Ikiwa mwajiri hajatekeleza makubaliano, naweza kujiuzuru kazi in 24 hrs? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikiwa mwajiri hajatekeleza makubaliano, naweza kujiuzuru kazi in 24 hrs?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chikuta, Jun 10, 2009.

 1. c

  chikuta Member

  #1
  Jun 10, 2009
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msaada kwenye tuta,

  Mimi nimekuwa katika ajira na mwajiri wangu mpya yapata mwaka sasa. Katika mkataba wa ajira, tulikubaliana mambo kadha wa kadha (mbali na mshahara), ni pamoja na marupurupu kwa ajili ya kodi ya nyumba, mawasiliano na usafiri.

  Hata hivyo, tangu mwenzi wa kwanza katika kumtumikia, marupurupu hayo yameonekana kuwa ni hadithi tu, kila kukicha ni subiri na subiri. Mwaka waisha sasa. Binafsi, nahisi kutotendewa haki na kwa maana nyingine nachukulia suala hili ni mpango tu wa kuhujumu utendaji na ufanisi wangu katika kazi.

  Baada ya kuwa nikifuatilia suala hili, pengine na hata kuonekana nakuwa bughudha, taratibu nilianza kuishiwa na hari ya kazi na pia kuanza kufikiria kutafuta ajira mpya.

  Hivi punde nimepata wito kutoka kwa mwajiri mpya, ambaye agependa nijiunge naye mapema iwezekanavyo.

  Swali langu la msingi ni je, naweza kuamua kuacha kazi kwa short notice? Moja pia kati ya makubaliano katika mkataba ni kutoa notice ya mwezi mmoja!

  Naomba msaada kwa wenye kujua na kuwa na uzoefu na masuala haya ya haki za wafanyakazi na sheria kwa ujumla.

  Ahsanteni
   
 2. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #2
  Jun 10, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi sikushauri kufanya hivyo kwani makubaliano ya wewe kutoa barua ya mwezi mmoja huenda ikakubana mwanawane!!

  Ila kidogo inakuwa tricky kuamua...
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ungeenda jukwaa la sheria, kaka
   
Loading...