Mrimi
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 1,691
- 633
Jamani,hivi ni mimi tu ninapata shida kujua tafsiri ya kauli hii? Ni kweli Tanzania kama zilivyo nchi nyingine duniani inaweza ikaingia katika machafuko..hilo halina ubishi,ingawa hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu anaombea hiyo itokee..Na ktk hili ni wajibu wetu sote kukemea kwa nguvu zetu zote vitendo vyote vinavyoashiria kupota kwa amani yetu.
Historia ya kuchafuka kwa Lybia wengi wetu tunajua ni kwa sababu ya nguvu ya magharibi ilivipa nguvu vikundi vya upinzani ili vimwondoe Ghadaffi madarakani..na kuanzia hapo amani imepotea hadi leo..
Hivi ni kwa nini siku hizi tunaambiwa kwamba ikiwa upinzani utashinda,nchi itageuka kuwa kama Lybia..Hii maana yake nini? Upinzani wa Lybia ulimwangusha Ghadaffi kwa kumwaga damu,upinzani wa Tanzania unaomba kuongoza nchi kwa ridhaa ya watanzania wenyewe..Hizi kauli zina maana gani?
Je,ndio kusema kuna watu wamejiandaa kutokubali wapinzani kuongoza nchi? Ndiyo kusema hata kama watanzania kwa ujumla wao wakiamua kuchagua upinzani,kuna watu hawako tayari kuona nchi inaongozwa na upinzani?
Hii tafsiri yake nini? Kwamba pengine labda kuna watu wamejiandaa kuleta machafuko ikiwa upinzani utashinda uchaguzi..na kama ndio hivyo,ina maana gani sasa kushiriki uchaguzi ikiwa vyovyote iwavyo upinzani hauwezi kuongoza nchi?
Wanaoleta machafuko Lybia ni pamoja na wafuasi wa Ghadaffi wanaoendelea kupigania kurudisha utawala wao..sasa,je huku kwetu kuna wanaojiandaa kupigania kurudisha utawala wao ikiwa kwa vyovyote vile upinzani utachukua nafasi zao? Au hii maana yake nini?
Sielewi..