Ikitokea umepata dharura ya ghafla inaitajika milion moja kwa contact zako za simu utapigia watu wangapi.??

Haya mambo yanategemea na wewe uko vipi kifedha pia, maana kuna maswali unaweza kujiuliza:
  1. Ikitokea kuna Rafiki yako kwenye hizo contacts akahitaji milioni 1, utampa? I mean, huwa kuna wakati unakuwa na balance ya 1m+, na unaweza kumpa rafiki kama hivyo?
  2. Baada ya hapo jiulize, ni wangapi kwenye contacts zako unaweza kuwapa bila kuwaza mara mbili uwezo wao na utashi wa kurudisha?
Point ni kwamba it begins with you, jinsi unavyodhaminika, kipato chako, na watu hao ambao uko associated nao.
Maana kuna wakati unaweza kuwa nao, ukapoteza kazi au biashara zikaenda tofauti hizo contacts zako zikayeyuka pasikojulikana.

Tupambane wakuu, assurance kubwa ni kutoa kwenye akiba yako. Au uwe na Fixed account, kiasi kwamba unaweza kuitumia kama dhamana kwa dharura.
 
Leo mchana kwenye safari zangu hapa mjini nilifika sehumu kilukua kuna kitu nataka kununua price ilikua 1.8m balance yangu ya ilikua laki 9 na 86 nikaona isiwe tabu nikaanza kuangalia majina ya nani wa anaweza kunikopesha 1m ya haraka

nilipiga sim 7 na baada ya kama 20-25 nikapokea mkopo huyu ni rafiki yangu tunapiga kazi pamoja

sasa ukiachana na mchango labda huyu laki 2 yule laki tatu utapiga sim ngapi kupata milion moja kwenye majina yaliyopo kwenye sim yako????
My banker.
 
Haya mambo yanategemea na wewe uko vipi kifedha pia, maana kuna maswali unaweza kujiuliza:
  1. Ikitokea kuna Rafiki yako kwenye hizo contacts akahitaji milioni 1, utampa? I mean, huwa kuna wakati unakuwa na balance ya 1m+, na unaweza kumpa rafiki kama hivyo?
  2. Baada ya hapo jiulize, ni wangapi kwenye contacts zako unaweza kuwapa bila kuwaza mara mbili uwezo wao na utashi wa kurudisha?
Point ni kwamba it begins with you, jinsi unavyodhaminika, kipato chako, na watu hao ambao uko associated nao.
Maana kuna wakati unaweza kuwa nao, ukapoteza kazi au biashara zikaenda tofauti hizo contacts zako zikayeyuka pasikojulikana.

Tupambane wakuu.
Nimekuelewa vzr mno, nadhani huwa inakuaga hivi
 
Bibi yangu, mungu ampe uhai mrefu, she's 75yrs lakin ukiwa na shida wa kukupa yeye, anakamsemo kake "Mimi mkubwa na Nina familia kubwa natakiwa niwe na akiba ili mkipata tatizo msiadhirike"

Kimbembe uzidishe ule muda uliomuahidi kurudisha na usirudishe utaona dunia chungu na wakati wakulipa lipa bank mpelekee pay slip, la sivyo ukajisahau ukampa mkononi anasema hii ya kula Deni langu Bado

Allah ampe uhai mrefu bibi yangu
Huyo bibi nimempenda yaani anakupa pesa huku akijua ni lazma urudishe na ukijichanganya unalipa mara mbili ..
 
Watanzania twatakiwa kuwa na akiba. Dharura bana saa zingine unaishia dharirika na kuaibika.

Mi siku zote nahimiza watu wawe na Bima ya Afya na Wawe na hela Cash na Mobile, Bank at all times maana lolote laweza jitokeza
 
Kwenye sim yangu kuna majina 30 mmoja tu ndiyo nauhakika wa kupata hela ya fasta ila sema sasa hadi nije niipate jasho lazma linitoke, maana ataniambia nimtumie kwanza hela niliyo nayo, kama kitu cha shilingi milion 2 na mfukoni na laki 8 ataniambia nimtumie hii laki nane/ au nimpe hii laki 8 cash anipe hiyo milion 2....

Ila sasa hivi watu wakavu balaa, kupata mkopo ni kwa mbinde saana.....
 
Bibi yangu, mungu ampe uhai mrefu, she's 75yrs lakin ukiwa na shida wa kukupa yeye, anakamsemo kake "Mimi mkubwa na Nina familia kubwa natakiwa niwe na akiba ili mkipata tatizo msiadhirike"

Kimbembe uzidishe ule muda uliomuahidi kurudisha na usirudishe utaona dunia chungu na wakati wakulipa lipa bank mpelekee pay slip, la sivyo ukajisahau ukampa mkononi anasema hii ya kula Deni langu Bado

Allah ampe uhai mrefu bibi yangu
Huyo bibi utakuwa mchaga tu :D :D
 
Huyo bibi nimempenda yaani anakupa pesa huku akijua ni lazma urudishe na ukijichanganya unalipa mara mbili ..
Kabisa unalipa Mara mbili akikukopesha mnaenda wote bank anakupa na wakati wakurudisha lipa bank leta pay slip
Kuna mjomba wangu alikopa 700k ila alilipa 1m maana alinisahau akampa cash akasema hi ya kula hela yangu bado
 
Back
Top Bottom