Ikiwa mradi wa Songo Songo gharama ni USD 420M; kwa nini Bomba la gas Mtwara USD 1200M? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikiwa mradi wa Songo Songo gharama ni USD 420M; kwa nini Bomba la gas Mtwara USD 1200M?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Synthesizer, Jun 23, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,331
  Likes Received: 3,124
  Trophy Points: 280
  Japokuwa wengi tunamuona Waziri mpya wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo kama shujaa mkombozi, lakini inashitua sana kututangazia kwamba bomba ka gas toka Mnazi bay hadi Somangafunga litaigharimu serikali USD 1200. Tunakumbuka kwamba bomba la gas toka kisiwani Songo Songo hadi Ubungo, kutia ndani na mitambo ya kusafishia gas pale kisiwani Songo Songo na fidia kwa watu, viligharimu kama USD 420, inatutia shaka sana kama hizi gharama za bomba la gas ya Mnazi Bay zina mshiko.

  Mradi wa Songo Songo ulijengwa na kampuni ya Canada ukisimamiwa na Benki ya Dunia, na huu wa Mnazi Bay ni wa Wachina.

  Je, inawezekana kwamba Prof. Muhongo kaingizwa katika mchezo asioujua? Je inawezekana kwa kuwa Songo Songo ulipitia Bank ya Dunia wao waliziba mianya yote ya ufisadi tofauti na Mnazi Bay?
   
 2. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,331
  Likes Received: 3,124
  Trophy Points: 280
  Utafiti zaidi unaonyesha Songo Songo iligharimu USD 320M na sio $420 kama nilivyosema hapo juu:

  The main sponsor of the Songo Songo $320m project was AES Sirocco of the US; the other sponsor was PanAfrican Energy, formerly Ocelot International. Investment in the project came from AES, PanAfrican Energy, Tanzania Electric Supply Company Ltd (Tanesco), Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC), UK investor CDC Group plc, Tanzania Development Finance Co Ltd (TDFL), the European Investment Bank and the World Bank, these last two through the Tanzanian Government.
   
 3. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Duh! uyu mzee anatia huruma! kaingizwa town, epa nyingne inakuja
   
 4. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,424
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Songosongo Gas pipeline ina urefu wa km 217 kuanzia Somanga Funga hadi Ubungo mpaka Wazo Hill. Mnazi Bay-Dar Gas Pipeline ina urefu wa km 290 kutoka Mnazi Bay hadi Somanga na km 207 hadi Ubungo. Hii ni urefu tu bado upenyo- inaaminika upenyo(diameter) wa Bomba Jipya ni mara mbili ya ule wa Songosongo. Na fungakazi, Mnazi Bay inajengwa zaidi ya miaka 10 tangu ule mradi wa Songosongo ujengwe.

  Si vizuri kuanza kupaka matope bila ya utafiti wa kina.

  "...
  Tanzania Petroleum Development Corporationsongo_songo.htm -

  After processing, the gas is be transported through a 25km 12-inch pipeline from Songosongo to Somanga Funga, and from Somanga Funga through a 207km ...

  The planned 24 to 36-inch gas pipeline would be 532 kilometres long from Mnazi Bay to Dar es Salaam via Somanga Fungu and would have ..

  Nadhani utakuwa umejua ulichotaka kukisema sasa
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Chezea shm yenye mkono wa mtu wa ccm wewe!
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Kwa maelezo haya inaonyesha bei inaweza kuwa sawa ukizingatia miaka 10 imepita tangu mradi wa kwanza hadi wa sasa...bado tuna imani na Prof muacheni achape kazi maana hakwenda kuomba uwaziri walimfuata kufuatana na merits zake!!!piga kazi uzalendo mbele!!
   
 7. M

  Makupa JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  wana jf fanyeni utafiti kwanza kabla hamjaanza kukurupuka na kuanza kulalama kitu msichokijua hata kidogo
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sina tatizo na gharama na gharama za mradi kwa sababu zinaweza kulingana na ukubwa wake. tatizo langu ni mantiki ya kusafiisha Gesimba kutoka Mtwara mpaka Dar. Kwa nini gesi isiwe processed hukohuko Mtwara? Uzalishwe umeme Mtwara na wenyewe ndio usafitishwe. Ukisafirish umeme unaweza kuipayia mini na vijijini vilify njiani, lakini hiyo gesi haitawezekana kuwanufaisha wanavijiji njian bombarded litakamopita. Uki-process gas Mtwara unangeza uwezekano wa ajira katika mkoa huo ambao ni moja ya mikoa maskini nchini.
   
 9. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Ufisadi huibuliwa kwa kuanzia kuuliza. Uliza tu mleta maada ili tupate justification.
   
 10. M

  Makupa JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu kuna processing plant mbili zitajengwa mtwara hivyo usiwe na hofu
   
 11. M

  Makupa JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Akili yako imekuwa na mawazo finyu, yaani unaamini kabisa kuwa chochote kinachofamyika ni ufisadi.
   
 12. kussy

  kussy JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 15, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  nina uhakika watumiaji wengi wa Gas watakuwa DSM, magari ni mengi na population ni kubwa hivyo ni sahihi zaidi kujenga bomba hilo kupunguza gharama za usafirishaji na usmbazaji, chukulia mfano maji ya Ruvu yangekuwa yanaletwa Dar kwa Malori ingekuwaje?
   
 13. Pastor Achachanda

  Pastor Achachanda JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 3,011
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Hakuna mradi ninaouamini ukafanyika Tanzania bila kaufisadi pembeni.Cha msingi wanachofanya ni kutupindua viini ubongo.
   
 14. B

  Bob G JF Bronze Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hizo ni 20% za mikataba ya serikali ya ccm zinazoongea bei ya miradi kuwa ghari sana,
   
 15. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kumbukeni hao wa-Canada ndio wamefisadi mpaka leo hawajalipa serikali zaidi ya Tsh. 30 Bln za mrabaha wa hiyo biashara ya gesi. Hata wakati wa kujenga Tazara propaganda ndio zilikuwa hizihizi. Kawaida yao kwa wamagharibi kuwaogopa wa-China ili waendelee kutunyonya.
   
 16. talentbrain

  talentbrain JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 903
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Nasikitika na jinsi kila kitu kinavyokuwa centralized dar! Hapa naona mapungufu makubwa, eti kwakuwa michikichi mingi inapatikana kgm na kwakuwa soko kubwa la mawese lipo dar basi viwanda vya mawese viwe dar!
  Vipi kuhusu makaa ya mawe kiwira tutapotaka kuzalisha umeme wa makaa nayo yatasafirishwa hadi dar kwakuwa kuna soko la makaa kwa ajili kupikia?
  Chamuhimu ni kuangalia ipi ni bora na rahisi.
  Huwenda mafuta yakagunduliwa ziwa Tanganyika, sitashangaa processing ikafanywa dar.
   
 17. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,331
  Likes Received: 3,124
  Trophy Points: 280
  Mie nadhani watanzania tumeshakuwa sugu wa kughilibiwa, ndio maana tunaona kila kitu sawa. Kwanza, ikiwa kuna bomba za gas ya Mtwara zitawekwa kuanzia Somanga Funga hadi Dar, basi gharama ya kuweka bomba za gas toka Somonga Funga hadi Dar ni ndogo sana ukilinganisha na gharama nzima ya huu mradi. Sababu ni kwamba bomba hizo zitapita katika njia iliyothibitishwa tayari (leeway) ya mradi wa Songo Songo. Kwa hiyo kazi ni kufukua na kufukia bomba katika njia ya mradi wa Songo Songo. Hii inapunguza sana gharama tofauti na kutafiti njia mpya (new leeway).

  Hivyo basi kimsingi, tulinganishe gharama ya Mnazi Bay yas na pipileline ya 290km Vs Songo Songo gas na piline ya 207km katika uwiano wa USD 320 kwa USD 1200.

  Kusema Songo Songo nio mradi wa miaka 10 iliyopita haina mshiko, hizi gharama ziko katika USD sio Tshs ambayo inashuka thamani kila siku. Nakubali kwamba kweli miradi ina utofauti, lakini thamani ya hizi project mbili kuwa na tofauti ya asilimia 275% ni jambo lenye kutia shaka. Kwanza mradi wa gas ya Mtwara hauna kipengele kikubwa cha kulipa fidia wakazi.

  Ila kama mnataka tukubali kwa kuwa Watanzania tumezoea kuwa malofa wa hii miradi ya nje, sawa, na tuendelee na ulofa wetu. Mie binafsi ninatilia shaka sana hizi gharama za mradi wa gas ya Mtwara.
   
Loading...