Ikithibitika CHADEMA ilihusika na uvunjifu wa amani, then inapaswa kufutwa kwa mujibu wa katiba!

Hahaha Paskali na ikiwa ccm na serikali wamevunja katiba nao wafutwe?!

CHADEMA wanatafutwa kufutwa na kila chombo cha dola na hata ccm wanaounda serikali ndio mpango wao kuondoa ushindani dhidi yao. Kama wanataka haki waruhusu chombo cha nje kilicho huru kisicho na maslahi yoyote ndani ndicho kisimamie chaguzi zote na uendeshaji wa shughuli za siasa nchini.

Tofauti na hapo chadema hawawezi kupata fair trial kwa namna yoyote.
Hao ccm mwenyekiti wao ndiye rais na ana control vyombo vyote vinavyotumika kuikandamiza chadema, tume ya uchaguzi, msajili wa vyama vya siasa, polisi, mahakama.

Sasa chadema atahukumiwaje na mpinzani wake halafu utegemee apate fair trial?!
Huo ni uonevu kuihukumu chadema wakati serikali nzima haiwatendei haki.
We have laws in this country but no justice.
 
John Tendwa tena?!!!......... Kweli mapepo ya Kinondoni si ya mchezo mchezo!!
elimu,elimu,elimu mnapenda kukurupuka tu mbona mkuu Mayala ametolea ufafanuzi kabisa kua ili bandiko ni la mwaka 2013 wakati msajili alikuwa John Tendwa hayo maelezo katoa mwishoni kabisa,ungesoma mpaka mwisho ungeelewa,
 
Pascal Mayalla Kaka Paschal nimependa uzi wako...umeongea ukweli mtupu. Ni lini maonevu yataisha nchi hii? Polisi wanapiga wananchi bila huruma na kuwavunja mikono, miguu na sehemu za mwili. Kama ni kukiuka taratibu kwanini wasikamatwe? Wamepiga risasi ovyo, wameua na kujeruhi wananchi wasio na hatia, ni lini huu ubabe utaisha?

Toka huyu Magufuli ameingia madarakani kazi yake ni kuua tu na kujeruhi tu. Sijaona serikali dhalimu kama hii isiyojali utu wa binadamu, watu wanabaguliwa kutokana na maeneo wanayotoka na vyama vyao halafu huyu huyu Magufuli anasema maendeleo hayana vyama, Tunaona wakuu wake wa mikoa kama Mnyeti, Makonda na huyo Polepole wakiongelea ubaguzi waziwazi , sijui wana nia gani?....MAGUFULI NI MNAFIKI.

Viongozi wa Tanzania bado wana ile notion ya wakoloni kuwa ukiwa kiongozi unahitaji kuogopwa na kuheshimiwa kupita kiasi na unaweza ukamfanya chochote raia na usichukuliwe hatua, Hawajui dunia imeshabadilika....Viongozi wanapaswa kutumikia wananchi! Na sisi ndiyo waajiri wao....wasipotuheshimu tutawa-vote out. Aibu aibu kwa serikali hii iliyojaa wauaji, siku moja watajibu haya mashtaka huko the Hague.
 
Mshitakiwa no 1 Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mshtakiwa no 2 Kamanda wa Kanda Maalum Dar
Rais Magufuli anatakiwa kuwaondoa haraka sana hawa kwenye nafasi zao ili kupisha uchunguzi.
 
Kwa maoni yangu na mtazamo wangu watu wanaostahili kulaumiwa kwa mauaji ya Aquilina
1. MKURUGENZI
2. CHADEMA
3. POLISI
Mkurugenzi alichelewesha barua za mawakala ikawafanya CHADEMA waandamane, CHADEMA waliandamana pasipo kuwa na kibali cha kufanya hivyo, POLISI walitekeleza wajibu wao kwa kutumia risasi za moto(kosa) kwa watu wasiokuwa na silaha
 
Umesomaa alichoandika

Mwisho kamalizia hivi
Kwanza MBOWE na Chadema hawajavunja sharia, ila wamekiuka kanuni kuandamana bila kibali, ila yale hayakuwa maandamano ya kupangwa, imetokea dharura, hawakutendewa haki, hivyo wamekuwa provoked na kulazimika kuandamana, kufuatia kwa nini CCM tuu ndio wapewe barua za utambulisho na wao wanyimwe?. Provocation ni defense before the court of law, mtu akiwa provocked, anaweza kufanya lolote hadi kuua, na kuachiwa, depending on the nature ya hiyo provocation, na bila maandamano yale, barua za utambulisho zisinge toka, zimekuja kutoka saa 5 usiku!.

Kufuatia mazingira hayo, then, hakukuwa tena na muda wa kufuata taratibu kuomba kibali, bali walikuwa na wajibu wa kufanya maandamano ya Amani, bila fujo wala vurugu yoyote!.
Nisimnukuu Mayalla, nikunukuu wewe. Kwanza sipendi kuyaongelea yaliyotukia, yamezungukwa na mengi na mengi kati ya hayo hayajulikani. Siasa zetu nchini ni kama mchezo wa vichaa tu.

Ila ndugu, provocation ni defense against murder cases tu? Haihusiki na other criminal cases. Ktk makala ya Mayala, nimeamua kuchangia hilo.
 
CCM wakiruhusu mikutano ya siasa, upinzani uwe huru kufanya siasa pasipo polisiccm kuwagasi gasi ujue CCM itapotea kwa mda mchache sana.
Hivi Kwanini watu hawakwenda kupiga kura? Kwa Dar es salam, sidhani kama kuna eneo watu hawana elimu ya uraia, wanahitaji mikutano waelimishwe tena juu ya siasa ya vyama vingi, au kuna chama hakijulikani kule. Kwanini watu hawakwenda kupiga kura.
 
Uthibitisho wa kweli ni polisiccm ndiyo walipiga Risasi, lakini kwa sasa CCM na polisiccm wamebuni mbinu ya kutengeneza Sinema mpya wapate kumbambikia kesi chadema na mbowe. Hizo njama zinasukwa na Maliyamungu Bashite, le mutuz, Jerry, Lipumba na wenzao wengine.
Hivi kwanza Kwanini walishiriki uchaguzi ule na kugomea ule uliopita? Ulikuwa na yapi wa awali ambayo kwa huu yamerekebishwa? Intention yao ya kushiriki tangu awali ilikuwa ni kushinda au? Haya maswali yananisumbua sana.
 
Habari zenu mabibi na mabwana, nimejikuta nawaza kwa upole sana kwamba ktk kipindi hiki cha huzuni nchini, nilitegemea kuwaona watu kama akina Pascal Mayala, Mshana Jr, Mzee tupatupa wa Lumumba, Gentacymine na wengine weeengi ambao ni prominent peoples in JF wakitoa makala au writings zao juu ya hali ya siasa, kijamii na kiuchumi kwa sasa.
 
Habari zenu mabibi na mabwana,nimejikuta nawaza kwa upole sana kwamba ktk kipindi hiki cha huzuni nchini, nilitegemea kuwaona watu kama akina Pascal Mayala,Mshana Jr, Mzee tupatupa wa Lumumba,Gentacymine,na wengine weeengi ambao ni prominent peoples in JF wakitoa makala au writings zao juu ya hali ya siasa,kijamii na kiuchumi kwa sasa.
unawatakia nini
 
Hata hivyo nikadadisi zaidi, iwapo tuhuma za ugaidi zatathibitika kufanywa na chama tawala CCM, jee nacho, atakifuta bila huruma?!. Baada ya swali hilo, kwanza Msajili alisita kidogo na baadae kusema kuwa kama ni CCM, kwa vile hiki ni chama tawala, kikithibitika kufanya makosa ya ugaidi, au uvunjifu wa Amani, hatakifuta right away eti kwa sababu ni chama tawala!, kukifuta chama tawala ni kuvunja serikali iliyopo madarakani!, CCM kikifanya ugaidi, au uvunjifu wa Amani hata kivunja, bali atakipeleka mahakamani ili mahakama ndio itoe utaratibu wa nini cha kufanya endapo chama tawala kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa wakati kingali madarakani!.
Hapa inabidi tuibadili hii sheria bila kujali Chama gani kipo madarakani, hatuwezi jua miaka 20 ijayo CCM itakuwa wapi, Je ikiwepo CDM madarakani tutafanyaje wengine!?.
Hizi sheria zisipoangaliwa upya, siku moja hii nchi tutageuka Baghdad na Mosul!..
 
Back
Top Bottom