Ikiwa Uhuru na Haki za Binadamu tayari vinazingatiwa kwa kiasi fulani, mengine tutarekebisha taratibu

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,179
73,623
Najua kuna mapungufu makubwa katika utawala wa awamu ya sita, wa Rais Samia. Lakini lazima tuwe na pa kuanzia.

1. Angalau kuna uhuru, watu wanaweza wakalala majumbani mwao wakiwa na uhakika kutakucha salama?

2. Kwa kiasi fulani haki za Binadamu zinazingatiwa ingawa bado kuna kazi kubwa ya kufanya, not to 100%

3. Utawala wa sheria unakuja taratibu, Mahakama zinaanza kutoa haki kadri ya sheria zetu, ingawa bado Ibrahim Juma ana kazi kubwa ya kufanya.

BADO: Bunge bado ni kituko!
 
Mkuu bado naona juhudi kubwa za kuminya HAKI ya Watanzania wengi. Kwa mfano mama alipofuta kesi 147 kwa kuwa zilikuwa ni za kubambikiwa alitakiwa pia afute hukumu zote za kesi za huyo Msowoya na hivyo kuwaachia huru wafungwa wote na kuwarudishia mabilioni yao waliyolipa kama faini.

Swala la COVID-19 mjengoni mama bado anademka wale hawastahili kuendelea kuwepo Bungeni huku wakipokea mabilioni kinyume na katiba ya nchi. Pia kauli yake kwamba tutasubiri sana kupata katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.

Sijui “kusubiri sana” kunamaanisha nini. Tutasubiri kwa miezi sita, mwaka, miaka miwili etc. Vipi kuhusu kukutana na Viongozi wa Chadema? Mbona miezi mitatu inakatika bado yuko kimya?
 
Najua kuna mapungufu makubwa
  • Kuna mapungufu.
  • Kuna mapungufu makubwa.
  • Kuna mapungufu makubwa sana.
  • Kuna mapungufu makubwa mno.

Hizo kauli zina vipimo na vigezo ili mtu aweze kujua ukubwa wa mapungufu, sasa wewe umetumia vigezo au vipimo gani ili kujua hayo mapungufu MAKUBWA ya serikali ya Samia Suluhu Hassan (SASHA)?
 
Mama alikula kiapo cha kuilinda na kuitetea katiba ya Nchi huku akiwa ameshika kitabu kitakatifu cha dini yake. Hakuwekewa mipaka ya nini anachoweza kukifanya au kutokufanya kama Katiba ya Nchi INAKIUKWA. Kama ipo mipaka hiyo ndani ya katiba basi iwekwe hapa
Hapo mnataka Mama aingilie Muhimili wa Bunge ili mpate kauli kwamba yeye naye anaingilia mihimili ya dola?
 
Mama alikula kiapo cha kuilinda na kuitetea katiba ya Nchi huku akiwa ameshika kitabu kitakatifu cha dini yake. Hakuwekewa mipaka ya nini anachoweza kukifanya au kutokufanya kama Katiba ya Nchi INAKIUKWA. Kama ipo mipaka hiyo ndani ya katiba basi iwekwe hapa...
Yeye ndiye kala kiapo cha yeye mwenyewe kulinda katiba na wala hajala kiapo kwa niaba ya Watu wengine, kuhusu kuvunjwa kwa katiba kwa minajili ya Wale Covid 19 kule Bungeni hilo lipo kwa SPIKA wa Bunge na sio kwa Mama.
 
Najua kuna mapungufu makubwa katika utawala wa awamu ya sita, wa mama Samia. Lakini lazima tuwe na pa kuanzia.
1. Angalau kuna uhuru, watu wanaweza wakalala majumbani mwao wakiwa na uhakika kutakucha salama?...
Naunga mkono hoja , kwa vile huu ni mwanzo tu, tumpe muda Mama Samia, atatenda.
P
 
Yeye ni Rais wa Nchi na katiba inampa madaraka makubwa ya kuilinda na kuitetea katiba hiyo. Kama kuna mipaka ndani ya katiba ambayo inamzuia kuilinda katiba inapokuwa inavunjwa Bungeni basi vipengele hivyo viwekwe hapa.

Sasa Bunge linapovunja katiba wazi wazi nani mwenye uwezo wa kuilinda na kuitetea katiba INAYOKIUKWA na Bunge? Bunge liachwe tu liendelee kuvunja katiba!?
Yeye ndiye kala kiapo cha yeye mwenyewe kulinda katiba na wala hajala kiapo kwa niaba ya Watu wengine, kuhusu kuvunjwa kwa katiba kwa minajili ya Wale Covid 19 kule Bungeni hilo lipo kwa SPIKA wa Bunge na sio kwa Mama.
 
Naunga mkono hoja , kwa vile huu ni mwanzo tuu, tumpe muda Mama Samia, atatenda.
P
Kumbuka pia ni Nature ya mwanadamu, hatoridhika mpaka aingie kaburini, je Mama afanye lipi kumridhisha kila mtu kwa kila kitu? America yenyewe haijawaridhisha Waamerica Wote sembuse Tz ya Mama?😁
 
Mkuu bado naona juhudi kubwa za kuminya HAKI ya Watanzania wengi. Vipi kuhusu kukutana na Viongozi wa Chadema? Mbona miezi mitatu inakatika bado yuko kimya!?

Najiuliza kwa Sauti, tangu CHADEMA kimeanzishwa ni lipi la kitaifa (baya/zuri) viongozi wake wamefanya kuwekwa kwenye kumbukumbu (legacy)?
 
Najua kuna mapungufu makubwa katika utawala wa awamu ya sita, wa mama Samia. Lakini lazima tuwe na pa kuanzia.
1. Angalau kuna uhuru, watu wanaweza wakalala majumbani mwao wakiwa na uhakika kutakucha salama?...
Yes and no.

Unaposema, Angalau na uhakika kutakucha salama ungesema angalau wamekula.

Unaposema, Kwa kiasi fulani haki za msingi..Blablabla. Ni bora ungezitaja. Mfugaji wa mwatuna mkwezi wa kengeja na mvuvi wa kilwa kivinje haki zao si sawa na kumtukana rais halafu ukimbilie belgium.

Unaposema ...Utawala wa sheria unakuja taratibu halafu unataja professor juma nashindwa kukuelewa. Professors do not grow on trees my fpfriend. Uchaguzi umepita majuzijuzi tu mkaanguka chini puu! Rais aliomba apelekewe gwajima walete maendeleo wapig kura wakampelekea gwajima, sasa tunasubiri maendeleo. Na kwa sugu hivo hivo, na hai, na kengeja, na tarime.

Watu wamewachoka ndiyo maana hakuna hatammoja alitelalamika kwa professor juma. Narudua, hata mmoja. You knew the law wouldn't help you break the law.

Unaposema bunge ni kituko mwulize tundulissu. Alikuta wabunge 113 na vitimaalum 60 waliletwa na Lowassa wa CCM. Katukana matusi weeeee kaambulia Mbunge mmoja, tena Mfipa siyo Mchagga. What happened exactly? Bado kuna nafasi 19, waliowahi wakawahi, wengi wao Wazaramo na Wasukuma na Washashi na Waha, siyo kama zamani. Hili nalo mnanuna mnataka bora tukose wote.

Mkitaka kutawala wacheni ubinafsi na ukabila. Unamsikia Mbowe anasema Geita ni mkoa mdogo kasahau kwao, analalamika Airport yeye kwao ziko 3. Anadai Chato wanajenga hospitali ya Rufaa kasahau kwao ziko 5. Watu si wajinga, wanawaona hamueleweki.

You are retired? Lea wajukuu zako, Tanzania hatuna pensheni ya wakulima, hiyo nayo ni haki YAO ya msingi huku wewe unaenda WB kutaka mabinti zao wasome darasani wakinyonyesha! Soma alama za nyakati dadangu.

ZFZMWCCM, la sivo nchi yetu itayumba.
 
Mkuu bado naona juhudi kubwa za kuminya HAKI ya Watanzania wengi. Kwa mfano mama alipofuta kesi 147 kwa kuwa zilikuwa ni za kubambikiwa alitakiwa pia afute hukumu zote za kesi za huyo Msowoya na hivyo kuwaachia huru wafungwa wote na kuwarudishia mabilioni yao waliyolipa kama faini...
Hivi unajua kuwa mawazo yako huwa ya kijuha!
 
Yes and no.

Unaposema ....Angalau na uhakika kutakucha salama ungesema angalau wamekula...
Inawezekana una hoja, ingawa mimi naona unachanganya mambo. Nakushauri anzisha uzi (thread) utoe hoja yako. It does not fit here , it is an outlier.
 
Yeye ni Rais wa Nchi na katiba inampa madaraka makubwa ya kuilinda na kuitetea katiba hiyo. Kama kuna mipaka ndani ya katiba ambayo inamzuia kuilinda katiba inapokuwa inavunjwa Bungeni basi vipengele hivyo viwekwe hapa...
Uko sahihi, kama kuna chochote kinavunja katiba, ni wajibu wa Rais kukikemea. Nadhani ndiyo maana Rais anaweza kulivunja Bunge akiona linavunja Katiba! Uko sahihi, ni wajibu wake kutetea Katiba
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Shukrani Mkuu 🙏🏾🙏🏾🙏🏾
Uko sahihi, kama kuna chochote kinavunja katiba, ni wajibu wa Rais kukikemea. Nadhani ndiyo maana Rais anaweza kulivunja Bunge akiona linavunja Katiba! Uko sahihi, ni wajibu wake kutetea Katiba
 
-Kuna mapungufu.
-Kuna mapungufu makubwa.
-Kuna mapungufu makubwa sana.
-Kuna mapungufu makubwa mno.

Hizo kauli zina vipimo na vigezo ili mtu aweze kujua ukubwa wa mapungufu, sasa wewe umetumia vigezo au vipimo gani ili kujua hayo mapungufu MAKUBWA ya serikali ya Samia Suluhu Hassan (SASHA)??
casual observation tells it all!
 
Najiuliza kwa Sauti, tangu CHADEMA kimeanzishwa ni lipi la kitaifa (baya/zuri) viongozi wake wamefanya kuwekwa kwenye kumbukumbu (legacy)?
Nafikiri uko nje ya mada. au kwa maksudi unajarib kupindisha uelekeo wa mada na kuhamisha watu.
Hii mada haina uhusiano na legacy au chadema.
uko out of topic
 
Yes and no.

Mkitaka kutawala wacheni ubinafsi na ukabila. Unamsikia Mbowe anasema Geita ni mkoa mdogo kasahau kwao, analalamika Airport yeye kwao ziko 3. Anadai Chato wanajenga hospitali ya Rufaa kasahau kwao ziko 5. Watu si wajinga, wanawaona hamueleweki...
Mkuu umemjibu Retired kwa ufasaha kabisa.

Nami mara nyingi najiuliza mawazo/hoja zake, na kundi lake, huwakilisha jamii ipi ya Watanzania!!!

Wakati wa Awamu ya Nne, Rais walimbeza na kumtukana ati kuwa ni dhaifu. Rais wa Awamu ya Tano ati dikteta. Sasa wameanza kwa Rais aliyeko madarakani.

Ushauri wangu kwake Retired na kundi lake, ambalo linajipambanua ni wafuasi wa CHADEMA, ili hili Jukwaa walitumie kwa faida ya chama. Wakati viongozi wao wanaendesha kampeni ya chama kujiendesha kidigitali na kuacha siasa za Uharakati, warejee kuelimisha "Sera mbadala ya Maendeleo ya Taifa" iliyozinduliwa kwa bwembwe mwaka 2018. Hata viongozi wao kwenye kampeni hiyo suala la Sera halizungumziwi kabisa.

NI MAWAZO YANGU TU KWENYE "KEYBOARD"
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom