Ikiwa tozo na VAT zina kiwango sawa, tafsiri nyepesi ni kwamba VAT imeongezeka mara 2

Jerlamarel

JF-Expert Member
Sep 14, 2021
843
2,517
IMG_20220902_092625.jpg

Picha hapo juu inajieleza. Tafsiri nyepesi ya hizi tozo ni kwamba VAT imepanda mara 2. Zile stori za sijui nchi ni yetu sote, tunajenga nchi, tunaendesha miradi ni vichaka tuu vya kujifichia ila ukweli ndiyo huo kwamba VAT ime-double.

Sasa kwa hali ya uchumi ilivyo ni mzigo tosha kwa mwananchi, na mfumuko wa bei ulivyo kwa sasa, then wewe kama kiongozi bado tena unakuja kuwaongezea mzigo wa VAT mara 2 hakuna jina jingine la kukupa zaidi ya "MUUAJI".

Viongozi acheni stori nyepesi nyepesi, wananchi hatutaki tozo.
 
Ni wakati wa sisi sasa kubadilisha mfumo wa serikali hii mbovu.

2025 tusisahau magumu tunayopitia na kufanya chaguo sahihi.

Wapinzani ni wakati wao wa kujenga ngome imara sasa,mwanga unaonekana kwa upande wao.

Wasibugi kupokea mamluki wa chama tawala.
 
Ni wakati wa sisi sasa kubadilisha mfumo wa serikali hii mbovu....
Kama unategemea mabadiliko kwenye tume ya jecha utarudi 2026 na comment chungu zaidi ya hii 😂😂😂😂😂😂!!! Huwezi kutegemea matokeo tofauti kwa kutumia njia ile ile.
 
Makato ya Serikali, hata yapewe majina gani, ukweli ni kwamba hiyo ni kodi. Na kimsingi kwa mlipaji, malipo hayo hata yapewe mapambo gani, maana yake anatakiwa kutoa zaidi.

Hizi tozo, kama ilivyoneshwa kwenye jedwali, wangeweza tu kusema kuwa Serikali imeongeza VAT kwenye miamala ya fedha toka 18% mpaka 35%.

Kwanza ukijiuliza, unapoweka VAT kwenye miamala, hata ile mantiki ya VAT inatoweka. VAT ni kodi kutokana na ongezeko la thamani ya bidhaa. Sasa unapomtumia gela mama yako kwa mpesa, au benki au tigopesa, n.k., ni thamani gani iliyoongezeka kwenye hiyo pesa kutokana na kuituma?

VAT ilipowekwa wakati wa utawala wa Hayati Mkapa, ni bidhaa fulani tu ndiyo zilikuwa na VAT, leo ni kila kitu, halafu na tozo tena inawekwa juu yake!!

Watawala wanatakiwa kufahamu kuwa, kama Serikali inavyohitaji sana hela kwaajili ya kutekeleza majukumu yake, hata hawa wananchi wanaokamliwa sana kodi, nao wanatamani sana kuwa na hela ya kutekeleza majukumu ya msingi ya kwao wenyewe, familia zao na hata jamaa zao. Ni lazima ipatikane balance, ambapo Serikali inapata kinachowezekana na kilicho halali, bila ya kumwumiza na kumdunisha mlipa kodi.
 
View attachment 2342857

Picha hapo juu inajieleza. Tafsiri nyepesi ya hizi tozo ni kwamba VAT imepanda mara 2. Zile stori za sijui nchi ni yetu sote, tunajenga nchi...
Sasa kwa hali ya uchumi ilivyo ni mzigo tosha kwa mwananchi, na mfumuko wa bei ulivyo kwa sasa, then wewe kama kiongozi bado tena unakuja kuwaongezea mzigo wa VAT mara 2 hakuna jina jingine la kukupa zaidi ya "MUUAJI
 
Tatizo ni kuwa hata VAT yenyewe ukimuuliza afisa haijui na hawezi kuielezea na hata kutoa elimu kuhusu ulipaji na utozaji wa kodi

Natamani Waziri ateue na kuelezea namna kodi inavyotozwa

Kwa mfano
Nimemuuliza mwenye duka unatoza VAT 18% vipi
Hajui kabisa na analalamika serikali inaonea watu

Halafu wakija kuchukua chao unalalamika na mtaji unaisha baada ya miaka mitatu tu

Elimu inahitajika sio kukadiria tu na kuwaumiza wafanya biashara
Sijui lawama hizi kama mwigulu anazijua
 
Ni wakati wa sisi sasa kubadilisha mfumo wa serikali hii mbovu..
2025 tusisahau magumu tunayopitia na kufanya chaguo sahihi.

Wapinzani ni wakati wao wa kujenga ngome imara sasa,mwanga unaonekana kwa upande wao. .
Wasibugi kupokea mamluki wa chama tawala.
tatizo tunaweza kukumbuka kila gumu tulilopitia na maamuzi sahihi yakafanyika lakini tusipewe tulichokichagua.

Tatizo lingine mpaka dakika hii hakuna mbadala ya waliopo sasa. Hata hao wanaojiita wapinzani fikra zao hazina tofauti na walio madarakani sasa. Mfano hai umeona, baada ya kupewa kila hitaji lao binafsi kila mmoja kwa nafasi yake wameufyata kimya.

Mkombozi hasa ni katiba mpya, hayo mengine yote ni maigizo tu.
 
Yani balance of payment ipo negative?. Ndio maana wananchi wanakamuliwa Bila huruma.
 
Makato ya Serikali, hata yapewe majina gani, ukweli ni kwamba hiyo ni kodi. Na kimsingi kwa mlipaji, malipo hayo hata yapewe mapambo gani, maana yake anatakiwa kutoa zaidi.

Hizi tozo, kama ilivyoneshwa kwenye jedwali, wangeweza tu kusema kuwa Serikali imeongeza VAT kwenye miamala ya fedha toka 18% mpaka 35%.

Kwanza ukijiuliza, unapoweka VAT kwenye miamala, hata ile mantiki ya VAT inatoweka. VAT ni kodi kutokana na ongezeko la thamani ya bidhaa. Sasa unapomtumia gela mama yako kwa mpesa, au benki au tigopesa, n.k., ni thamani gani iliyoongezeka kwenye hiyo pesa kutokana na kuituma?

VAT ilipowekwa wakati wa utawala wa Hayati Mkapa, ni bidhaa fulani tu ndiyo zilikuwa na VAT, leo ni kila kitu, halafu na tozo tena inawekwa juu yake!!

Watawala wanatakiwa kufahamu kuwa, kama Serikali inavyohitaji sana hela kwaajili ya kutekeleza majukumu yake, hata hawa wananchi wanaokamliwa sana kodi, nao wanatamani sana kuwa na hela ya kutekeleza majukumu ya msingi ya kwao wenyewe, familia zao na hata jamaa zao. Ni lazima ipatikane balance, ambapo Serikali inapata kinachowezekana na kilicho halali, bila ya kumwumiza na kumdunisha mlipa kodi.
Kwanza ukijiuliza, unapoweka VAT kwenye miamala, hata ile mantiki ya VAT inatoweka. VAT ni kodi kutokana na ongezeko la thamani ya bidhaa. ONGEZA NA HUDUMA SIYO BIDHAA TU
 
Back
Top Bottom