"Ikitokea siku Marekani akanisifia,Lazima nitarudi nyuma na kuangalia nimekosea wapi?" Mwalimu Julius Nyerere.

MduduWashawasha

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
1,653
2,000
Mawazo mazuri ila shida ni kwamba wazungu wana control almost everything dunian na pale pasipo maslahi wanapakaushia.dunia hii ni kama ya kwao manake ss tunakopi tu vitu toka.maujuzi yote kemia,biolojia jiografia uchumi ,udaktari ,uhasibu fedha ,bima cjui nn vimetoka kwao.susi waafrika sijui ni jambo gani mbalo tumeligundua na wazungu waje walisome kwetu na mwisho sisi kuamua kama wanapata bachelor,masters au phd degree?
 

chipa GM

JF-Expert Member
Jan 21, 2012
1,632
2,000
Baada ya muda mrefu sasa marekani na vi baraka wake waingereza wametoa tamko kuwa Rais Magufuli ni dikteta mwingine wa Afrika.Katika mtazamo mpana zaidi,tafsiri ya kauli hii ni,"Magufuli ni mwamba mwingine wa Afrika." mwaka 2016 wakati uingereza wapo katika vuguvugu la kutaka kujitoa katika umoja wa ulaya yupo mwanadada mwanaharakati ambaye alisimama kidete kutetea uingereza asitoke katika umoja huo wa ulaya.Unajua kilicho tokea? yule mwana Dada aliuawa katika mazingira ya kutatanisha na hakukuwa na taifa lolote kutoka ama Afrika ama Asia ama marekan ambao walilaani au kumshutum David Cameroon kuwa ni diktet au hata kuitangazia dunia kuwa uingereza si mahala salama pakwenda.Mwaka 2011 Uingereza na Marekani kupitia Jeshi la NATO walifanya uvamizi katika taifa huru(sovereign state) Libya wakavuruga amani ya Libya wakamuua kiongozi ambaye alichaguliwa na wanalibya.Hakuwahi kutokea mataifa ama ya Asia ama ulaya kulaani tukio lile ambalo lilienda kuvuruga hali ya amani na uchumi w Libya.

Marekani katika kipindi cha mwaka 2013-2014 kulitokea matukio kadhaa ya ukiukwaji wa haki za binadamu,polisi waliuwa kwa kukusudia vijana wenye asili ya kiafrika tena mpaka maandamano yalifanyika lakini hakuna aliyejitokeza ama Afrika ama ulaya kulaan matukio hayo.

Pamoja nakwamba kuna taasisi kubwa duniani inayoungnisha mataifa yoote na kuhughulia kero zao pale zinapo jitokeza,Somalia mpaka sasa si Marekani,si Uingereza ambaye alishawahi kujitolea kwenda kuweka usalama katika mataifa hayo,zaidi kila siku viongozi Wao hutoa kauli za kudhalilisha viongozi wa Afrika na watu wake.Sudan kabla ya kutengana mwaka 2011 nakuwa mataifa 2 Sudan kusini na kaskazini na hata kupelekea machafuko Sudan kusini,si marekani wala si Uingireza ambaye alishawahi hata kukanyaga tu katika ardhi ya mataifa hayo na kutafuta masuluhisho.

Sikuzote Marekan na Uingereza watalaumu na kuingilia Uhuru wa taifa Fulani endapo katika taifa hilo kuna(dhahabu,gesi,mafuta,diamond na rasilimali nyingine kama hizo) na huwa wakali zaidi endapo akitokea kiongozi jasiri na mwenye msimamo wa kuzilinda na kuzitetea raailimali hizo zisitumike kwa maslah ya Wao.

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani,kumeshafumuliwa mikataba ya madini na sasahv kuna 50-50 yaani kati ya taifa na wawekezaji kuna mgawanyo sawa wa faida,kwanini wasiseme Rais dikteta?? miaka yoote wamejichukulia bure leo wanaacha faida kwann wasiseme Rais dikteta?? Uingereza ametawala Tanganyika tangu baa ya vita kuu ya pili ya dunia lakn aliacha mainjinia wasomi 2,aliacha taifa watuwake 98% hawajui kusoma na kuandika.Aliacha taifa huduma za maji upatikanajiwake ni asilimia 0.005%,aliacha taifa ambalo matumizi ya nishati ni 0.01%, aliacha taifa kuna reli ambayo zilijengwa kutoka maeneo wanakozalisha malighafi na kupeleka mjini basi tena reli hizo hazikuweza kutuunganisha hata na Rwanda na Burundi ambao wakati wa ujeruman walikuwa sehem ya Tanganyika.Uingereza wanaondok Tanganyika walisha waua watu wenye ujuzi kichwani na wengine wakakatwa viganja vya mikono(ukatili huu hawajawahi kusema) Uingereza wanaondoka,Km za lbarabara nchi nzima ilikuwa 1000Km. katika nchi yenye ukubwa wa 947,303KM.Katika nchi ya watu ambao hawa kuzidi hata 20000 walishindwa hata kujenga zahanati kila sehem,pamoja na kuwa tuna 6% ya maji yanayopatikana ndani ya nchi,walishindwa hata kujenga visima vya maji kwa watanganyika.Pamoja na kwamba walikaa tangu mwaka 1919 mpaka 1961 Lakin hawakujenga hata chuo kikuu kimoja zaidi waliacha taasisi ya ustawi wa jamii tu,na ilikuwa ni kwamaslahi yao binafsi.

Leo hii ambapo wanamwita Rais Magufuli dikteta,Tanzania nzima imeunganishwa na barabara, 60% ya watanzania wanatumia nishati ya umeme,ukiachana na mareli yao,tunajenga reli zetu tena ni standard kwa maana sio tu kuwa ni treni za umeme,lakn kwa Afrika ndio teen pekee zitakazokuwa zinaenda kwa kasi ya uhakika.Leo hii,achana na kila kata kuwa na zahanati masuala ya watu kulala chini katika mahospital zetu inaenda kuwa historia,sasahivi Tanzania ya miaka 50 tu ya Uhuru wake tunazungumzia uchumi wa viwanda,wasichojua watu wengi katika mataifa Mengi ya ulaya na Marekani,miaka yao ya mwanzo ya Uhuru(50) Ukiangalia utaona yalikuwa ni mataifa ya hovyo,yalikuwa kama dust bin....

Leo,tunazungumza Tanzania inayojenga mahusiano mazuri ya kiuchumi na mataifa ya ukanda huu kwa kujenga reli itakayotoka Tanzania mpaka Rwanda.Kwanini wasiseme Rais Magufuli dikteta?? jambo ambalo Wao katika miaka yao 50 ya kwanza walishindwa halafu wanaona taifa ambalo linaviongozi wa awamu 4 tu wamefanikiwa kufanya mambo ambayo Wao walifanya kwa miaka 100!!

Kinachotushangaza nipale wapinzani wa Tanzania wanaposhangia haya mambo na kuzania ukienda Marekani maisha ni kama peponi.Ivi tujiulize bila unafiki,unazani kwa aina ya siasa wanazofanya upinzani wa hapa kwetu wangekuwa ndo wapo marekan au huko uingereza wangekuwa wapi???

Kosa kubwa tunalotaka kufanya sisi ambao tunashuhudia haya ni kuruhusu Uhuru wetu wa kimaamuzi kuingiliwa na mataifa ya nje.Wakati wa awamu ya nne walitaka gesi,waka leta chokochoko za udini na kuua viongozi wakafeli.

Namalizia,wakati mwalm Nyerere anawaaga rasm umoja wa mataifa kabla ya kung'atuka aliwaambia"my last speech to the general assembly,I have described events and trends and needs as we are Tanzanians perceive them,to be silent when we see danger,to refrain from attaching policies which we see as contrary to the peace and justice to do this things will be to surrender our freedom and our dignity that we shall never do"

MAGUFULI TUBEBE TUNAIMANI NAWE!!!!
By Dr. John Mahimbo

ambacho hujui South Sudan kuna mafuta..na ile vita baina ya wao kwa wao kimsingi ina kolezwa sana na USA/U.K ...na bahati mbaya Uchimbaji wa mafuta kwa sasa unanchibwa na mchina..na ndiyo kutokana na hivyo wapo zaidi ya vijana 1500 wa south sudan Nchini China wamepewa schoralship moja ya mkataba wa uchimbaji huo..

Tanzania tukiona tunasemwa cha msingi tuangalie tunakosea wapi, mawazo ya Nyerere ya kipindi kile yanaweza yasiyo maajibu kwa matatizo yetu. Mimi binafsi sijaona ugumu wa RAis kufanya maendeleo kwa wnannchi na kuruhusu watani wake kisiasa kufanya siasa zao.
 

boaz mwalwayo

JF-Expert Member
Jan 27, 2015
5,766
2,000
Wanatanzia mnapenda kuwasemea wa Libya hawana amani mbona waLibya wajisemei kwamba sisi hatuna amani unajisifia kua na Amani wakati Tanzania ni miongoni mwanchi ambazo wananchi wake hawana furaha
 

wiseboy

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,944
2,000
Nyie tutisheni sisi tu

Marikani akiwaamulia kina mambo Sasa na siro utakuta wanajinyambia barabarani peke yao

Yule wa mjengo mwingine anaweza akajishoot ili asiaibike km mkwawa ahaha

Trump kuja uku Kuna watu wamechoka kula kodi za watanganyika
Laana ya ukoloni inakumaliza vibaya! Penda nchi yako acha kuita ita hapa shetani kuu la mizimu huyo Trump wako.
Haipo na haitakuwepo siku hata mjukuu wako akanufaika na huyo unaemuona mungu mtu kwako (ze takataka trump)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom