Iko haja na hoja ya kupata tafsiri sahihi ya ziara za ufuatiliaji na ukaguzi wa utekelezwaji wa ilani na mikutano ya hadhara

AUGUSTINO CHIWINGA

Verified Member
Apr 23, 2017
214
1,000
Na,
Augustino Chiwinga
0756810804.


Wapotoshaji wa mitandaoni wamekalia kidete ziara za ufuatialiaji na ukaguzi wa utekelezwaji wa Ilani anazofanya Katibu wa Halmshauri kuu ya CCM Taifa-Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole katika mikoa, Wilaya, Kata, Vijiji, Mitaa na Vitongoji mbalimbali hapa nchini wakiziita ziara hizo kuwa eti ni mikutano ya hadhara.

Inabidi tuchore mstari na kutofautisha kazi za msingi za CCM za kuisimamia Serikali ili kuleta maendeleo tarajiwa kwa Umma, na mikutano ya hadhara.Serikali haisimamiwi kwa maneno matupu serikali inasimamiwa kwa vitendo. Serikali iliyoko madarakani ni ya CCM na Ilani inayotekelezwa ni ya CCM, kwa vyovyote vile CCM haiwezi kukaa kando bila ya kukagua na kuisimamia Serikali kwa kufanya ziara za kufuatilia utekelezwaji wa Ilani ambayo ni dira na kiini cha kuwaletea wanachi maendeleo.

Wapotoshaji wanapaswa waelewe kwamba,Chama Cha Mapinduzi kilifanya makubaliano (Mkataba) na Wananchi mwaka 2015 kupitia Ilani yake ambayo imeeleza mambo mengi ambayo CCM inatarajia kuyafanya iwapo wananchi watakipa ridhaa ya kushika dola. Mathalani Ilani hiyo imeelezea mambo mbalimbali kama vile kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama , ujenzi wa Hospitali, Vituo vya afya na Zahanati, nishati ya umeme, miundombinu na kadhalika.
Sasa mwaka 2015 CCM ilipewa ridhaa hiyo na Wananchi ya kuunda Dola baada ya Wananchi kuielewa na kuikubali Ilani yake. Kwa sasa CCM imebaki na deni la kuhakikisha kila kilichoandikwa katika Ilani hiyo kinatekelezwa kupitia Serikali yake iliyoiunda.

Sio dhambi viongozi wa CCM kufanya ziara za kufuatilia utekelezwaji huo.Ili ahadi zilizohaidiwa katika Ilani hiyo ziweze kutekelezeka ni lazima Serikali ya CCM itoe fedha za kuwezesha utekelezwaji wake sasa hapo ndipo kazi ya CCM ya kuisimamia Serikali inapoingia rasmi katika kusimamia fedha hiyo itumike kwa nidhamu na kwa maslahi ya Umma.Kwa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa ya CCM- Itikadi na Uenezi ndiye msimamizi mkuu wa Sera za CCM. Ilani ni sera hivyo anawajibika kutembelea na kuzuru maeneo mbalimbali nchini ili kujionea na kujiridhisha iwapo Ilani na Sera za CCM zinatekelezwa na Serikali haswa ikizingatiwa naye ni mtafiti wa Sera na muandishi wa Ilani ya CCM.

CCM ikikaa kando na kuiachia Serikali ifanye mambo bila ya kusimamiwa, mambo mengi yatakwamwa na wananchi wanaweza kuvunja mkataba huo watakapoona mambo yaliyoandikwa katika IIani hayatekelezwi kama inavyopaswa.
Haingii akilini CCM iahidi maendelo halafu ikae mstari wa nyuma bila ya kuhakikisha iwapo maendeleo hayo yanapatikana na yanatekelezwa na Serikali iliyoiunda. Ni wajibu na lazima CCM ifuatilie, ikague, isimamie, na kujiridhisha kama wale waliowapa dhamana ya kutumikia Serikali wanafuata na kutekeleza Ilani yake.

Huko nyuma CCM ilifanya makosa hayo ya kutofuatilia utekelezwaji wa Ilani na iliharibikiwa sana.CCM Mpya inajiweka karibu zaidi na wananchi na kutatua kero zao kwani imeachana na siasa za kutafuta madaraka bali inafanya siasa za maendeleo. CCM imepevuka sana kipindi hiki haitaki porojo, sasa vyama vingine vikimuona Ndg.Polepole akikagua miradi juani huku akimimika jasho au akinyeshewa na mvua ,wanaiita ni mikutano ya hadhara.Hiyo ni kazi yake hawezi kujifungia ofisini kwake Dodoma bila ya kusimamia utekelezwaji halafu baadae mambo yakiharibika CCM itupiwe lawama na yeye akitazama.

Ndg. Humphrey Polepole hafanyi mikutano ya hadhara bali yeye akiwa msimamizi mkuu wa Sera za CCM Kikatiba, anatembelea maeneo ya miradi (Project Sites) ili kufuatilia na kujiridhisha kama Serikali inatekeleza Ilani na maelekezo ya Chama.Mathalani anapotembelea miradi ya ujenzi wa Zahanati,shule au mradi wa maji, miradi hiyo haitekelezwi mbinguni sehemu ambayo watu hawawezi kuona bali inafanyika katika maeneo wanayoishi watu na muda mwingine unakuta wananchi wamechangia katika kufanikisha miradi hiyo.

Anapokuwa anatembelea maeneo hayo kwa vyovyote vile wanachi watahamasika kumsikiliza, kutoa kero , maoni na changamoto zao kwa sababu wanajua na kufahamu huyo ni kiongozi wa chama chenye Serikali, chama ambacho wao wananchi walikipa ridhaa ya kuongoza nchi. Huo huwezi kuuita ni Mkutano wa hadhara.
Ukibahatika kumsikiliza Ndg. Polepole akiwa eneo la mradi hutomsikia akizungumzia siasa bali huwa anaongea mambo ya kitaalamu na kusisitiza zaidi juu ya nidhamu ya matumizi ya fedha, ujenzi wa kiwango na uharakishwaji wa ukamilishaji wa ujenzi wa mradi husika kwa manufaa ya wakazi wa eneo hilo. Maendeleo hayana vyama, miradi hiyo ikikamilika watatumia watu wa vyama vyote.

Mkutano wa hadhara ni ule mkutano wananchi wanatangaziwa kukusanyika katika eneo fulani la wazi kwa ajili ya kusikiliza hotuba ya kiongozi atakayehutubia hapo.Ziara za Ndg. PolePole huwa huzifanyiwi matangazo yoyote.
Kama ni mikutano huwa anafanya na wanachama wa CCM lakini huwa ni mikutano ya ndani ambapo hujifungia ndani ya kumbi za majengo ya CCM. Mikutano ya ndani imeruhusiwa na hata vyama vingine nao wanafanya mikutano ya ndani tena mingi zaidi kuliko CCM.

Kazi ya kuleta maendeleo ni ya CCM na kazi ya kusimamia na kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa hakika pia ni ya CCM.Tuache siasa nyepesi kwenye maendeleo ya watu. CCM Mpya imejifungamanisha na maendeleo ya Wananchi.
 

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
8,907
2,000
Hoja ya kipuuzi kabisa.

Rais ni Mwenyekiti wa CCM. Polepole aliyeokotwa na Mwenyekiti akiwa hohe hahe, hana mbele wala nyuma, hana ajira wala kipato cha kueleweka, akapewa nafasi ya kuwa mshereheshaji, anaweza kumsimamia Mwenyekiti aliyempa tumaini la maisha?
 

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,601
2,000
Tatizo si lako, tatizo ni njaa na ubashite wako. Kama Bashite ndiye propagandist mkuu wa CCM unadhani sisi wananchi tutakiona nini kutoka wanaccm kama wewe?
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
5,005
2,000
Ilani ipi inatekelezwa na kusimamiwa? ni Ile ya milion 50 kila kijiji, watoto wa kike waliobakwa na kupewa mimba kurudi shuleni,watumishi kupandishwa mishahara au ununuzi wa korosho kusini?
 

papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
3,592
2,000
yaani ukiwa mwanachama wa ccm tuu, akili na uwezo wako wa kufikiri vinapungua, unakuwa mzee wa ndiyoooooo!
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,237
2,000
Tatizo mnawafanya watanzania hawana akili. Mnalazimisha kupendwa! Mnataka msikilizwe na kuonekana nyinyi tu. Inahuzunisha sana mnapotaka kuwarudisha watanzania kwenye mfumo wa hovyo wa chama kimoja. Sidhani kama mtafanikiwa. Wengi hatuifagilii hiyo mivyama yenu.
 

Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,736
2,000
wewe ni mkola muhuni wa kutupwa kule kwani chadema kwanini wasifuatilie ilani yao wakati wanhalmshauri zao mbona wanakamatwa na kuswekwa ndani wewe huna tofauti na matahira mengine yaliyoko huko kwenu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom