Ikiwa hadi leo Afande Muroto hana majibu ya nani alimshambulia Tundu Lissu asituaminishe kwamba anaweza kutupa majibu ya yaliyompata Mbowe

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Mnyika amehoji kwa nini jeshi la police litoke haraka na kauli ya kwamba tukio la kushambuliwa Mh Mbowe ni la kawaida?
Wamefanya uchunguzi wapi?

Mlimuumiza Kubenea mkasingizia mwanamke. Kwa Ulimboka mkasingizia mwanamke. Kwa Kibanda mkasingizia mwanamke. Kwa Lissu mkatunga zikashindikana. Kwa Akwilina mkadai risasi ilitoka juu! Kwa Mdude mkachomeka hoja ya mwanamke. Sasa mmemuumiza Mbowe, bado mnataka kusingizia mwanamke?

Lakini pia watu wanahoji kwa nini Mbowe hana ulinzi. Tunachotakiwa kuhoji ni kwa nini mtanzania ashambuliwe tu akiwa anaelekea kwake. Kutokuwa na ulinzi hakutoi tiketi ya binadamu kushambuliwa!

JF kennedy , Rais wa 35 wa Marekani alikua na the best security detail in the world lakini bado alishambuliwa na kupoteza maisha ! Kuwa na ulinzi au kutokua na ulinzi kusiwe ajenda, ajenda kuu ni kwa nini kiongozi ashambuliwe!

Lissu alipigwa Risasi 16 Bila aibu wakasema alipanga mwenyewe, Mnashangaa leo wanaposema Mbowe alianguka kwenye Ngazi? Hawa sio Binadamu, wako tayari kupata madaraka kwa Damu za Watu.

Tunaposema ubaguzi upo kila sehemu duniani hii ndiyo maana yake. Bora ubaguzi wa mzungu kuliko wa mtu mweusi. Mtu mweus anakubagua, anakunyanyasa, anakufilisi, anakubambiza kesi za uwongo. Ukipona uko anaamua kukuvamia akuue ili upotee kabisa. Viongozi wa Africa ni mashetani.

Kama hamtaki Vyama Vya Upinzani nchini pelekeni Bungeni Mswada wa kuvifuta vyama vya upinzani nchini ili mbaki peke yenu ila kuwaua, kuwapoteza, kuwapiga risasi na kuwajeruhiwa Viongozi na Wanachama wa Upinzani sio sawa, huu ni ushetani uliopitiliza.

Matumaini yangu Freeman atapata nafuu. Lakini kwa sasa hatuna budi kujisaili tena,tumefikaje hapa? Hawa ndio sisi kweli au ni wengine? Mashetani hawa wametokea wapi, au tunao siku zote bila kuwajua?

Jambo wanalopaswa kufahamu CHADEMA, ni kwamba muda wa kufanya siasa za kistaarabu umekwisha

Mr mkiki.
 
Katika hali ya kawaida,watu waliomshambulia Lissu,watakuwa hai au nao wao watakuwa wameshughulikiwa ili kupoteza ushahidi iwapo walitumwa?

Yaani watumwe(kama walitumwa), alafu mpaka leo hii wawe tu uraini huko kukiwa na shinikizo la uchunguzi kufanyika?

Kama walitumwa,waliowatuma hawawezi kuhofia kuwa walionekana na mashuhuda wa lile tukio?

Swali gumu, pengine kuliko yote ni je,kama walitumwa,waliowatuma hawatakuwa na hofu ya kutajwa mahakamani iwapo wahalifu hao watapandishwa kizimbani?

Kingine:kama walitumwa na kazi hawakuikamilisha,waliowatuma watawaacha hivi hivi tu?

Ipo Siku majibu ya maswali haya na mengineyo kuhusu tukio hili, yatapatikana.
 
Katika hali ya kawaida,watu waliomshambulia Lissu,watakuwa hai au nao wao watakuwa wameshughulikiwa ili kupoteza ushahidi iwapo walitumwa?

Yaani watumwe(kama walitumwa) alafu impala leo hii wawe tu uraini huko kukiwa na shinikizo la uchunguzi kufanyika?

Kama walitumwa,waliowatuma hawawezi kuhofia kuwa walionekana na mashuhuda wa lile tukio?

Kingine:kama walitumwa na kazi hawakuikamilisha,waliowatuma watawaacha hivi hivi tu?

Ipo Siku majibu ya maswali haya na mengineyo kuhusu tukio hili, yatapatikana.
Subiri kesho Kubenea anataka kumwaga mboga!
 
Katika hali ya kawaida,watu waliomshambulia Lissu,watakuwa hai au nao wao watakuwa wameshughulikiwa ili kupoteza ushahidi iwapo walitumwa?

Yaani watumwe(kama walitumwa), alafu mpaka leo hii wawe tu uraini huko kukiwa na shinikizo la uchunguzi kufanyika?

Kama walitumwa,waliowatuma hawawezi kuhofia kuwa walionekana na mashuhuda wa lile tukio?

Kingine:kama walitumwa na kazi hawakuikamilisha,waliowatuma watawaacha hivi hivi tu?

Ipo Siku majibu ya maswali haya na mengineyo kuhusu tukio hili, yatapatikana.
Hivi kweli unatumwa ukamuue flani halafu unatumia risasi nyingi vile!...

Basi serikali ya Tanzania haina wadunguaji...
 
Back
Top Bottom