Ikitokea mashehe au mapadri wanawapeleka na kuwakataza kuhoji juu ya serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikitokea mashehe au mapadri wanawapeleka na kuwakataza kuhoji juu ya serikali

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Godwine, Mar 13, 2011.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Katika dunia ya sasa ambapo idadi kubwa ya wahumini wa dini zote ni waelewa je inawezekanaje watu hao kushawishiwa na kufanyiwa maamuzi ya kisiasa na wakuu wao wa dini? wanawezaje kuambiwa mchague nani? au kuwepo kwenye dini ni kupoteza uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi?
   
 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  ???????!!!!!!!!!
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  ukiwa thinker ni pamoja na kujua mwandishi anadhani kuhusu nini na sentesi ikiwa na makosa kuielewa.....kwa ujumla ni kujilazimisha kutumia kiswahili kwani mimi ni fundi sana wa kifaransa na kireno sasa si vema kuacha tamaduni zetu
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Hapa sio mahali pa waliokimbia umande bob!!! Bora uandike hicho kireno au kifaransa... kuliko kiswahili crap namna hii
   
 5. G

  Godwine JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kiswahili si kipimo cha kukimbia umande kwani ni lugha unaweza ukasoma kwa kireno mpaka ukamaliza chuo lakini si kwamba wewe umekimbia umande........naona umepoteza dira mjumbe au umefungiwa katika sehemu moja na kudhani kiswahili kinatumika dunia nzima
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Ona sasa baada ya kukuzodoa umeandika kiswahili fasaha na kinachoeleweka! Hongera sana kwa kujirekebisha!
   
 7. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,775
  Likes Received: 6,108
  Trophy Points: 280
  Inategemea na mtu (mdini) mwenyewe jinsi alivyouza uhuru wake kwa viongozi wake kiasi kwamba viongozi wake wa dini wanafikiri na hata kuamua kwa niaba yake na yeye mhusika akibaki kuburuzwa tu. Tena utashangaa hata wasomi wazuri tu bado kifikra ni watu kuburuzwa. Ndugu yangu dunia ya leo unatakiwa kuhoji na kuwa na fikra huru na sio kuuza utu wako kwa viongozi wako wa dini, kisiasa, n.k.

  Kwa mfano, usishangae watu na "akili" zao akasimama kiongozi wa dini yao na akahubiri kwamba hakuna binadamu mwingine anayestahili kuishi katika eneo fulani la Tanzania isipokuwa watu wa dini yao na kwamba wengine wote wanastahili kuuwawa; usishangae kesho maandamano yakafanywa na "waumini" wake kumuunga mkono. Vivyo hivyo hata kwa baadhi ya asasi vikiwemo vyama vya siasa; watu (waumini) hawajisumbui kufikirisha akili zao na kuhoji uhalali wa kauli za viongozi wao! Wanaburuzwa tu kama mazuzu.

  Tumezaliwa huru na hivyo tunapaswa kuwa na fikra na maamuzi huru alimradi hatuvunji taratibu na sheria za nchi. Usidhani kila anayejiita kiongozi wa dini ni kiongozi kweli; wengine wanawatumikia mabwana zao badala ya Mwenyezi Mungu.
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kweli wengine wantumikia mabwana zao badala ya mwenyezi Mungu! Kwa mfano una kuta kiongozi wa dini anawaambia waumini wa chini yake kwamba fulani ambaye anaonekana fisadi ni chaguo la Mungu/ Khalifa! Hii ni hatari sana. Hata hivyo wanafanikiwa kwa kiwango kikubwa kwani waumini wengi hupenda kumeza wanayoambiwa bila tafakuri jadidi au kutafuta maarifa zaidi!
   
 9. G

  Godwine JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  najua wewe ni juzijuzi tu umetoka kujifunza fasihi .......ukikuwa kwenye fani utanyamaza..........kaza buti
   
Loading...