Ikitokea, Traffic Police mna kesi ya kujibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikitokea, Traffic Police mna kesi ya kujibu

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Columbus, Apr 13, 2011.

 1. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni muda mrefu sasa nashuhudia vijana mateja wakivamia malori na kukinga mafuta yaliyobaki kwenye foleni, jana niliwakuta Tazara wakikinga mafuta wengine wakiwa wanavuta sigara.

  Nataka kujua hawa polisi wa usalama barabarani wanalijua hili?nina hakika madereva wa malori hayo wanaona na hawachukui hatua yoyote.Na je ikitokea(siombei)mlipuko wa moto katika foleni hizi ni nani wa kumlaumu kama sio hawa polisi wetu?

  Ninachojua TAMKO LA SERIKALI LA SIKU MOJA LINATOSHA KUTUEPUSHA NA BALAA HILI LISITOKEE


  Nawasilisha
   
 2. C

  Clego Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio Trafiki tu, kuna wale wanao patrol na piki piki wanawaita tigo fasta, wakiwaona huwa wanapita tu wao wako bize na kuangalia Road licence na bima kama imeisha. Wana uwezo wa kusoma vibali vya kwenye vioo vya gari hata umbali wa mita zaidi ya kumi.
   
 3. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mimi naamini askari wetu hawajui wajibu wao ni nini maana ya usalama wa raia, na pia wamejenga silka mbaya ya kuwa kama akifanya kazi bila chochote nje ya mshahara wake anaidharau.

  Nimeshashuhudia katika nchi za wenzetu askari wakiwa katikati ya barabara kuu wakiongoza magari sehemu ambayo waya wa umeme umekatika na kuangukia barabarani, nilisikitika ktk nafsi na kujisemesha...."wenzetu wako mbali sana"...lakini kwetu mara nyingi askari wanafika baada ya tukio.
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Sio polisi tu hata wananchi wote tunatakiwa kukemea au kumwita huyo polisi mara moja kwenye tukio kama hilo. Mimi siku moja pale Ubungo maji nilimfokea mkinga mafuta ambaye alikuwa na sigara iliyowashwa mdomoni huku akikinga mafuta kwani gari yangu ilikuwa jirani sana na hilo lori ingawaje ilikuwa na bima 'comprehensive'.

  Na hao wa malori wawe wanashusha mafuta yote au matenki yawe na koki pale kwa chini ya tank ili kutoa mpaka tone la mwisho.
   
 5. N

  Nanu JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sure it is a big risk!!!!
  We are waiting for a "kaboom" to happen for action to be taken.
  It is unfortunate that we always react after something has happened instead of preventing something from happening!
   
 6. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Wakinga mafuta wote huwa wako full ukimsogelea kwa nia ya kumkataza anaweza kukudhuru, inasemekana walishawahi kuuwa mtu kwa bisibisi, ndiyo maana madereva huwa hawashughuliki nao.
  Mafuta machafu ni mazito kidogo kulinganisha na petrol au diesel ndiyo maana hawayamalizi kabisa wakati wa kushusha yanakuwa yanaendelea kutelemka kidogokidogo wakati gari inatembea na si ajabu kupata walau nusu ndoo kwa compatment zote.
   
 7. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama wanajihami kwa bisibisi basi ni hatari, ni vizuri wahusika kama polisi ndio wadhibiti hali hii. Hiyo jana niliona wakikinga diesel kwenye mifuko ya rambo na sina hakika huwa wanamuuzia nani!!!! Kama ni sisi wenye magari tuache kununua mafuta nje ya vituo.
   
 8. k

  kamimbi Senior Member

  #8
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku gari ikilipuka najua watakufa watu wengi na wengine wengi kuumizwa, nadhani kwa hili njia sahihi ni kuchukua sheria mkononi dhidi ya hawa vibaka ili wafe waliyojiharalishia kifo, huu ni muda wa kutekeleza kwa vitendo yote ambayo ni ya muhimu then serikali inayapuuza; si unakumbuka yaliyotokea kule Tegeta? sasa ndo wakobize kufuatilia, but i believe on prevention is better ehan cure.
   
 9. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Siyo traffic tu bali polisi wote
   
 10. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nimepata ushahidi wa picha,sikuweza kupata vizuri niliogoa bisibisi.
   

  Attached Files:

Loading...