Ikitokea Tundu Lissu anateuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko mbeleni, utaunga mkono?

Tundu Lissu akiteuliwa na Raisi Samia kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, utaunga mkono?

  • Ndio

    Votes: 51 69.9%
  • Hapana

    Votes: 20 27.4%
  • Sijui

    Votes: 0 0.0%
  • Bado mapema

    Votes: 2 2.7%

  • Total voters
    73

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Kufuatilia kauli ya Raisi Samia kuwa atateu watu wa kufanya nae kazi bila kujali itikadi zao; je utaunga mkono ikitokea Lissu anateuliwa kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali?

Mbali na kupiga kura,tutoe pia maoni na ushauri au hata angalizo(kama unalo) kwa wapinzani juu ya swala hili ambalo litakuwa ni geni kwa nchi yetu tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini mwaka 1992.

Na je, huu ni wakati wa kubadili katiba ili kuruhusu tuwe na serikali ya mseto na pia kuruhusu mawaziri wateuliwe nje ya ubunge(bila kuwa wabunge)?

Tundu Lissu nimemtumia kama mfano tu ili tupate mawazo ya watanzania kuhusu nia hii ya Raisi Sami ila hii inawahusu wapinzani wote.

Maoni yetu yanaweza kusaidia nchi yetu kuliko hata tunavyodhani.
 
Binafsi naona ni wazo zuri ila kuna umuhimu wa kujipa muda ili kusoma dhamira ya Mama Samia na kuona kama anamanisha anayoyahubiri kwa vitendo.

Hata hivyo, hatua hii inaweza kuwajenga wapinzani kisiasa ikitokea wanaamua kujiuzulu nafasi zao pale watapoona ushauri wao na masilahi ya Taifa hayazingatiwi na watawala hasa itapokuja kuthibitika kuwa walifanya maamuzi sahihi.
 
Ndiyo nitaunga mkono. Unajua mwendazake alikuwa ana akili za kukalili formula za chemistry tu lakini busara alikuwa hana hata kidogo aliamini tu mtumishi mpaka awe katika chama cha mapinduzi hakujua kwamba upinzani ulikuwepo kwa sheria ya bunge na katiba ili kuuwa kama alivyokuwa anafanya alibidi sheria ya bunge na katina vihusishwe
 
Umeniwahi post.
Binafsi naona kabisa karibuni wote upinzani waliopoteza ubunge wao huenda wakaula
Ila wakiingia serikalini wawe makini sana kwani wabaya wao bado wako kwenye system na sidhani kama wanapenda, hivyo wanaweza kuwatengenezea kashifa kwa kuwaingiza kwenye mtego mfano kusaini mikataba mibovu, n.k.
 
Akifanya hivyo Mama hakika atakua ameonesha uzalendo wa kweli pia asitarajie kwamba wateule wake wote watakua wanamuungo mkono so ajipange kwenye hizo teuzi.
 
Hii issue complicated sana, naona watu wanafurahia hiyo kauli ya Rais kuwa tayari kuwateua wapinzani lakini napata shaka hao wateuliwa kama watakuwa huru kutimiza majukumu yao huko serikalini, hapatakuwa na mizengwe huko ofisini toka kwa wasaidizi wao ambao kimsingi watakuwa CCM?

Kama pakiwepo na mizengwe itakayowazuia hao wateuliwa kutimiza majukumu yao then kuna uwezekano mkubwa wakaharibu kazi, na kama wakiharibu kazi lawama watatupiwa wao binafsi, kwamba hata hao wapinzani mliowaweka hawana jipya, hili litakuwa doa litakalowaharibia wapinzani, wawe makini sana.

Kufanya kazi na serikali ya CCM ni sawa na kujiingiza mtegoni bila kujua, hasa mpinzani anapozungukwa na watu wenye tamaa ya vyeo na madaraka, sidhani kama atakuwa na uhuru wa kufanya kazi zake vizuri, mfano ni RC Mghwira alivyosumbuana na kina Sabaya Moshi.

Hao CCM wameandaliwa vipi kisaikolojia kufanya kazi na wapinzani, je, wao wapo tayari au ni wazo binafsi la mwenyekiti wao? watu waliokuwa wanawatukana na kutumia polisi kuwaharibia mikutano yao au kuwaibia kura leo wanaambiwa wakae nao ofisi moja...
 
Ndiyo nitaunga mkono. Unajua mwendazake alikuwa ana akili za kukalili formula za chemistry tu lakini busara alikuwa hana hata kidogo aliamini tu mtumishi mpaka awe katika chama cha mapinduzi hakujua kwamba upinzani ulikuwepo kwa sheria ya bunge na katiba ili kuuwa kama alivyokuwa anafanya alibidi sheria ya bunge na katina vihusishwe
Chuki hupofusha. Prof. Mkumbo na Mama Mgwila walipoteuliwa walikuwa chama gani?

Shida mnapenda maneno ya kufurahisha. Waswahili husema vitendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno.
 
Chuki hupofusha. Prof. Mkumbo na Mama Mgwila walipoteuliwa walikuwa chama gani?

Shida mnapenda maneno ya kufurahisha. Waswahili husema vitendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno.

..mbona haraka-haraka waliondoka upinzani?

..tunataka watu watakaoteuliwa wakiwa upinzani, na waendelee hukohuko wakati wakitumikia ktk nafasi zao.
 
Back
Top Bottom