Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,920
- 31,153
Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu mwaka huu 2020 mwezi October.
Chama tawala CCM chini ya Rais Magufuli inamaliza muda wake wa miaka mitano.Serekali ya awamu ya tano imefanya mambo mengi mazuri katika kipindi chake cha miaka mitano,lakini pia yapo mambo mengi imekosea mojawapo kubwa ni uhuru wa vyombo vya habari,uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zao za siasa katika mazingira ya haki,usawa na misingi ya utu yamekumbana na dhoruba kali ya viwango vya kutisha.
Majuzi tumesikia taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu CHADEMA akidai kwamba Tume ya uchaguzi haitolazimika kutoa fomu kwa mawakala wa vyama.Nimekuwa nikijiuliza ikiwa unaamini umewatendea wananchi wako vizuri ni kwanini unaandaa mazingira mabovu na yaliyojaa mashaka makubwa katika uchaguzi !.
Kwanini taifa letu sote tuna andaa uchaguzi ambao unawanyima wananchi haki ya kuwachagua viongozi wao wanaowataka badala yake unatengeneza mazingira ya kupachika viongozi ambao wananchi hawakuwachagua ?.
Nimeendelea kujiuliza tena na tena ni kwanini resources za nchi zinatumika kugandamiza viongozi wa vyama vya upinzani wakati wapo kwa mujibu wa katiba yetu.Utashangaa viongozi wanabambikiwa kesi,wanatiwa ndani hovyo hovyo,wananunuliwa kama viazi huku wakitoa sababu za kijinga.
Wakati umefika sasa tukaacha mambo ya hovyo,taifa hili letu sote walio na madaraka na wasio madaraka,wananchi wa kawaida kwa maana ya wakulima na wafanyakazi wote tunahitaji heshima na haki.