Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 129
Tangu matokeo yatangazwe kwa ujumla nimekuwa ninajiuliza maswali mengi sana moja wapo kama wapinzani na wanamapinduzi hawaikubali tume na kwa mfano chadema na dr slaa wamegomea matokeo kuna ulazima kweli wa kuwapeleka wabunge bungeni? kama upo kwanini? na kwanini iwe sitaki nataka? Naomba tusiwe wanafiki hapa kama umeamua kuoga basi huna budi kuvua nguo na ukishayavulia maji nguo huna budi kuyaoga. Chadema na Slaa waamue moja kukataa matokeo na kushinikiza wabunge wao wasiingie bungeni nadhani dunia itasikia na sio kwa chadema tu hata vyama vingine vya upinzani! sio kukaa kipembeni unalalamika huku unakula posho wakati sisi watanzania wa kawaida tukiumia na ugumu wa maisha.
Mtafakari tusikubali kutumiwa jamaniiiiiiiii
Mtafakari tusikubali kutumiwa jamaniiiiiiiii