Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,440
113,448
Wana MMU,

Salaam.

Sisi binaadamu kila mtu ana kitu chake apendacho ndani ya moyo wake, na kila akikiona hicho apendacho, anakuwa roho kwatu!.

Nina swali, inapotokea wewe unapenda macho, halafu kukatokea kuna kiongozi fulani mwanamke ana jicho hilo!, wewe unapenda jicho, ukimuona huyo mwenye jicho, unafurahi na huchoki kumwangalia.

Je, kuna ubaya ukimsifia kiongozi huyo au itaonekana huo ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu, heshima na ustaarabu?.

Kama kiongozi fulani amejaaliwa kitu fulani, mfano Jokete ni mrembo, jee kuna ubaya wowote kumsifia Jokate ni mrembo?.

Nimeuliza hili swali kufuatia kuangalia ITV matangazo ya moja kwa moja, mubashara, ya Tuzo za I Can, zinazotolewa na Reginald Mengi kupitia Taasisi yake ya Reginald Mengi Foundation, inayowasaidia watu wenye ulemavu, mgeni rasmi ni kiongozi fulani mwanamke, ana jicho hilo!.

Paskali.
 
Duuhh kwa uzi huu , mkuu Mayalla ni bora ulizaliwa zaman saiz una mke na watoto.

BILA HIVO izi ligi za ujana kwasasa usingeziweza kabisa , na watoto wakali wakali km Jokate, Usingethbutu hata kumshika mkono maana ni kiongozi alafu ni mkaliiii kinyama.

Watoto hawa wanapenda sisi masela, ambao tunajiamin kiasi kwamba hata mbele za vyombo vya habar bado unaweza mwambie "Mkuu wangu umependeza sana nahayo macho yako mimi najikuta ulimi unakua mzito"

Utamuona anacheka cheka kwa aibu alafu anakujibu " hahah Pascal bwanaaaa ,aya nashukuru sana".

Umenikumbusha Mzungu mmoja m'mama alinifundishaga Pathology , sasa huyu mama kila nlipokutana naye namsifia kinyamaa, aiseeee kuna likizo yupo Kwao Ujeruman alivorudi kanilitea Bongee la zawadi .

NASIKITIKA KUKUAMBIA WATOTO WAKALI WAKALI WOTE UNGEWAITA SHEMEJI
 
Umenikumbusha Mzungu mmoja m'mama alinifundishaga Pathology ,
Du!...Mkuu Carlos The Jackal (aka Vladimirovich Putin), umetisha, kumbe umepiga Pathology?. Toka nimejiunga JF, leo ndio nimekutana na mtu wa Pathology, zamani enzi za Nyerere, tulikuwa na ma pathologist wawili tuu, mmoja ni Dr. Shaba alikuwa Muhimbili na mwingine ni Dr. Mkulila alikuwa Bugando. Inasemekana kwenye medical school ya enzi hizo, kabla ya mambo ya neurosurgery, pathology ndio lilikuwa somo gumu sana, jee ni kweli?, Au ugumu wa pathology, ni uoga tuu wa kucheza na zile cadavers?.

Au pathology yako ni somo tuu kwenye mtaala wa MD na sio kusoma pathology ili uwe pathologist?.
P
 
Du!...Mkuu Vladimirovich Putin, umetisha, kumbe umepiga Pathology?. Toka nimejiunga JF, leo ndio nimekutana na mtu wa Pathology, zamani enzi za Nyerere, tulikuwa na ma pathologist wawili tuu, mmoja ni Dr. Shaba alikuwa Muhimbili na mwingine ni Dr. Mkulila alikuwa Bugando. Inasemekana kwenye medical school ya enzi hizo, kabla ya mambo ya neurosurgery, pathology ndio lilikuwa somo gumu sana, jee ni kweli?, Au ugumu wa pathology, ni uoga tuu wa kucheza na zile cadavers?.

Au pathology yako ni somo tuu kwenye mtaala wa MD na sio kusoma pathology ili uwe pathologist?.
P
 
Back
Top Bottom