Ilonga Msalabani
Senior Member
- Nov 23, 2012
- 111
- 36
Suppose umepata nafasi ya kuwa Rais wa Tz. leo keeping other factors constant ungefanya nini au mambo gani mema yenye kuleta maendeleo usisahaulike? I well come you all
ningeondoa viongozi wote wa serikali na kuweka wapya ....... i mean all tasisi za serikali nianze moja na wapya.....
1. Ningefuta nafasi za ukuu wa wilaya na mkoa.
2. Ningepunguza wizara kuwa chini ya 15
3. Ningepiga marufuku ununuzi wa magari ya anasa
4. Ubunge ungekuwa wa kujitolea - no mishahara
Suppose umepata nafasi ya kuwa Rais wa Tz. leo keeping other factors constant ungefanya nini au mambo gani mema yenye kuleta maendeleo usisahaulike? I well come you all
Suppose umepata nafasi ya kuwa Rais wa Tz. leo keeping other factors constant ungefanya nini au mambo gani mema yenye kuleta maendeleo usisahaulike? I well come you all
Safi mkuu, lakini hapo kwenye ubunge no mshahara??? Kwa nini ungondoa mshahara?
Yale magari ya anasa au magari ya kazi?
Na hapo wilaya zingeongozwa na nani sasa?
Ahsante mkuu.
mimi ninge fanya yafuatayo,
- Ningefufua reli na kuziboresha Ziwe mbili mbili moja kwenda moja kurudi.
- Miji yote pawepo na miundo mbinu ya reli ili kuwezesha city trains kama kwa wenzetu ulaya.
- Ningemalizia na kuboresha barabara zilizopo
- Ningeboresha mazingira ya kilimo kwa kutoa elimu kwa wakulima na kutengeneza mazingira ya masoko mazuri ya mazao ya wakulima.
- Ningepunguza kodi kwa wafanyakazi iwe atleat 10% na kupanua wigo wa kodi kwa kuhakikisha Kila mwananchi analipa kodi reasonably kuanzia Rais Mpaka mwananchi wa kawaida, na kutengeneza mazingira yanayovutia kulipa kodi kuliko kukwepa. Hii ingeongeza mapato ya serikali,
- ningeruhusu mashirika ya uma kufanya biashara na kulipa kodi kama kwa kutoa huduma bora.
- Ningepunguza utegemezi kwa mataifa ya nje kwa ku-focus zaidi katika kuimarisha uchumi wa ndani na vyanzo vyetu, Madini yote ni yetu hivyo tunge uza wenyewe,gesi an rasilimali zote tulizo nazo, ningepitia upya mikataba yote tuliyo ingia na kuuza mashirika mfano NBC
- na kila shirika lililowahi kuuzwa kwa namna yoyote na kuyafanya ya resikali na kuyaboresha upya na wale wazungu wanaofanya kazi nisinge wafukuza bali ninge waajiri wawafundishe kazi watanzania.
- ningefufua kile kiwanda chetu cha kutengeneza magari cha NYUMBU izae kila aina ya gari kama ilivyo TATA leo.
- Ningeboresha miji kwa kuweka huduma zote muhimu.
- Ningeongeza idadi ya Hospitali zenye hadhi ya rufaa na za kawaida na kuboresha sana Mazingira ya kazi na vitendea kazi vya Madactari
- ningechukua na kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazotolewa kwa chama changu tawala kutoka kwa vyama pinzani na kuweka mazingira ya amani na umoja wa kitaifa.
- Baadhi ya mambo ya msingi ninge iga mazuri ya nchi nyingine mfano USA, National interests first vyama baadae, ili kwamba chama kingine kikija mambo ya msingi kwa Taifa mfano Elimu na Rasilimali za Taifa ziwe priority always for the future of our nation.
- Ningepiga marufuku matendo ya kishetani mfano ushoga na mengine ya aibu ili kujenga taifa lenye tabia njema.
Chukua like yangu hio
Ningekua Dictaror
1-Ukidhibitika umetoa/kupokea rushwa kifungo cha maisha/kunyongwa
2-Ningebadili mfumo wa elimu kuwa na vitu vichache sana vyenye tija (kilimo, ufugaji, ufundi stadi) mambo ya elektoniki nigewaachia nchi wanayoyaweza hayo mambo kutupatia huduma (outsourcing)
3-Wabunge wangelipwa kutokana na jinsi wanavyotekeleza au kutimiza malengo na wajibu wao. Hakuna fixed amount kwa wote.
4 - Mawaziri wote wangekua wanaomba kama nafasi zingine za ajira, unajieleza kwa nini tukupe wizara fulani na utatufanyia nini ili usipowajibika tukuwajibishe.
5 - Ningeshirikisha wataalamu kuandaa mpango maendeleo wa nchi unaozingatia vipaumbele vya nchi na ufuatwe licha ya chama gani kipo madarakani. Mkipata nafasi ya kushika nchi, mnajua kabisa kwamba dictator Samaritan ametutoa A mpaka D, sisi inabidi tuendeleze from D to F kwa kipindi mtakachokuwa madarakani.
6 - Kwa kuwa ntakua Dictator, ntapitia mikataba yote na kufuta yoye yenye chembechembe za rushwa au maslahi ya wachache.
ningeondoa viongozi wote wa serikali na kuweka wapya ....... i mean all tasisi za serikali nianze moja na wapya.....
Ni kweli ukiwa dictator pia inasaidia. maana sometimes wananchi wanaandamana bila sababu za msingi kwa vile tu kuna uhuru wa aina fulani. Lakini hata usipo kuwa dictator unweza kuwa strict na sheria na misimamo ambayo itapelekea kufikia malengo ambayo watu watafurahi.
mara nyinyi hata familia kipindi wanajenga huwa ni kipindi kigumu kimaisha, kuna mambo fulani yasiyo ya lazima gharama zake hupelekwa mbele. Nchi pia hivyo hivyo, ili kuijenga lazima kuna watu waumie kwa manufaa ya baadae ya wengi. It is all about difficult decision making.