Ikitokea alietuumba hakuagiza tufanyayo, Wengi itakula kwetu.

dalalitz

JF-Expert Member
Sep 6, 2013
3,418
1,980
Habari Waungwana.
Tuvumiliane iwapo maudhui ya Uzi huu yatakwaruza Mtu kwa namna yoyote.
Naheshimu na ninatambua subira itupasayo kumpa kila mmoja wetu kuamini na kuabudu chochote apendavyo.

Wakati ambapo Imani zimekuwa nyingi na kila mmoja ikiamini uwepo wa Muumba (mmoja) ambaye ndie chanzo cha uwepo wa Dunia na Vilivyomo pia. Hata hivyo, Imani zipo nyingi na tofauti ingawa kwa ujumla wake yapo mafundisho ambayo kwa kiasi kikubwa yanarandana juu ya Nini tufanyiane, Tule kipi, Tuepuke kipi, Tunywe nini nk.

Najaribu kujiuliza, Itokee imefika siku moja Wanadamu woooote tumekusanywa mbele ya Aliyetuumba Sisi kisha, akakanusha kwa herufi kubwa:
Mfano, ''Yoooote mliyojizuia nayo mimi sikuyaagiza''.

Fikiria zile burudani zoote, Yaani Totooz bin Michepukoooz, Vidumuuz, Biere kwa Watumiaji, Na nyingine nyingi ambazo tumekuwa tukijizuia nazo kufuata maelekezo ya Imani zetu. -Yote iwe haikuwa lazima? Ikitokea hii itakula kwetu wengi aisee.
 
tutamuuliza
"MBONA HUKUJITOKEZA KUTUSAHIHISHA!?"
Na hapo itakua imekula kwake!..
 
Uwepo wa Ibilisi a.k.a Shetani ndio changamoto, tangu mwanzo hakutaka/hataki tujue ukweli kuhusu maagizo ya Mungu! Mambo mengi tunayoaminishwa ni hila za Ibilisi ambae kwetu tunaoamini Ukristo ana wafuasi wengi nahisi ni zaidi ya 90% (rejea mlango wa mbinguni ni mwembamba lakini mlango wa kuzimu ni mpana sana)! Kama wafuasi wa ibilisi ni wengi inamanisha mafundisho mengi na makatazo mengi yana uibilisi! Tena siku hizi upotoshaji umeongezeka sana! Ni vizuri tukasoma wenyewe Maandiko "Matakatifu" na kuutumia ubongo wetu kisawasawa ili kuepuka matapeli wa kidini!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom