Ikiwa leo ni siju ya Demokrasia duniani , Hiki ndicho kinachoogopwa na CCM

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,571
217,928
Subpost 1 - Happy birthday to you Mwenyekiti. Umeongoza struggle ya kuleta demok.jpg

Bila kumung'unya maneno ccm imekwishapoteza ushawishi kwa wananchi , haina tena uwezo wa kukusanya watu wa kuwaeleza chochote , ili ipate watu wajinga ni lazima idanganye kwamba kuna wachina watagawa hela .

Na baada ya kutambua hilo Mwenyekiti wa CCM ndugu Magufuli akaamua kupiga marufuku demokrasia ya vyama vingi ili kuivisha taulo ccm ambayo tayari ilishadhalilika katikati ya soko.

Ikiwa leo ( 15 september ) ni siku ya demokrasia duniani tunawaomba Wazungu waendelea kuinyima misaada nchi hii mpaka pale itakaponyooka na kuruhusu uhuru wa kujieleza na demokrasia ya kweli
 
mkuu moderator heshima kwako , kuna error ndogo kwenye heading , Mungu akikuwezesha unirekebishie tafadhali , natanguliza shukrani
 
Demokrasia si vyama vingi tu hata chama kimoja ni demokrasia kama serikali ni ya watu, kwa ajili ya watu na imewekwa na watu. uwepo wa utitiri wa vyama vya siasa vyenye mrengo hasi ni mzigo mkubwa sana kwa hicho unachokiita demokrasia.

CCM haiogopi demokrasia na hayo ni mawazo yenu wapinzani mnapopata hisia za kushindwa. CCM inataka vyama viwe vingi ili kuleta ushindani lakini vyama vya upinzani Tanzania kusema kweli ni mzigo mkubwa sana kwa maendeleo yetu, hatuwezi kuendelea kama vyama hivyo ndio vinaitwa vya kidemokrasia
 
Umeandika mengi lakini yote ni pumba tupu , walioasisi mfumo wa vyama vingi hawakuwa wapumbavu kama mnavyodhani na ndio maana nusu ya viongozi waliopo sasa mmewaokota upinzani
 
View attachment 1208092

Bila kumung'unya maneno ccm imekwishapoteza ushawishi kwa wananchi , haina tena uwezo wa kukusanya watu wa kuwaeleza chochote , ili ipate watu wajinga ni lazima idanganye kwamba kuna wachina watagawa hela .

Na baada ya kutambua hilo Mwenyekiti wa CCM ndugu Magufuli akaamua kupiga marufuku demokrasia ya vyama vingi ili kuivisha taulo ccm ambayo tayari ilishadhalilika katikati ya soko.

Ikiwa leo ( 15 september ) ni siku ya demokrasia duniani tunawaomba Wazungu waendelea kuinyima misaada nchi hii mpaka pale itakaponyooka na kuruhusu uhuru wa kujieleza na demokrasia ya kweli
Huma haja ya kuwaaomba wanyime misaada we sema ccm iendelee kukandamiza watu kila kitu kitakuwa poa waliokomafichoni watatoka tu siku sio nyingi tutaimba wimbo mmoja unaojukikana kila kona ya nchi
 
Demokrasia sio kama Pepsi Cola kuwa lazima ifanane Dunia nzima

PM wa Uingereza badala ya kushawishi Bunge la Uingereza kwa kukubaliana na mpango wake wa kujitoa Umoja wa Ulaya ( Brexit) ameamua kusitisha Bunge Mpaka hapo atakapo jitoa

Na sie tunaweza kusitisha Shughuli za Kisiasa baada ya uchaguzi kuruhusu Rais atekeleze ahadi
Marekan baada ya Uchaguzi umeona kuna vugu vugu la Siasa kwa maana yaMikutano ya hadharan pamoja na madhaifu ya Trump?

Ndani ya hivyo vyama vinavyolilia Kinachoitwa Demokrasia havina Demokrasia
 
Mkuu mengine nayaacha ila kwa marekani umedanganya.unajua mpambano unaoendelea marekani now kuelekea uchaguzi wa mwakani?
 
Back
Top Bottom