Ikiwa sharti kuu la kula kiapo ni kuilinda na kuihifadhi Katiba ya nchi, ni kwanini viongozi hao baada ya kula viapo hivyo, wanaisigina Katiba hiyo?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,418
2,000
Tumekuwa tukishuhudia kila kiongozi kabla ya kukabidhiwa madaraka, ni lazima kwanza aape na katika kiapo hicho, sharti kuu ni kuilinda na kuiheshimu Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama ya nchi yetu

Sasa ni kwanini baadhi ya viongozi Mara tu wanapoanza kutumikia nyadhifa hizo wanaipuuza Katiba ya nchi na kuiona kama takataka?

Ifahamike kuwa Katiba ya nchi ni lazima uitekeleze na kuipuuza Katiba hiyo ni sawasawa na uhaini na huyo kiongozi anastahili kushitakiwa.

Sasa ninachojiliuliza ni kwa nini baadhi ya viongozi wakubwa ambao nao wameapa kuitii na kuiheshimu Katiba hiyo wakiipuuza na kuiona kama takataka na kuisigina Katiba hiyo?

Mfano dhahiri ni kwa Spika wa Bunge letu la Jamhuri, Spika Ndugai, ambaye anajua kuwa huwezi kuwa mbunge kama umevuliwa uanachama wako na chama kilichokudhamini ubunge wako.

Spika Ndugai amesema hadharani kuwa atawalinda kwa nguvu zote wabunge wa viti maalum wa Chadema, ambao chama chao cha Chadema kimeutangazia Umma kuwa kimewavua uanachama wao.

Sasa kama Spika anaonyesha mfano mbaya kiasi hicho, wa kuamua kuisigina Katiba ya nchi kadri atakavyo, hivi huyu Spika ana nia ya kulitumbukiza Taifa hili shimoni na tusiweze tena kujikwamua?
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,587
2,000
Wanasiasa bana.
EolbH7_WMAYAwWW.jpg
 

Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
2,411
2,000
Tumekuwa tukishuhudia kila kiongozi kabla ya kukabidhiwa madaraka, ni lazima kwanza aape na katika kiapo hicho, sharti kuu ni kuilinda na kuiheshimu Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama ya nchi yetu...
Kumbuka katiba Ina mpa ulinzi pindi akifanya makosa latina utekelezaji wa majukumu na baada.
 

Usher-smith MD

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
8,511
2,000
Mfumo dhaifu ndio shida ya nchi yetu
Wangekuwa wanashitakiwa na kuhukumiwa kwa haki, wasingethubu kutufanya mazombi
 

Blackjew

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
639
1,000
Katika upumbavu na ushetani unaofanywa na kina ndugai jiwe na maraisi waliopita mbele ya jamaii na unaogharimu mamilioni ya fedha za walipa Kodi kwa kukufuru ni KUAPA kuilinda katiba. Kama katiba ingekuwa mtu aliye hai katiba yetu ingekuwa ilikufa iko makaburini au imeoza nzi wanaila tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom