Ikiwa Serikali na madaraka yake yote na mamlaka yake yote yanatoka kwa Wananchi, kuna kosa gani wananchi kumuuliza kiongozi wa serikali?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,681
1,109
Wakati mwingine ukitafakari Sana unaweza kujisemea kwa kunong'ona kuwa hii nchi ina vichaa wengi Sana!

Rais wetu mpendwa alikwisha sema vita ya kichumi haiwezi kutuacha salama, kwa kuwa tupo kwenye nia thabiti ya kuijenga nchi katika kupambana kuidhibiti vita hii, lazima wapambanaji mmoja wao akipotea atafutwe au maelezo ya kina juu ya kupotea kwake yawe wazi.

Ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema (1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na Hali ya kijamii kwa hiyo.

(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii;

(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;

(c) serikali itawajibika kwa wananchi;

(d) wananchi watashiriki katika shughuli za serikali yao kwa mujibu wa masharti ya katiba hii.

Ikiwa serikali na madaraka yake yote na mamlaka yake yote yanatoka kwa wananchi, kuna kosa gani wananchi kumuuliza kiongozi wa serikali aliyechaguliwa na wenye mamlaka ya kuiweka madarakani ikiwa haonekani na hakuna taarifa zozote juu yake!

Hii kamata kamata ya tamko la mawaziri inazingatia katiba ya Jamhuri ya Muungano waliyoapa kuilinda na kuihifadhi au wanakurupuka bila kuzingatia ufafanuzi na takwa la kikatiba bila kuleta mitafaruku isiyo na msingi!!!

Je, wananzingatia ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inayotamka bayana kuwa ;

Kila mtu-
(a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake;

(b) anayo Haki ya kutafuta ,kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi;

(c) anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake;na

(d) anayo Haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii.

Naamini kwa vacuum ninayoiona, nchi inaendeshwa kwa mihemuko bila kuzingatia sheria na katiba.

Hoja yangu nini!!

Kumbe kwa mujibu wa katiba wananchi wana haki ya kujua hali ya kiongozi wao akiwa mgonjwa, mfu au mzima kwa kuwa ndiyo wenye mamlaka inayojenga misingi ya kuipa serikali mamlaka na madaraka ya kuongoza. Hivyo basi-

Rais ni mtumishi wa wananchi, kujua Hali yake na uwepo wake kosa liko wapi!! Hatuoni kama tuna tengeneza ukakasi usio na ulazima wowote zaidi ya kuimarisha chuki ya wananchi dhidi ya serikali yao!!!

Ustawi wa wananchi uko wapi au kuwakamata watu wanaotaka kujua kiongozi wao ndio ustawi wa wananchi!!!

Kuna mahali tumekwama kwa kushindwa kuruhusu akili zetu kutawaliwa na mihemuko. Maana ya kuapishwa kwa katiba na vitabu vitakatifu ni kukuhofisha na hofu ya Mungu lakini kukumbusha kuwa utakayo yatekeleza hayatakuwa kinyume na matakwa ya sheria.

Kwa kukosa weledi serikali imekuwa inatengeneza hasara kubwa kuwalipa wahanga wa matukio ya nguvu za dola bila kuzingatia maarifa kwenye majukumu yao kwa ufaili kesi za udhalilishaji.

Niase serikali,kuhoji afya ya kiongozi si dhambi, dhambi ni kutumia maguvu bila weledi. Serikali itoe tamko kuwatoa wasiwasi wananchi vinginevyo mnaingiza nchi kwenye taharuki kubwa.
 
Mabeberu wa Nchi jirani ya Kenya labda!

Ila kuhusu Mabeberu wa Ulaya na Marekani, nadhani tutakuwa tunawaonea tu!
Kenya ni wadogo zetu,na ndg zetu.hivi hujui kwenye vita ya uchumi,mlengwa akawa mwingine lakini kwa kuwa ,uchumi haunaga mipaka impact yake husambaa hata ambako hapakulengwa!? Hivyo automatically inakuwa under mutuy inclusive,na usipo jidhatiti unaumia pakubwa.unajua Ila unajifanya hujui !
 
kuna wakati inabidi mtu ajifanye mpumbavu ili ku suit eggo zake.

ni kuwavumilia tu.
 
Yaani hizi drama, mwanzoni alianza kutokea ghafla bandarini, airport, TRA, wizara ya fedha zikapazwa sauti kuwa wapo wasaidizi kwa nini yeye n.k. , sasa kawaacha wasaidizi waliosemwa wafanye kazi sauti tena juu zaidi hatumuoni loh!!
 
Sijui kama uzalendo utaamka, ngoja tujaribu.

View attachment 1727863
Kipimo moja wapo kati ya kiongozi na mtawala ni hiki. Kiongozi anachaguliwa na watu na anasimamia kuongoza yale walio mchagua wameyaweka . Mtawala anaweza kurithi ama kutumia njia zisizo haki kupata madaraka, yeye hasimamii maamuzi ya liyowekwa na wenye nchi Bali kauli yake ndiyo sheria. Kwa ufupi, KIONGOZI ANAPENDWA NA MTAWALA HAPENDWI ILA ANAOGOPWA
 
Yaani hizi drama, mwanzoni alianza kutokea ghafla bandarini, airport, TRA, wizara ya fedha zikapazwa sauti kuwa wapo wasaidizi kwa nini yeye n.k. , sasa kawaacha wasaidizi waliosemwa wafanye kazi sauti tena juu zaidi hatumuoni loh!!

Jibu ni fupi sana

Mimi nipo huku nafanya A, B, C

Dungu zangu watanzania msiwe nahofu. Nawajali na wapenda sana.

Mungu ibariki Tanzania

Akisha kufanya hivo teyari kutatua mehemko, mitafaruku na kelele zote kwisha.
 
Kuna shida gani asijitokeze,mitume waliumwa na waumini walielezwa sembuse siye
Jibu ni fupi sana

Mimi nipo huku nafanya A, B, C

Dungu zangu watanzania msiwe nahofu. Nawajali na wapenda sana.

Mungu ibariki Tanzania

Akisha kufanya hivo teyari kutatua mehemko, mitafaruku na kelele zote kwisha.
 
Wakati mwingine ukitafakari Sana unaweza kujisemea kwa kunong'ona kuwa hii nchi ina vichaa wengi Sana!

Rais wetu mpendwa alikwisha sema vita ya kichumi haiwezi kutuacha salama, kwa kuwa tupo kwenye nia thabiti ya kuijenga nchi katika kupambana kuidhibiti vita hii, lazima wapambanaji mmoja wao akipotea atafutwe au maelezo ya kina juu ya kupotea kwake yawe wazi.

Ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema (1) Jamhuri y
Wakati mwingine ukitafakari Sana unaweza kujisemea kwa kunong'ona kuwa hii nchi ina vichaa wengi Sana!

Rais wetu mpendwa alikwisha sema vita ya kichumi haiwezi kutuacha salama, kwa kuwa tupo kwenye nia thabiti ya kuijenga nchi katika kupambana kuidhibiti vita hii, lazima wapambanaji mmoja wao akipotea atafutwe au maelezo ya kina juu ya kupotea kwake yawe wazi.

Ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema (1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na Hali ya kijamii kwa hiyo.

(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii;

(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;

(c) serikali itawajibika kwa wananchi;

(d) wananchi watashiriki katika shughuli za serikali yao kwa mujibu wa masharti ya katiba hii.

Ikiwa serikali na madaraka yake yote na mamlaka yake yote yanatoka kwa wananchi, kuna kosa gani wananchi kumuuliza kiongozi wa serikali aliyechaguliwa na wenye mamlaka ya kuiweka madarakani ikiwa haonekani na hakuna taarifa zozote juu yake!

Hii kamata kamata ya tamko la mawaziri inazingatia katiba ya Jamhuri ya Muungano waliyoapa kuilinda na kuihifadhi au wanakurupuka bila kuzingatia ufafanuzi na takwa la kikatiba bila kuleta mitafaruku isiyo na msingi!!!

Je, wananzingatia ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inayotamka bayana kuwa ;

Kila mtu-
(a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake;

(b) anayo Haki ya kutafuta ,kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi;

(c) anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake;na

(d) anayo Haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii.

Naamini kwa vacuum ninayoiona, nchi inaendeshwa kwa mihemuko bila kuzingatia sheria na katiba.

Hoja yangu nini!!

Kumbe kwa mujibu wa katiba wananchi wana haki ya kujua hali ya kiongozi wao akiwa mgonjwa, mfu au mzima kwa kuwa ndiyo wenye mamlaka inayojenga misingi ya kuipa serikali mamlaka na madaraka ya kuongoza. Hivyo basi-

Rais ni mtumishi wa wananchi, kujua Hali yake na uwepo wake kosa liko wapi!! Hatuoni kama tuna tengeneza ukakasi usio na ulazima wowote zaidi ya kuimarisha chuki ya wananchi dhidi ya serikali yao!!!

Ustawi wa wananchi uko wapi au kuwakamata watu wanaotaka kujua kiongozi wao ndio ustawi wa wananchi!!!

Kuna mahali tumekwama kwa kushindwa kuruhusu akili zetu kutawaliwa na mihemuko. Maana ya kuapishwa kwa katiba na vitabu vitakatifu ni kukuhofisha na hofu ya Mungu lakini kukumbusha kuwa utakayo yatekeleza hayatakuwa kinyume na matakwa ya sheria.

Kwa kukosa weledi serikali imekuwa inatengeneza hasara kubwa kuwalipa wahanga wa matukio ya nguvu za dola bila kuzingatia maarifa kwenye majukumu yao kwa ufaili kesi za udhalilishaji.

Niase serikali,kuhoji afya ya kiongozi si dhambi, dhambi ni kutumia maguvu bila weledi. Serikali itoe tamko kuwatoa wasiwasi wananchi vinginevyo mnaingiza nchi kwenye taharuki kubwa.
a Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na Hali ya kijamii kwa hiyo.

Duu kumbe kuongoza nchi siyo km kuongoza familia ama kampuni binafsi
 
Daah mnaandika maandishi marefu sijui hata kama wanawaelewa au kusoma hao wananchi viongozi..
 
Watanzania wavivu wa kusoma lakini ingekuwa story ya mapenzi hapa mashallah
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom