Ligaba
JF-Expert Member
- Oct 12, 2018
- 1,045
- 2,821
Inashangaza kidogo, hivi hata tuliowakabidhi dhamana ya maisha yetu hawalitambui? Hawajui walipoomba kura zetu walikuwa na maana ya kuomba kulinda uhai wetu?Kwamba hawajui mmoja wa adui yetu mkubwa ni Maradhi? na sio Vita na majirani zetu, wapinzani wao kisiasa hata hili nao hawalijui?
Hivi ingekuwa vita ya msituni saa hizi si wangelikuwa wameshatenga bajeti kubwa ya dharula? Au kwa vile vita vya msituni madhara yake ni kuwatoa madarakani? Ipo wapi bajeti kubwa ya kupambana na adui maradhi? Au hawaoni hii ni vita kubwa zaidi ya msituni? MWENYEZI MUNGU TUJALIE.
Na sisi watanzania tunapowachagua Hawa watu huwa tunafahamu kwamba tunawapa dhamana ya uhai wetu? Kwamba wao ndio marefarii wa uhai wetu? Hivi tunafahamu kero za marefarii wakiamua kutokuwa upande wako?
Mbona marefarii hawa hawako upande wetu, kwa nini wamechagua kuwa upande wa ugonjwa ili watuangamize?. Hivi kuna sababu gani ya kuendelea ujenzi mkubwa wa umeme wakati unaowajengea wako katika taharuhuki inayotokana na hofu ya uhai wao? Hivi ni nani ajuaye hiyo Corona itaisha kwa mkakati gani na muda gani?
Aibu gani hii kusubiri misaada ya wazungu wakati sisi tunajenga reli, kweli? Kwa macho yetu watanzania tupembue tunaowachagua hawajui kwa nini tunawachagua. Usisikilize maneno ya wanasiasa hata wao hawajui tutavukaje, chukua hatua kubwa kujihami ila Mungu akikuvusha salama tathmini sana kwa wale unao wachagua.
Sent using Jamii Forums mobile app