Ikiwa Watanganyika hawataki Serekali 3 au kurudisha Tanganyika yao lengo lao nini mbeleni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikiwa Watanganyika hawataki Serekali 3 au kurudisha Tanganyika yao lengo lao nini mbeleni?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by abdulahsaf, May 7, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Wazanzibar tungekuwa mbali kama sio kujipakatisha kwa Muungano fake.


  Mimi nahisi hapa kuna mtego umetegwa na huenda kutokana na viongozi wetu wa Smz wakauingia na kutuingiza sisi kutokana na uzaifu wao wa kukumbatia Muungano usio na zamira njema kwa uchumi na maendeleo ya Zanzibar kama nchi yenye watu kidogo na ardhi ndogo.

  Uhakika wa kupiga hatua ya maendeleo ya kujikwamua Zanzibar kiushumi na kimaendeleo tusahau? Hakuna sababu kwa nini Watanganyika wakatae Tanganyika yao au Serekali 3?.

  Kama tungekuwa na mfumo wa Serekali 3 yani Serekali ya Tanganyika kwa mambo ya Tanganyika yasio ya Muungano na Serekali ya Zanzibar kushuhulikia mambo ya Zanzibar yasio ya Muungano basi ingepunguza utata na ulalamishi wa kero za Muungano?.

  Lakini inaonekana wenzetu yote hayo hawayataki lengo ni kusema ni Serekali 2 kuelekea 1? Jee ikiwa hivi sasa Wzanzibar Watanganyika wanatuhukumu kutokana na udogo wa watu wetu na nchi yetu kusema haifiki hata mkoa moja wa Tanganyika, tukiingia ktk hio Serekali 1 status ya Zanzibar itakuwa vipi?. itakuwa ni Zanzibar kumezwa na kupoteza utaifa wake ndani ya Tumbo la Muungano wa Tanganyika ijitayo Tanzania kwa kulindwa na Sera za chama.

  Tusahau Zanzibar kupiga hatuwa ya maendeleo kwa vile mambo yake yote yako undercontrol ya tanganyika na sirahisi Zanzibar kujikwamua kwa vile Serekali ya Tanganyika haipo na wenzetu ccm/smz huongozwa kwa itikadi ya sera za chama.

  Kwani kuna ubaya gani kuwa na Serekali ya Tanganyika ikasimamia mambo ya Tanganyika tu? mbona Egepty inashiriki ktk jumuia ya AU na jumuia ya nchi za Kiarabu? kwa hio na Muungano wetu tunaweza kukutana kwa mambo yale tuliokubaliana kuungana.

  Mimi nahisi lengo la Muungano wenzetu nikututawala kimpinu na Tayari viongozi wetu wameshakuwa mental slaves, kama hakuna Tanganyika lengo Wazanzibar nikuuza nchi yetu na kuwa utaifa wa Zanzibar kuwa nchi na Tanganyika kubaki na utaifa wao na power yao kwa jina la Tanzania.

  Mungu ibariki Zanzibar na Wazanzibar wote
   
 2. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Nimekusoma vyema Mkuu na nakutumia makala haya, hebu yazingatie vizuri na kutafakari:

  MUUNGANO NA MADUKA YA "WAPEMBA" NAMANGA‏

  Maneno uliyoeleza yana ukweli na kuhamasisha ila maoni yangu mimi, na pengine nayasema haya baada ya kuanza kukata tamaa, na unaweza kunisahihisha ni kuwa kwa hapa tulipofikia, huu Muungano hata hautatetereka mpaka siku ambayo wananchi wengi wa Zanzibari kwa ujumla wao watapokubali kuchukua jukumu wenyewe la kuiteteya Zanzibar kwa njia yoyote ile waiwezayo itayoweza kuwakomboa (nakusudia "any means necessary"). Vyenginevyo huu hautavunjika n'gooo. Kwasabau kuvunja muungano huu uliowakaba roho Wazanzibari kunataka viongozi madhubuti sana, waliojitolea kuwa tayari kwa lolote lile litakalotokea. Mimi sijawaona kwa hawa tulionao wanazo sifa hizo.

  Muungano huu hautatetereka hata siku moja pindipo wananchi wa Zanzibar kwa wingi wao wanashindwa kutoa msimamo wa pamoja uliodhahiri kwa dunia nzima na dunia nzima ikaona dhahiri shahiri kuwa Wazanzibari hawautaki Muungano, na wanapinga hadharani kuwa hawataki tena kulazimishwa katika muungano huu. Dunia ya leo ina Satelite na TV, Internet na You tube na njia nyingi za kuweza kuonekanwa tunapinga muungano kwa malaki ya watu.

  Sio wananchi tu, jukumu kubwa lipo kwa viongozi katika kujuwa hatima ya Zanzibar kama aidha kujitowa katika muungano au kuendelea na muungano. Kwa hali tunayoendela nayo sasa hivi ambapo Viongozi wa Zanzibar wanashindwa "kwa dhati yao" kuweka maslahi ya nchi mbele dhidi ya yale ya vyama vyao na sera za vyama vyao, basi pia sio rahisi kujitoa katika muungano. Na tuseme hawataki kujitoa katika muungano, basi hata kupatana kuyarejesha mambo kadhaa yaliyoingizwa kinyemela katika Muungano ili kuyalinda maslahi ya Zanzibar dhidi ya yale ya Tanganyika, basi hakutakuwa kwa ufanisi mkubwa ambao wananchi tungeutarajia. Nasema haya kutokana na ninavyoziona nyendo za hawa viongozi wetu ambao kauli zao hazieleweki ama wengine wamenyamaza kimya kwa kulinda maslahi yao binafsi. Na nitawabana sana viongozi katika maelezo yangu humu, kwasababu wao ndio tumewapa umbele katika kuamua hatima ya Zanzibar, mpaka pale wathibitike wameshindwa kabisa kabisa. Ila nasikitika dalili nyingi zaonyesha kuwa huko kwenye kushindwa ndiko tunakoelea. Hakuna muelekeo wa kuweza kuikomboa Zanzibar kujitoa katika muungano. Na hakuna muelekeo hata kuyarejesha mambo ya muungano kuwa yale 11 ya awali. Na hakuna hata uhakika kama Serikali ya Tanganyika itazaliwa tena. Na hata ikizaliwa tena hakuna uhakika kama Serikali ya muungano haitadhibitiwa na Watanganyika kama ilivyokuwa hapo awali. Ila natoa Indhari kuwa pindipo viongozi wakishindwa basi wananchi tusishindwe.

  Bahati hawa viongozi wetu wa leo waliopo Zanzibar wengi wao wanasiasa na wasomi. Takriban, viongozi wote wenye dhamana za juu sana katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK/GNU/SMZ) na wana sifa hizo mbili. Na hata viongozi waliochaguliwa au waliopelekwa kutoka Zanzibar katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano pia nao wana sifa hizo mbili.

  Sisi wananchi wa kawaida tngetegemea kwamba kwa sifa zao za uwanasiasa basi wangekuwa na ujasiri kulikabili suala la Muungano bila ya muhali ama kuoneana haya na viongozi wenzao wa Tanganyika, kwasababu wanachojadili ni maslahi ya nchi sio mahusiano yao binafsi au kujuwana na kuzoweana kwao. Wanachowakilisha ni taifa, roho ya taifa, hisia za ujanachi, na zaidi ni suala linalohusiana na "matakwa ya wananchi" wa Zanzibar. Kama wanasiasa ungewategemea wanazingatia hisia za wananchi kuhusu Muungano kwa hali ya unyeti wake. Ungetegemea viongozi hawatoi kauli za kukebehi madai ya wananchi. Kuhusu suala hili la Muungano, ungetegemea viongozi wa kisiasa wanaweza kutoa kauli ambazo zilizo wazi na rahisi kueleweka na zenye kuwakilisha hisia na mawazo ya wananchi ambao wanaowaongoza.

  Vyenginevyo wamewaacha wananchi wao wengi hawajui kwa uwazi kabisa misimamo ya viongozi wao kuhusu muungano na wamebakia kukisia tu. Vipi wananchi wawe wamo katika hali ya kukisia tu misimamo ya viongozi wao kuhusu jambo lenye umuhimu na nchi kama Muungano na katika wakati kama huu? Katika hali kama hiyo wananchi wanategemea nini kutoka kwa viongozi wao? Kila kiongozi aliye na nafasi juu katika SUK au mwenye nafasi ya kuwawakilisha Wazanzibari kwenye Muungano ni lazima aeleweke wazi wazi msimamo wake kuhusu Muungano, hapo ndipo itajulikana kwa uwazi na dhati ni vipi anawakilisha au ataiwakilisha Zanzibar katika masuala ya Muungano. Akifanya vyenginevyo atabanwa kwa kauli kauli na ahadi zake.

  Haya ya kujuwa kwa uwazi misimamo ya Muungano kutoka kwa viongozi Wazanzibari hatutayapata kamwe ikiwa hatutakuwa tayari kuwabana viongozi wetu kwa viwango vya juu vya uwajibikaji kuliko tufanyavyo sasa hivi. Hivi jamani hatushangai kuwa masuala ya Muungano yanajadiliwa na hatujasikia kauli yoyote kwa kiongozi yeyote wa juu kabisa nchini si Raisi wa Zanzibar wala Makamo wake wa Raisi wawili. Ingalikuwa nchi yeyote nyengine duniani wananchi wake wake wangesema huo ni ujinga (samahani lugha yangu hapa). Kwasababu duniani kote ama niseme nchi nyingi duniani katika hali kama tuliyokuwa nayo sisi huko Zanzibar hivi karibu kuhusu mjadala wa rasimu ya Muungano kitu cha kwanza wananchi wangedai wasikie kauli za viongozi wao wa juu kabisa. Kutotoa kauli yoyote na kukaa kimya katika mambo nyeti, kusingeonekana hata kidogo kama ni umahiri wa kisiasa. Kwasababu kwa vyovyote vile, kama walikubali kuwa viongozi basi moja ya jukumu walilokubali katika uongozi huo ni kukabiliana mambo magumu na nyeti ya kinchi na kuyaeleza kwa wananchi wao bila ya woga.

  Ya pili, sifa ya usomi kama nilivyoeleza awali wengi wa viongozi wa juu wa SUK na wa SMT kutoka Zanzibar wanayo. Na kwa usomi wao tungewategemea muadham viongozi wetu hawa wanatufanyia uchambuzi wa kisomi kuhusu huu Muungano, badala ya kutshindilia hoja ya Muungano huu wa kidugu tu . Kweli Hassan Nassor Moyo kasema kuwa hawa vijana wa leo ni tafauti na wale wazee wa zamani (viongozi wa zamani wa Zanzibar) kina Karume waliokuwa wakifanya mambo na viongozi wa Tanganyika kwa kujuana juana tu na kuaminiana kwa kutmia mbiu ya "udugu", lakini hawa ni tafauti. Lakini pamoja na kuwasikia Wanasheria kuweka bayana mapungufu ya Muungano katika Semina (EACROTANAL) na kwenye fursa nyengine iliyojitokeza wakati wa kujadili rasimu, hatuwaoni kujieleza kwa uwazi na kutumia hoja za kisomi kutushawishi sisi wananchi wa kawaida juu ya faida na hasa za Muungano. Lakini hili hata hao wasomi wa Tanganyika hawalifanyi, kwani wengi wao huko bado wanaendelea kuuchambua muungano huu kwa jazba zaidi kuliko usawa na haki za hoja ambazo kwa kawaida ndivyo ambavyo wasomi tungewategemea wanafanya. Na kwa bahati mbaya kwa miaka mingi viongozi wa SMZ walijengwa na tabia ya kuwa ni wategemezi wa uchambuzi wa wasomi wa Tanganyika kuhusu Muungano aidha kwa kuogopa wakihoji watachukuliwa hatua za kichama kama yaliyomfika Aboud Jumbe au wengine kwasababu ya kuukosa upeo kikweli kweli au kwasababu ya kulinda maslahi yao binafsi. Jamii hutegemea sana wasomi wao, ikiwa inaona wazi wazi umahiri, uono na misimamo thabiti ya wasomi wao katika kuilinda jamii yao. Vyenginevyo tusijekustaajabu hata kama jamii itawadharau wasomi hao pamoja kuwa wamemaliza madigirii ya juu katika vyuo vya heshima duniani.

  Katika sifa hii hii ya usomi wao hawa viongozi wetu, basi tungewategemea alau hata pale wanapotafautiana kama aidha hawautaki au wanautaka Muungano basi kwa hoja za kisomi, zitazotutoa matongotongo sisi raia zao wa kawaida. Wanaposhindwa kuwa na uchambuzi wa Muungano unaoendana na sifa zao za usomi, na zaidi kushindwa kusoma alama za nyakati, na badala yake tukija kuwaona viongozi wetu hawa wasomi wanagawika katika mapande ya wanaoutaka na wasioutaka Muungano, au wanaoutaka wa Serikali mbili (kwendea moja) na wale wanaoutaka wa Serikali tatu, na kadhalika na hatimae kuwakuta wamegawika makundi mbali mbali yenye uono tafauti na yasiyo na msimamo mmoja ni wazi uttetzi wa Zanzibar utakuwa umo mashakani. Zanzibar haitakuwa na watetezi thabiti. Taifa lolote lile ambalo wasomi na mashujaa wapiganaji madhubuti wake watakuwa wanatafautiana sana kimawazo na hawakubaliani kiasi cha kujiweka pembeni, basi taifa hilo halina budi kuwa litakuwa likiongozwa kwa kutumia fikra za waoga na wataosimama mbele kujifanya kama mashujaa wa utetezi wa fikra za viongozi hao waoga ni wapumbavu. Haya yalisemwa na Thucydides aliyeishi kati ya karne ya 460 hadi 395 kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (yaani BC) ambaye alikuwa ni Mwanahistoria wa Kigiriki.

  Nahitimisha kwa kusema hivi, ikiwa Wazanzibari hawautaki Muungano basi lazima viongozi watoe kauli ilio wazi na wananchi kwa wingi wao wawe nyuma yao kuunga mkono kauli hiyo. Na ikiwa WaZanzibari kwa wingi wao wanataka Muungano uendelee basi kwahilo pia Wazanzibari wanahitajika wawe na uwazi wa kutosha wa kutoa kauli moja ya nguvu ya kusema wanataka Muungano, na wanautaka uwe wa aina kadhaa wa kadhaa na mambo kadhaa wa kadhaa. Na dunia isikie waziwazi kilio hicho cha Wazanzibari kwa sauti kubwa zikiwemo nchi za hao umetaja JT yaani Wamarekani, lakini pia Waingereza na nchi zote za Afrika na nyengine duniani. Mimi ninaamini, si Tanganyika wala taifa kubwa lolote duniani lenye uwezo wa kuilazimisha Zanzibar kwenye Muungano ikiwa Wazanzibari kwa ujumla wao wameamua hawautaki Muungano.

  Lakini kama nilivyosema awali, wacha tuwatizame viongozi wanakotuelekeza kwa muda huu, ingawaje naweka msisitizo kuwa kwa hapa tulipofikia hatima ya Zanzibar haipo juu ya mikono ya viongozi tu wa Zanzibar, wananchi wasijipweteke, wajue ni jukumu la wananchi wote wa Wazanzibari kwa ujumla wao kuitetea Zanzibar wakiondosha tafauti zao zote za kivyama, kidini, kiasili, kikabila, kirangi, kimajimbo, kilahaja na vilugha, kiuwezo wa kipato, uwezo wa nguvu, uwezo kielimu na hata uwezo wa kujieleza . Kwa lugha ya kimisemo (slang) ya Kin'gwen'gwe cha kisiasa wanachozungumza "wenyewe" ni kuwa "the buck stops with all Zanzibari nationals together". Ikiwa Wazanzibari wataambiwa ni "nationalist" na iwe hivyo hivyo.
   
Loading...