku kitawaka tu usiwe na haraka.bado bongo tunaogopa ogopa risasi hivi,,ila zitazoeleka , kwani hukumbuki tulivyokuwa tunaogopa polisi zamani sikuhizi je...so worry not baby
   
 4. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Tusubiri tamko la serikali, ndo litatupa picha kamili juu ya jambo hili. Si ajabu kusikia inapiga magoti kwa wahindi na kuwasaliti watanzania.
   
 5. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Nimegundua kitu kimoja...kama kweli macho yangu yana machozi basi bora niyaache nije kujililia mwenyewe maana kila mtu ana kila sababu ya kubeba mzigo wake.
   
 6. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ngoja nikusiadie......!...aiyaiyaaa iya iya mama!....mwezi nao uteremke mama......nyota nazo ziteremke mama..aiyaiyaiya iya mama.....!

  Baba Paroko....! ''Liwalo na liwe kila mmoja na lwake''!
   
 7. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  We all wish wish wish wish......and wish......and wish.....and write....it ends here...
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Nov 11, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  poleni kwa maumivu makali yasababishwayo na mfisadi wa nnchi hii, poleni, iko siku, yana mwisho haya. Tusikate tamaa.
   
 9. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  REV huchochei machafuko. Wanasiasa na viongozi wetu wabovu ndio watakaotuletea machafuko. Wala usijitetetee.
   
 10. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  At least we write sir. Wanasoma sana humu. Ila wanatuchosha haswa!
   
 11. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #11
  Nov 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,942
  Trophy Points: 280
  Rev, jogoo akiwika uje kumepambazuka. TRL ni jogoo awikaye kulipopambazuka, uliyosema ni sahihi kabisa. Kwa mwendo huu wa usingizini usishangae siku moja watu wakaichukua hiyo Ikulu na Bunge lao na kuendesha watakavyo kuliko hii style ya mipasho na taarabu zisizo na melody
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Nov 11, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Rev. I dare anyone in Tanzania to do so;
  Tunashindwa kumsaidia jirani hata akiingiliwa na vibaka
  Tunashindwa kutetea haki za watoto na wanawake
  Tunashindwa kumuondoa afisa mtendaji bazazi
  Tunashindwa kumuondoa mwalimu mbakaji
  Tunashindwa kumuondoa mchuna ngozi

  Tunashindwa kujiandikisha kupiga kura
  tunashindwa kuhoji matumizi ya fedha za wafadhili
  tunashindwa kuhoji lead time iliyotumika kuleta mafuta ya IPTL tunajua wiki tatu huwezi kuagiza, kupaki na kusafirisha
  Tunashindwa kuhoji kikao cha bunge cha november 2009 kimedeliberate nini
  tunashindwa kudai kodi zinazokatwa isivo na utaratibu

  Tunashindwa kuhoji mapato ya madini, ardhi, misitu na maliasizi nyongine
  tunashindwa hata kuhoji wanaopiga raia
  Tunashindwa kuhoji haki za mama njamzito clinic
  Tunashindwa hata kusaidia usafi wa mitaa yetu
  Tunashindwa hata kusaidiana basic needs

  Tunajali mazishi kuliko uzazi salama
  Tunajali harusi kuliko elimu
  Tunajali send of kuliko kupokea bwana harusi
  tunajali kitchen party kuliko misa za shukrani

  Tunashindwa hata kumzuia askari asimpige polisi
  tunashindwa kuhoji baadhi ya wabunge mafisadi
  tunashindwa kuhoji nguvu ya rushwa
  tunashindwa kuhoji uhalali wa uwepo wa mawaziri


  I dare anyone kuchukua nchi... NINAOMBA NIWE HAI NA NIBEBE BENDERA ZA WANAMAPINDUZI AU NGOMA ZA SHEREHE

  Peace
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Nov 11, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  mkataba ulishapigiwa kelele muda mrefu na waheshimiwa lakini ikulu wanakwambia mkataba safi pamoja na kuambiwa kasoro kibao.........tatizo hata rais mwenyewe huwa anahusishwa kwenye mikataba yote hewa na huwa anajua kuwa mkataba hauna maslahi ila kwa kuwa kauli mbiu ya chama chetu ni chukua chako mapema hivyo rais anajitahidi angalau ajichotee kupitia mikataba hii mibovu kwa kutumia watu wengine na ndio maana hawezi kuwawajibisha,kama isingekuwa hivyo angekuwa anachukua hatua fasta ili kunusuru wananchi wanaoteseka bila sababu......
  Nchi iliisha oza,mwl.nyerere alishatutadhadharisha kuhusu lundo la watu waliokuwa wakiutaka yongozi wa juu wa nchi kwa udi na uvumba....sasa dhambi aliyosema itatufuata kama tukipuuza ushauri wake ndio hiyo tunayoiona sasa..........kwa kweli haya mabo yanakera sana.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Nov 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  HIvi pale watu wa Tanesco walipojifanya wanaleta mapinduzi dhidi ya wakaburu serikali ya Mkapa ilifanya nini?
   
 15. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #15
  Nov 11, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  mwanakiji wawekezaji wale waliingizwa ofisini kwa mtutu wa Bunduki, walikula wee wakashiba, kisha wakaondolewa, lakini ujumbe ulifika.
  Pamoja na nguvu zao, kama umma wote utaamka kweli SMG zao hazitzfua dafu, kwani Suharto wa Indonesia hakuwa na Bunduki, aah wapi, watu wakichoka ni hatari.
   
 16. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #16
  Nov 11, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Tunamuhitaji mtu kama Kinjeketile Ngw'ale ambaye atatutia ujasiri kuwa risasi zitageuka maji.
  Nadhani wananchi wameanza kuzoea risasi - ebu kumbuka matukio ya wananchi kuvamia vituo vya polisi; si risasi zinapigwa lakini wananchi wanasonga mbele hadi walilokusudia litimie!
  Iko siku kweli na si mbali sana.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Nov 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,882
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280
  Naam inawezekana kabisa siku hiyo tukaiona. Maana watu wamevumilia vya kutosha na uvumilvu una kikomo chake. Kulikuwa na nafasi chungu nzima za kukatisha mkataba na matapeli hawa toka India ambao na wao tuliwaita "Wawekezaji" lakini Serikali ya Kikwete kama kawaida yake ikafumbua macho kasoro mbali mbali zenye uzito wa hali ya juu ambazo nyingi zilikiuka vipengele mbali mbali vya mkataba na matapeli hao.

  Hongera Wafanyakazi wa Reli kwa kutuonyesha njia Watanzania ya kurudisha hadhi ndani ya nchi yetu labda siku za usoni mikakati yenu inaweza kabisa kutumika katika kuchukua Ikulu yetu toka mikononi mwa papa fisadi Rostam Aziz na kundi la mafisadi wenzie.
   
 18. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #18
  Nov 11, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Rev. Watanzania bado hawana ujasiri huo. Mfano ni wa Walimu ambao wale waliolipwa madai yao wameshindwa kushirikiana/kushikamana na wenzao katika kuiadabisha Serikali ili isirudie tena mchezo wa kuwatumia walimu (na wananchi wengine) bila kujali maslahi na maisha yao. Wafanyakazi wa Kiwira nao ni mfano mwingine; walisahau machungu yote walipoambiwa na Ngeleja kwamba watalipwa malimbikizo ya mishahara yao na ajira zao zitaendelea k.k. Wakaamua kusukuma gari la Ngeleja na Mwakyembe kwa furaha na kusahau yote!

  Serikali ya CCM inajua udhaifu wa wananchi. Mbinu za kuwaghilibu wananchi na kuwadanganyia 'pipi' zinatumiwa sana na Chama cha Mapinduzi. Bila kujali mustakabali wa wananchi, CCM na Serikali yake wanachukulia shida za wananchi kama mtaji wa kuendelea kuwa madarakani. Inasikitisha sana.

  Wananchi kuamua kujichukulia Ikulu labda inaweza kutokea pale generation ya wazee waliopo madarakani sasa itakapoondoka na kwenda kwa Sir God!
   
 19. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #19
  Nov 11, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Haki huinua Taifa, tunapoendelea kuwanyima Watanzania haki na kuwazereu, mwishowe ni kupigwa mawe!
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Nov 12, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Rev. je hauoni pia kwamba ni sisi ndio tunawapa hawa watawala haki ya kuchukua hta hazi zetu?? what a re we doing from grassroot level??
   
Loading...