Ikiwa nadaiwa mkopo na nikakiri nimeshindwa kulipa ni hatua gani naweza kuchukuliwa?

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,041
10,463
Mtu ambaye amepitia struggle ya kudaiwa kiwango cha pesa ambacho kipo nje ya uwezo wake atakuwa ashaelewa nini namaanisha.

Mfano unafanya kazi unalipwa 500,000/= per month una madeni sehemu tofauti lakini Total ya madeni yako ni 10,000,000/= ikumbukwe kwamba kwenye hayo madeni kuna madeni umiza(yaani kadri unavyochelewa kulipa ndivyo kiasi unachodai kinaongezeka).

A part from that wewe ni Baba, Mume, Kaka na mtoto unategemewa na kuhakikisha kuwa panapotokea tatizo basi liwe under control kwa kutumia akili na uwezo wako.

Bila ya kusahau kuwa gharama za maisha zipo palepale
  • Kodi ya nyumba
  • Chakula
  • Bili za umeme na ving'amuzi
  • Mavazi
  • Ada. etc
Ikumbukwe sina assets zozote zinazoweza kucompensate mikopo yangu dhamana niliyonayo ni kazi pekee.

Kwa situation kama hii unahitajika muujiza tu kulipa hiyo pesa sasa nikikubali na kukiri siwezi kulipa madeni yangu je kisheria ntachukuliwa hatua gani?

Mara mwisho nilisikia Zambia ilikiri kushindwa kulipa madeni yake lakini heri Zambia sababu ni nchi wanaweza binafsisha serikali.
 
Ni vigezo gani walitumia kukupa mkopo?

Maana hata Mimi nataka mkopo lakini Sina vigezo kwahiyo siwezi kupata mkopo.

Je, wakati unapewa mkopo ulikua na mdhamini?

Je, huo mkopo haukuwa na Bima na je kazi ya bimai hua Ni nini kwenye mkopo?

Ukipata hayo majibu nadhani utajua nini Cha kufanya.
 
Basi wachukue hiyo kadi na ili kila hela ikingia kwenye Akaunti yako wachukue kiasi hadi hapo deni lao litakapoisha.

Tahadhari usiwape namba yako ya siri na ingependeza kama mtakubaliana kuwa utakuwa unalipa kiasi gani kwa mwezi.
 
Huo mkopo uliouchukua uliufanyia kazi gani mpaka unakosa hela ya kuulipa kwa installment?
Sio kwamba hiyo hela nilichukua kwa wakati mmoja na kutoka kwa mtu mmoja ni kuwa watu na taasisi tofauti zinanidai ambapo nikipiga Total ni 10,000,000 na kuhusu hela niliifanyia nini nilifungua business imebuma nimelipia watoto ada na nyingine imetumika katika gharama za kawaida za maisha
 
Basi wachukue hiyo kadi na ili kila hela ikingia kwenye Akaunti yako wachukue kiasi hadi hapo deni lao litakapoisha. Tahadhari usiwape namba yako ya siri na ingependeza kama mtakubaliana kuwa utakuwa unalipa kiasi gani kwa mwezi.
Je, nitamudu vipi gharama za maisha ikiwa kila hela yangu kwenye account wanaichukua?
 
Hicho unachokisema watu wa mkopo walishakitathmini, ndipo wakakupatia mkopo huku wakikata mshahara wako kupitia kwa muajiri,

inapotokea labda umeachishwa kazi, kwenye mkopo huwa kuna bima ya kuachishwa kazi ambao wataubeba wao. kama wewe ndio umeamua kuacha kazi, huo mzigo wa kulipa deni utakuangukia wewe.
 
Hivi hizi hela huwa mnapeleka wapi? Kuna mtu mshahara ukiingia hizo taasisi zinabeba anabakiwa na elfu80. Hivi mtu mwenye familia 80elfu unafanyia nini na una mke(mama wa nyumbani) na mtoto
 
Back
Top Bottom