Ikitokea Rais wa nchi akagundulika sio raia wa nchi anayoongoza, nini kinaweza tokea?

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2016
3,590
8,475
Wakuu najaribu kujiuliza sana,hivi ikitokea mkuu wa nchi yeyote duniani akigundulika sio raia wa nchi husika nini kinaweza tokea?

Maana wapo maraisi wengine huko duniani hufurahi wanapoona walalahoi walio wachaguwa kwa ahadi kedekede wakiteseka sana ndani ya nchi yao.

Kuna maraisi wengine huwa wanataka raia wao waishi maisha ya shida karaha na kushibdia mlo mmoja,hakuna haja ya nchi hizo kufanya uchunguzi kugundua mkuu wa nchi hiyo duniani kama hana uzalendo na taifa lake(si RAIA) nini kinaweza tokea?.

Maana huwa nasikia nchi yeyote duniani huwa inakitengo maalumu kinachochaguwa raisi wa nchi(huthibitishwa na wananchi)je kitengo kikigundua kimemchagua raisi wa nchi nakashapewa madaraka lakini si raia nini kinaweza tokea?.

Ningeomba mada hii ichagiwe bila kutaja jina la kiongozi yeyote wa nchi yeyote duniani,maana mada nzima kuna neno ikitokea ikitokea ikitokea,sasa kwa bahati nzuri au mbaya haijawahi tokea.Ningeomba watu wa usalama na wanaofahamu issues hizi watupe somo nini kinaweza tokea.
 
Mtu huchaguliwa au kuondolewa kwenye Urais kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi husika. Moja kati ya matakwa ya sheria katika sifa za mgombea wa Urais ni kuwa raia wa nchi husika. Kwahiyo,itakapogundulika kuwa Rais aliyechaguliwa si raia wa nchi hiyo, kwanza anapoteza Urais wake kwakuwa anapotez sifa za kuwa hapo. Pia, mambo ya kihamiaji yatafuatia.
 
Mkuu mimi sio mwanasheria lakini nafahamu fika wewe nimwanasheria.Sasa kuna sheria ambayo hairuhusu kumshitaki raisi wa nchi mahakamani either akiwa madarakani or akiondoka sasa nichombo kipi kitajachotengua uraisi wa muhusika.Mfano tuchukulie mfano kwa nchi yetu Tz.
 
Mkuu mimi sio mwanasheria lakini nafahamu fika wewe nimwanasheria.Sasa kuna sheria ambayo hairuhusu kumshitaki raisi wa nchi mahakamani either akiwa madarakani or akiondoka sasa nichombo kipi kits macho ten cues uraisi wa muhusika.Mfano tuchukulie mfano kwa nchi yetu Tz.
Bunge laweza kumuondoa Rais madarakani kwa mujibu wa Katiba
 
Ni nchi gani duniani imewahi kuchagua Rais ambaye baadaye akajulikana si RAIA wa nchi hiyo?

Na imani Tume za Uchaguzi moja ya maeneo ambayo wako makini sana ni uthibitisho wa uraia wa mgombea.
 
Kwani Nchi ni nini? Mipaka au nini? Binafsi nikijiona najiona Mwafrika ninae fanana na Mwafrika yoyote wa Afrika.

Kila kitu kina usahihi kwa wakati wake, na wakati sahihi anaepanga ni Mungu tu. Shukuru kwa yote maana hujui nini kusudio kwa kilicho pangwa na Mpangiliaji wa kweli. Only God.
 
Mtu huchaguliwa au kuondolewa kwenye Urais kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi husika. Moja kati ya matakwa ya sheria katika sifa za mgombea wa Urais ni kuwa raia wa nchi husika. Kwahiyo,itakapogundulika kuwa Rais aliyechaguliwa si raia wa nchi hiyo, kwanza anapoteza Urais wake kwakuwa anapotez sifa za kuwa hapo. Pia, mambo ya kihamiaji yatafuatia.
Na pili anapelekwa mahakamani. Hatuwezi kumuwacha hivihivi
 
story za hivyo zipo nyingi tu...kuepuka kutaja majina ni ngumu ila kutaja waliopo madarakani ndio sio vizuri......story zinasema mikhail gorbachev ni mmarekani alipandikizwa USSR Urusi ya Zamani,story pia zinasema Yassir Arafat kiongozi wa PLO huko Palestine ni Mmisri alipandikizwa....ni dhahiri Mamlaka husika hugundua kabla mtu husika hajatoka madarakani lakini ninahisi zinatumika mbinu za kijasusi kumdhibiti mtu akigundulika si raia kuliko kumtoa kibabe itaonyesha udhaifu!!!

Hivyo basi nionavyo mimi mtu akigundulika sio raia mamlaka za usalama za taifa husika zitampiga pini mbaya asiharibu nchi husika
 
Ni nchi gani duniani imewahi kuchagua Rais ambaye baadaye akajulikana si RAIA wa nchi hiyo?

Na imani Tume za Uchaguzi moja ya maeneo ambayo wako makini sana ni uthibitisho wa uraia wa mgombea.
Zambia yasemekana Kaunda hakuwa Mzambia....

Kuna Nchi moja nayo raisi wake wa kwanza yesemekana alikuwa ni Tutsi amepigania uhuru wa Mataifa mengi Africa almaarufu sana kwa kuchonga Meno.. Pia Kuna Nchi moja hivi Africa raisi wake alikuwa kipande cha mtu yasemekana ni chinga kutoka Msumbiji...

Hitler Wa Ujerumani alikuwa ni Kutoka Austria
Obama - Yahudi,Kenyan
Karume Kenge - Malawi
Papa Fransis - Anaongoza nchi iitwayo Vatican huku yeye akiwa ni raia wa Argentina
Same Na Pope Benedict alikuwa raia wa Germany
Huyu wa sasa mtu akiniambia ni From Rwanda sikatai hata kidogo..

Nakumbuka Mtikila alishawahi kusema Tanzania haijawahi kuwa na Raisi Mtanzania
 
Kama kweli ulichokiandika ndicho uliçhofundishwa au kuambiwa au kusoma basi Watanzania bado tuna safari ndefu.

Halafu ulivyomuoga mengine unaandika kwa mafumbo,ukiwa mwoga utafahamu vipi vitu!?

Uliza maswali kwa uwazi ili upate majibu sahihi sio kwa mafumbo!!!
 
Mkuu mimi sio mwanasheria lakini nafahamu fika wewe nimwanasheria.Sasa kuna sheria ambayo hairuhusu kumshitaki raisi wa nchi mahakamani either akiwa madarakani or akiondoka sasa nichombo kipi kits macho ten cues uraisi wa muhusika.Mfano tuchukulie mfano kwa nchi yetu Tz.
Ni mweli sheria inamkinga rais dhidi ya mashitaka akiwa madarakani, lakini huo urais Ni lazima uwe hali, sasa kwa sababu za kiusalama Ili mtu aweze kuwa rais Ni lazima awe Na uraia, tena siyo uraia Tu, Bali Ni uraia wa kuzaliwa wa nchi husika.

hivyo atakuwa Na urais batili, Na ufahamu ya kwamba hata hapa Tz siyo kwamba ukishakuwa rais hauwezi ondolewa hata Kama wewe Ni raia, rais anaweza kuvuliwa madaraka yake wakati wowote Kama Kuna ulazima huo.

Bunge Lina mamlaka ya kumvua urais yoyote awaye madarakani.

Nothing in law is absolute
 
bunge gani!kama la huku kwetu linaweza kumuondoa rais?
 
Back
Top Bottom