"Ikitokea siku Marekani akanisifia,Lazima nitarudi nyuma na kuangalia nimekosea wapi?" Mwalimu Julius Nyerere.

red fox

Senior Member
Jan 5, 2017
127
342
Baada ya muda mrefu sasa marekani na vi baraka wake waingereza wametoa tamko kuwa Rais Magufuli ni dikteta mwingine wa Afrika.Katika mtazamo mpana zaidi,tafsiri ya kauli hii ni,"Magufuli ni mwamba mwingine wa Afrika." mwaka 2016 wakati uingereza wapo katika vuguvugu la kutaka kujitoa katika umoja wa ulaya yupo mwanadada mwanaharakati ambaye alisimama kidete kutetea uingereza asitoke katika umoja huo wa ulaya.Unajua kilicho tokea? yule mwana Dada aliuawa katika mazingira ya kutatanisha na hakukuwa na taifa lolote kutoka ama Afrika ama Asia ama marekan ambao walilaani au kumshutum David Cameroon kuwa ni diktet au hata kuitangazia dunia kuwa uingereza si mahala salama pakwenda.Mwaka 2011 Uingereza na Marekani kupitia Jeshi la NATO walifanya uvamizi katika taifa huru(sovereign state) Libya wakavuruga amani ya Libya wakamuua kiongozi ambaye alichaguliwa na wanalibya.Hakuwahi kutokea mataifa ama ya Asia ama ulaya kulaani tukio lile ambalo lilienda kuvuruga hali ya amani na uchumi w Libya.

Marekani katika kipindi cha mwaka 2013-2014 kulitokea matukio kadhaa ya ukiukwaji wa haki za binadamu,polisi waliuwa kwa kukusudia vijana wenye asili ya kiafrika tena mpaka maandamano yalifanyika lakini hakuna aliyejitokeza ama Afrika ama ulaya kulaan matukio hayo.

Pamoja nakwamba kuna taasisi kubwa duniani inayoungnisha mataifa yoote na kuhughulia kero zao pale zinapo jitokeza,Somalia mpaka sasa si Marekani,si Uingereza ambaye alishawahi kujitolea kwenda kuweka usalama katika mataifa hayo,zaidi kila siku viongozi Wao hutoa kauli za kudhalilisha viongozi wa Afrika na watu wake.Sudan kabla ya kutengana mwaka 2011 nakuwa mataifa 2 Sudan kusini na kaskazini na hata kupelekea machafuko Sudan kusini,si marekani wala si Uingireza ambaye alishawahi hata kukanyaga tu katika ardhi ya mataifa hayo na kutafuta masuluhisho.

Sikuzote Marekan na Uingereza watalaumu na kuingilia Uhuru wa taifa Fulani endapo katika taifa hilo kuna(dhahabu,gesi,mafuta,diamond na rasilimali nyingine kama hizo) na huwa wakali zaidi endapo akitokea kiongozi jasiri na mwenye msimamo wa kuzilinda na kuzitetea raailimali hizo zisitumike kwa maslah ya Wao.

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani,kumeshafumuliwa mikataba ya madini na sasahv kuna 50-50 yaani kati ya taifa na wawekezaji kuna mgawanyo sawa wa faida,kwanini wasiseme Rais dikteta?? miaka yoote wamejichukulia bure leo wanaacha faida kwann wasiseme Rais dikteta?? Uingereza ametawala Tanganyika tangu baa ya vita kuu ya pili ya dunia lakn aliacha mainjinia wasomi 2,aliacha taifa watuwake 98% hawajui kusoma na kuandika.Aliacha taifa huduma za maji upatikanajiwake ni asilimia 0.005%,aliacha taifa ambalo matumizi ya nishati ni 0.01%, aliacha taifa kuna reli ambayo zilijengwa kutoka maeneo wanakozalisha malighafi na kupeleka mjini basi tena reli hizo hazikuweza kutuunganisha hata na Rwanda na Burundi ambao wakati wa ujeruman walikuwa sehem ya Tanganyika.Uingereza wanaondok Tanganyika walisha waua watu wenye ujuzi kichwani na wengine wakakatwa viganja vya mikono(ukatili huu hawajawahi kusema) Uingereza wanaondoka,Km za lbarabara nchi nzima ilikuwa 1000Km. katika nchi yenye ukubwa wa 947,303KM.Katika nchi ya watu ambao hawa kuzidi hata 20000 walishindwa hata kujenga zahanati kila sehem,pamoja na kuwa tuna 6% ya maji yanayopatikana ndani ya nchi,walishindwa hata kujenga visima vya maji kwa watanganyika.Pamoja na kwamba walikaa tangu mwaka 1919 mpaka 1961 Lakin hawakujenga hata chuo kikuu kimoja zaidi waliacha taasisi ya ustawi wa jamii tu,na ilikuwa ni kwamaslahi yao binafsi.

Leo hii ambapo wanamwita Rais Magufuli dikteta,Tanzania nzima imeunganishwa na barabara, 60% ya watanzania wanatumia nishati ya umeme,ukiachana na mareli yao,tunajenga reli zetu tena ni standard kwa maana sio tu kuwa ni treni za umeme,lakn kwa Afrika ndio teen pekee zitakazokuwa zinaenda kwa kasi ya uhakika.Leo hii,achana na kila kata kuwa na zahanati masuala ya watu kulala chini katika mahospital zetu inaenda kuwa historia,sasahivi Tanzania ya miaka 50 tu ya Uhuru wake tunazungumzia uchumi wa viwanda,wasichojua watu wengi katika mataifa Mengi ya ulaya na Marekani,miaka yao ya mwanzo ya Uhuru(50) Ukiangalia utaona yalikuwa ni mataifa ya hovyo,yalikuwa kama dust bin....

Leo,tunazungumza Tanzania inayojenga mahusiano mazuri ya kiuchumi na mataifa ya ukanda huu kwa kujenga reli itakayotoka Tanzania mpaka Rwanda.Kwanini wasiseme Rais Magufuli dikteta?? jambo ambalo Wao katika miaka yao 50 ya kwanza walishindwa halafu wanaona taifa ambalo linaviongozi wa awamu 4 tu wamefanikiwa kufanya mambo ambayo Wao walifanya kwa miaka 100!!

Kinachotushangaza nipale wapinzani wa Tanzania wanaposhangia haya mambo na kuzania ukienda Marekani maisha ni kama peponi.Ivi tujiulize bila unafiki,unazani kwa aina ya siasa wanazofanya upinzani wa hapa kwetu wangekuwa ndo wapo marekan au huko uingereza wangekuwa wapi???

Kosa kubwa tunalotaka kufanya sisi ambao tunashuhudia haya ni kuruhusu Uhuru wetu wa kimaamuzi kuingiliwa na mataifa ya nje.Wakati wa awamu ya nne walitaka gesi,waka leta chokochoko za udini na kuua viongozi wakafeli.

Namalizia,wakati mwalm Nyerere anawaaga rasm umoja wa mataifa kabla ya kung'atuka aliwaambia"my last speech to the general assembly,I have described events and trends and needs as we are Tanzanians perceive them,to be silent when we see danger,to refrain from attaching policies which we see as contrary to the peace and justice to do this things will be to surrender our freedom and our dignity that we shall never do"

MAGUFULI TUBEBE TUNAIMANI NAWE!!!!
By Dr. John Mahimbo
 
Nyie tutisheni sisi tu

Marikani akiwaamulia kina mambo Sasa na siro utakuta wanajinyambia barabarani peke yao

Yule wa mjengo mwingine anaweza akajishoot ili asiaibike km mkwawa ahaha

Trump kuja uku Kuna watu wamechoka kula kodi za watanganyika
 
Baada ya muda mrefu sasa marekani na vi baraka wake waingereza wametoa tamko kuwa Rais Magufuli ni dikteta mwingine wa Afrika.Katika mtazamo mpana zaidi,tafsiri ya kauli hii ni,"Magufuli ni mwamba mwingine wa Afrika." mwaka 2016 wakati uingereza wapo katika vuguvugu la kutaka kujitoa katika umoja wa ulaya yupo mwanadada mwanaharakati ambaye alisimama kidete kutetea uingereza asitoke katika umoja huo wa ulaya.Unajua kilicho tokea? yule mwana Dada aliuawa katika mazingira ya kutatanisha na hakukuwa na taifa lolote kutoka ama Afrika ama Asia ama marekan ambao walilaani au kumshutum David Cameroon kuwa ni diktet au hata kuitangazia dunia kuwa uingereza si mahala salama pakwenda.

DAVID CAMERON alikuwa upande wa huyo DADA aliyeuawa, kwa sababu hakutaka nchi yake ijitoe MUUNGANO WA ULAYA.
Ndio maana hoja yake ilivyopingwa kwa kura za wananchi ikiamua wajiondoe kwenye umoja huo alijiuzulu UWAZIRI MKUU wa UINGEREZA.
 
[QUOTE="red Mwaka 2011 Uingereza na Marekani kupitia Jeshi la NATO walifanya uvamizi katika taifa huru(sovereign state) Libya wakavuruga amani ya Libya wakamuua kiongozi ambaye alichaguliwa na wanalibya.Hakuwahi kutokea mataifa ama ya Asia ama ulaya kulaani tukio lile ambalo lilienda kuvuruga hali ya amani na uchumi w Libya[/QUOTE]

Yanayoendelea LIBYA yanasikitisha sana, lakini hii yote ni kwa sababu ya viongozi hasa wa nchi zetu za kiafrika kujigeuza mungu watu. haiwezekani utawale wenzako miaka nenda miaka rudi kwa madai wewe ndio pekee mwenye akili na uzalendo.
Nashukuru Zimbabwe hatimaye wamemalizana na Mugabe.

Haki na Usawa ndio Msingi Imara wa AMANI na mshikamano katika taifa lolote liwe.
Hakuna anayepinga maendeleo, WANAPINGA HAYO MENGINE AMBAYO HAUJATAJA na KAMA umetaja ni katika kuweka ulinganisho KUHALALISHA mauaji kama casualties ya kupata MAENDELEO
 
Baada ya muda mrefu sasa marekani na vi baraka wake waingereza wametoa tamko kuwa Rais Magufuli ni dikteta mwingine wa Afrika.Katika mtazamo mpana zaidi,tafsiri ya kauli hii ni,"Magufuli ni mwamba mwingine wa Afrika." mwaka 2016 wakati uingereza wapo katika vuguvugu la kutaka kujitoa katika umoja wa ulaya yupo mwanadada mwanaharakati ambaye alisimama kidete kutetea uingereza asitoke katika umoja huo wa ulaya.Unajua kilicho tokea? yule mwana Dada aliuawa katika mazingira ya kutatanisha na hakukuwa na taifa lolote kutoka ama Afrika ama Asia ama marekan ambao walilaani au kumshutum David Cameroon kuwa ni diktet au hata kuitangazia dunia kuwa uingereza si mahala salama pakwenda.Mwaka 2011 Uingereza na Marekani kupitia Jeshi la NATO walifanya uvamizi katika taifa huru(sovereign state) Libya wakavuruga amani ya Libya wakamuua kiongozi ambaye alichaguliwa na wanalibya.Hakuwahi kutokea mataifa ama ya Asia ama ulaya kulaani tukio lile ambalo lilienda kuvuruga hali ya amani na uchumi w Libya.

Marekani katika kipindi cha mwaka 2013-2014 kulitokea matukio kadhaa ya ukiukwaji wa haki za binadamu,polisi waliuwa kwa kukusudia vijana wenye asili ya kiafrika tena mpaka maandamano yalifanyika lakini hakuna aliyejitokeza ama Afrika ama ulaya kulaan matukio hayo.

Pamoja nakwamba kuna taasisi kubwa duniani inayoungnisha mataifa yoote na kuhughulia kero zao pale zinapo jitokeza,Somalia mpaka sasa si Marekani,si Uingereza ambaye alishawahi kujitolea kwenda kuweka usalama katika mataifa hayo,zaidi kila siku viongozi Wao hutoa kauli za kudhalilisha viongozi wa Afrika na watu wake.Sudan kabla ya kutengana mwaka 2011 nakuwa mataifa 2 Sudan kusini na kaskazini na hata kupelekea machafuko Sudan kusini,si marekani wala si Uingireza ambaye alishawahi hata kukanyaga tu katika ardhi ya mataifa hayo na kutafuta masuluhisho.

Sikuzote Marekan na Uingereza watalaumu na kuingilia Uhuru wa taifa Fulani endapo katika taifa hilo kuna(dhahabu,gesi,mafuta,diamond na rasilimali nyingine kama hizo) na huwa wakali zaidi endapo akitokea kiongozi jasiri na mwenye msimamo wa kuzilinda na kuzitetea raailimali hizo zisitumike kwa maslah ya Wao.

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani,kumeshafumuliwa mikataba ya madini na sasahv kuna 50-50 yaani kati ya taifa na wawekezaji kuna mgawanyo sawa wa faida,kwanini wasiseme Rais dikteta?? miaka yoote wamejichukulia bure leo wanaacha faida kwann wasiseme Rais dikteta?? Uingereza ametawala Tanganyika tangu baa ya vita kuu ya pili ya dunia lakn aliacha mainjinia wasomi 2,aliacha taifa watuwake 98% hawajui kusoma na kuandika.Aliacha taifa huduma za maji upatikanajiwake ni asilimia 0.005%,aliacha taifa ambalo matumizi ya nishati ni 0.01%, aliacha taifa kuna reli ambayo zilijengwa kutoka maeneo wanakozalisha malighafi na kupeleka mjini basi tena reli hizo hazikuweza kutuunganisha hata na Rwanda na Burundi ambao wakati wa ujeruman walikuwa sehem ya Tanganyika.Uingereza wanaondok Tanganyika walisha waua watu wenye ujuzi kichwani na wengine wakakatwa viganja vya mikono(ukatili huu hawajawahi kusema) Uingereza wanaondoka,Km za lbarabara nchi nzima ilikuwa 1000Km. katika nchi yenye ukubwa wa 947,303KM.Katika nchi ya watu ambao hawa kuzidi hata 20000 walishindwa hata kujenga zahanati kila sehem,pamoja na kuwa tuna 6% ya maji yanayopatikana ndani ya nchi,walishindwa hata kujenga visima vya maji kwa watanganyika.Pamoja na kwamba walikaa tangu mwaka 1919 mpaka 1961 Lakin hawakujenga hata chuo kikuu kimoja zaidi waliacha taasisi ya ustawi wa jamii tu,na ilikuwa ni kwamaslahi yao binafsi.

Leo hii ambapo wanamwita Rais Magufuli dikteta,Tanzania nzima imeunganishwa na barabara, 60% ya watanzania wanatumia nishati ya umeme,ukiachana na mareli yao,tunajenga reli zetu tena ni standard kwa maana sio tu kuwa ni treni za umeme,lakn kwa Afrika ndio teen pekee zitakazokuwa zinaenda kwa kasi ya uhakika.Leo hii,achana na kila kata kuwa na zahanati masuala ya watu kulala chini katika mahospital zetu inaenda kuwa historia,sasahivi Tanzania ya miaka 50 tu ya Uhuru wake tunazungumzia uchumi wa viwanda,wasichojua watu wengi katika mataifa Mengi ya ulaya na Marekani,miaka yao ya mwanzo ya Uhuru(50) Ukiangalia utaona yalikuwa ni mataifa ya hovyo,yalikuwa kama dust bin....

Leo,tunazungumza Tanzania inayojenga mahusiano mazuri ya kiuchumi na mataifa ya ukanda huu kwa kujenga reli itakayotoka Tanzania mpaka Rwanda.Kwanini wasiseme Rais Magufuli dikteta?? jambo ambalo Wao katika miaka yao 50 ya kwanza walishindwa halafu wanaona taifa ambalo linaviongozi wa awamu 4 tu wamefanikiwa kufanya mambo ambayo Wao walifanya kwa miaka 100!!

Kinachotushangaza nipale wapinzani wa Tanzania wanaposhangia haya mambo na kuzania ukienda Marekani maisha ni kama peponi.Ivi tujiulize bila unafiki,unazani kwa aina ya siasa wanazofanya upinzani wa hapa kwetu wangekuwa ndo wapo marekan au huko uingereza wangekuwa wapi???

Kosa kubwa tunalotaka kufanya sisi ambao tunashuhudia haya ni kuruhusu Uhuru wetu wa kimaamuzi kuingiliwa na mataifa ya nje.Wakati wa awamu ya nne walitaka gesi,waka leta chokochoko za udini na kuua viongozi wakafeli.

Namalizia,wakati mwalm Nyerere anawaaga rasm umoja wa mataifa kabla ya kung'atuka aliwaambia"my last speech to the general assembly,I have described events and trends and needs as we are Tanzanians perceive them,to be silent when we see danger,to refrain from attaching policies which we see as contrary to the peace and justice to do this things will be to surrender our freedom and our dignity that we shall never do"

MAGUFULI TUBEBE TUNAIMANI NAWE!!!!
By Dr. John Mahimbo

Yaani mnajitahidi sana ila hamuwezi!

Huyu Dr nae anajitafutia uteuzi...Eti DR MAHIMBO,Sizonje akiona mahala DR au PROF basi uteuzi nje nje!

Jitahidini bana!
 
Huyo mwanaharakati aliye uwawa kutetea Uingereza isijitoe EU anaitwa nani ?

Unajua kilicho fanya Cameron ajiuzulu ni kipi ?

David na huyo aliyeuwawa wote walikuwa wanatetea UK kutojitoa EU
Sasa Cameron atamuuaje huyo dada ?
 
Namalizia,wakati mwalm Nyerere anawaaga rasm umoja wa mataifa kabla ya kung'atuka aliwaambia"my last speech to the general assembly,I have described events and trends and needs as we are Tanzanians perceive them,to be silent when we see danger,to refrain from attaching policies which we see as contrary to the peace and justice to do this things will be to surrender our freedom and our dignity that we shall never do"

MAGUFULI TUBEBE TUNAIMANI NAWE!!!!
By Dr. John Mahimbo

Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na madhaifu yake kama mwanadamu, na hakika tutamheshimu milele kwa sababu ya matendo na ushauri wake APUMZIKE KWA AMANI

"dhambi ya ubaguzi ni sawa sawa na kula nyama ya mtu"
Mwl. Nyerere

'Mtu mwenye akili akikuambia neno la kipumbavu -ukalikubali, anakudharau!' 01/5/1995
Mwl. Nyerere

"Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika” –MwalimuNyerere (Januari, 1966)
 
tungepata vjana 100 kama ww taifa tungekuwa san big up;,,mfano mzuri kwa kijana makonda ajawaitokea
 
Nionavyo katika nchi tofauti,nimegundua CHINA na URUSI wana aina yao ya demokrasia ambayo,imewasaidia kupiga hatua kimaendeleo (ndio nchi zenye uhuru wa kweli).Ila sisi waafrika hatuna aina yetu demokrasia ,sisi tumekopi kutoka kwa mataifa ya magharibi na kupesti na wao ndio wanaicontrol hii demokrasia kwa kumuweka wamtakaye na ukienda kinyume utaundiwa mizengwe mpaka utoke ww mwenyewe.Wanajifanya kuguswa na matukio ktk nchi yetu,ila najiuliza mbona YEMEN wameisusa sijasikia tamko la Mmarekani au taifa lolote kutoka Ulaya,Saudi Arabia anainyuka YEMEN atakavyo Mmarekani kakaa kimya kisa anafaidika na mafuta yao.Matokeo yake YEMEN ina hali mbaya wananchi wake wanakufa kwa mabomu, njaa na kipindupindu na ndio maana ninawaona hawa nchi za magharibi wakilalamikia haki za binadamu,najiuliza hivi hawakioni Saudi Arabia anachomfanyia YEMEN,ndio hapo ukikaa ukitafakari unagundua ni UNAFIKI.
 
Kwani watu huwezi kuwapa maendeleo mpaka uwauwe,uwafunge na kuwatia ulemavu? Lakini pia ww unaweza kuwa mkamilifu mpaka usikosolewe umekuwa mungu? Hakuna mtu anaemsikiliza Marekani wala Wingereza ss tunaongelea tunacho kiona kwakuwa kinatugusa.Ww ndugu yako angepigwa risasi ungefurahi? au kufungwa kwenye kiroba ukamkuta baharini ungejisikiaje ,ndugu yangu tumia akili kufikiri usitumie matako hakuna maendeleo kama hamna amani ya nafsi.Hayo maendeleo anamletea nani kama anafikiri kuuwa tu? Mungu anakosewa na binadam kila kukicha lakini anendelea kuturuzuku sembuse binadam anae kula na kunya na kusinzia.
 
Hata yaliyompata ni kwasababu Mungu alipenda yampate, ila tunaakili sisi tumepewa na Mungu, tunaweza kuona nini kinaenda kutokea mbeleni kutokana na matendo ya watawala...
Uko sahihi mkuu,kama akili yake ilivyomtuma kulianzisha ndivyo atakavyolimaliza!bila kusahau malecturer wake wanavyosubiri kumgawana kama nyama ya sadaka.
[QUOTE="red Mwaka 2011 Uingereza na Marekani kupitia Jeshi la NATO walifanya uvamizi katika taifa huru(sovereign state) Libya wakavuruga amani ya Libya wakamuua kiongozi ambaye alichaguliwa na wanalibya.Hakuwahi kutokea mataifa ama ya Asia ama ulaya kulaani tukio lile ambalo lilienda kuvuruga hali ya amani na uchumi w Libya

Yanayoendelea LIBYA yanasikitisha sana, lakini hii yote ni kwa sababu ya viongozi hasa wa nchi zetu za kiafrika kujigeuza mungu watu. haiwezekani utawale wenzako miaka nenda miaka rudi kwa madai wewe ndio pekee mwenye akili na uzalendo.
Nashukuru Zimbabwe hatimaye wamemalizana na Mugabe.

Haki na Usawa ndio Msingi Imara wa AMANI na mshikamano katika taifa lolote liwe.
Hakuna anayepinga maendeleo, WANAPINGA HAYO MENGINE AMBAYO HAUJATAJA na KAMA umetaja ni katika kuweka ulinganisho KUHALALISHA mauaji kama casualties ya kupata MAENDELEO[/QUOTE]
Tunachohitaji hapa mkuu,ni kupambanua mambo na kupambana na hali zetu,bila kudhani kuwa hao ngozi ya nguruwe watatubeba. Familia isiyo na migogoro/changamoto ni familia iliyokufa na haina utamaduni wake yenyewe wa kujivunia. Ni kweli tunamatatizo yetu,let's face it our own ways.
 
Back
Top Bottom