Ikishafika buchani, nyama hairudi kuwa ngómbe

Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
122
Mh!!!!!!!! nisameheni leo niandike kwa herufi za kupiga kelele

HIVI KWELI KATIKA VIWANGO VYOVYOTE VYA KIMAADILI, KUNA HAJA GANI YA KUWA NA MAZUNGUMZO NA EL- ADAWI AU KUFIKIRIA HATA KUTUMIA HIYO MITAMBO YA DOWANS?

HAIJALISHI TUKO KATIKA GIZA LA AINA GANI, THE END CAN'T JUSTIFY THE END KATIKA HILI!

SHAURI LIMESHAFIKA BUNGENI, LIMESHAFIKA MAHAKAMANI, TULISHA HUKUMIWA (VIBAYA), LIMESHAWAFIKIA WANANCHI NA WAMESHAPOKEA MACHUNGU YOTE YA KUANZIA UTAPELI WA WAMILIKI WA AWALI, JE TUNAWEZAJE KURUDISHA MMLIKI WA DOWANS (YEYOTE YULE) KUWA MFANYABIASHARA MWENZA MTARAJIWA MWENYE SIFA KUINGIA MKATABA NA SERIKALI YETU?

HATA KAMA ANGESEMA AMETUSAMEE DENI LOTE, NA ANATUPA HIYO MITAMBO BURE, KWA KIWANGO CHANGU CHA UADILIFU, NINGEKATAA NA BADO NINGETAFUTA KUWASHITAKI WAHUSIKA KWA HASARA NA ADHA AMBAYO WAMESHAISABABISHA KATIKA JAMII YETU!

NYAMA IMESHAFIKA BUCHANI!
 
Mkuu hakuna mazungumzo yeyote yanayofanyika hivi sasa. Kilichopo ni usanii mtupu unaolenga katika kuwafumba macho watanzania ili waunge mkono utekelezaji wa yale yaliyopangwa hapo awali.
 
Hivi mbona Watanzania na Akili zetu timamu tunageuzwa mbumbu? Mhesh.mmoja alisema Haijui Dowans na wala hana maslahi nayo.Halafu huyohuyo ndiye mwenye vyombo vya Usalama imekuwaje huyo El- A dawi apenyeze mipaka NA AJE NA GIA ati ya kutusamehe/kupunguza deni.Nani amemwalika kama siyo hao hao wanatuuma na kupuliza?Mboa mlimkatalia Kafulila(MB) asipeleke hoja bungeni mlijua siri ya ujio wa Mwarabu wa Dowans.Wadau nifumbueni.Mi na hasira.
 
Ujanja wa Rostam huo. Kamleta Mwarabu ili yeye aonekane kuwa sie mmiliki wa Dowans. Watanzania hatudanganyiki tena.
 
hapa kuna mawili! aidha serikali ya JK inatufanyia UHUNI au huyu jamaa ni muhuni na anafanya usanii wa darasa la kwanza!!!!!
 
Wakatae alafu......???Wanataka njia mpya ya kushinikiza malipo yatolewe!Kesho watasema ''Dowans sio adui yetu...deni amepunguza na pamoja na usubufu TULIOSABABISHA bado amekubali tutumie mitambo yake!!Sisi ndio tunaofaidika kwahiyo ni vyema na sharti kumlipa kutimiza wajibu wetu.''
Hapo kilichobaki ni nguvu ya umma kupaza sauti kwamba HATUKUBALI TENA KUFANYWA WAJINGA....zaidi ya hapo wataendelea na usanii wao mpaka watakapoimaliza Tanzania kabisa!
 
Jamaa kaja kuchukua chake mapema. Inanitia kichefuchefu jamaa linatoa statement za kejeli na kujivinjari Nchini. Wakati mkuu wa kaya anasema hamjui, na wafuasi wake wanapiga makofi! KWAKWELI TUNAJIDHALILISHA WENYEWE.
 
Hivi mbona Watanzania na Akili zetu timamu tunageuzwa mbumbu? Mhesh.mmoja alisema Haijui Dowans na wala hana maslahi nayo.Halafu huyohuyo ndiye mwenye vyombo vya Usalama imekuwaje huyo El- A dawi apenyeze mipaka NA AJE NA GIA ati ya kutusamehe/kupunguza deni.Nani amemwalika kama siyo hao hao wanatuuma na kupuliza?Mboa mlimkatalia Kafulila(MB) asipeleke hoja bungeni mlijua siri ya ujio wa Mwarabu wa Dowans.Wadau nifumbueni.Mi na hasira.

What is a way foward then?
 
Wakatae alafu......???Wanataka njia mpya ya kushinikiza malipo yatolewe!Kesho watasema ''Dowans sio adui yetu...deni amepunguza na pamoja na usubufu TULIOSABABISHA bado amekubali tutumie mitambo yake!!Sisi ndio tunaofaidika kwahiyo ni vyema na sharti kumlipa kutimiza wajibu wetu.''
Hapo kilichobaki ni nguvu ya umma kupaza sauti kwamba HATUKUBALI TENA KUFANYWA WAJINGA....zaidi ya hapo wataendelea na usanii wao mpaka watakapoimaliza Tanzania kabisa!

Naona sasa inabidi tupambane tu kwa vitendo maana Kikwete ameziba masikio kabisa na anatuletea usani tu
 
:mullet: kweli nimeamini mtoto wa panya ni panya haachi kuchimba mashimo,mwizi ni mwizi awe mfupi au mrefu mnene au mwembamba wote ni wezi tu! na kinyesi kiwe cha kabila lolote vyote ni vinyesi harufu yake ni mbaya kabisa!! natamani nisepe nchi jirani kulingana na harufu mbaya ya Tanzania open your mind nchi haina mwenyewe hii ati !! wote wezi wanaitafuna Tanzania kama mchwa tunabaki kama Yatima, amekuja huyo mhuni wa kariakoo anajifanya yeye ndiye mmilki wa Dowans amakweli duniani kuna maajabu any way hv kweli tuna viongozi??mpira gani unachezwa bila refa?is some thing paradox in my side!! i dont belive with my two eyes is just like a dream huyu mhuni anataka hela yake ijumaa iwe imeisha lipwa! hv sisi ni watoto ?
E Mungu inusuru Tanzania.
 
Kwa yeyote mwenye hekima; kwenye suala la Maslahi ya Kitaifa na katika kusimamia Maadili na Utawala wa Sheria, huwa hakuna misimamo ya vyama. Ama unasimama katika upande ulio sahihi au usio sahihi basi!

Nikiwa mwanachama wa CCM ,nakushauri Rais (Watendaji wengine wote ni wafuasi wako), usimame sasa na kuingilia kati hili 'jinamizi' la Dowans kwani sasa umeshamtambua mhusika maana amejileta, maana vinginevyo litatupeleka pabaya sana na tukifika huko naomba wana CCM wenzangu tusitafute mchawi bali kumbukeni tu hii thread yangu ya 'ikifika buchani nyama hairudi kuwa ngómbe!

Hakika,haiitaji mtu kuwa na shahada kuweza kuona kuwa, HATA KAMA TUNA SHIDA VIPI YA UMEME,

1. HATUWEZI KUKUBALI KUINGIA MKATABA NA MFANYABIASHARA AMBAYE WAASISI WAKE (AU MWENYEWE) WALISHAANZA KWA KUTUTAPELI!

2. MAELEZO YA KAMPUNI YAO YAMEGUBIKWA NA UTATA MKUBWA

3. TULISHAFIKISHWA MAHAKAMANI NA TUMEHUKUMIWA NA SASA TUKO KWENYE MCHAKATO WA KESI MAHAKAMANI (PINGAMIZI)

4. NA HATA KUJA KWA MWAKILISHI WA KAMPUNI , HAKUNA ANAYETAKA KUKUZUNGUMZIA SI WIZARANI WALA TANESCO, ZAIDI YA YOTE SAUTI YAKE INASAFIRI KWA KASI KULIKO MWANGA WAKE NDO MAANA HATA WAANDISHI WAKASHINDWA KUPIGA PICHA YAKE KATIKA TUKIO KUBWA LA WAZI AMBALO YEYE MWENYEWE NDO KAITA PRESS CONFERENCE!
Naombeni mwongozo hapa, kama yeye alikuwa na haki ya kusema asipigwe picha, je na sisi kama Taifa hatukuwa na haki ya kusema pia masikio yetu hayataki kusikia habari yake na matarajio yake kwenye press conference?

Narudia tena maana nina uchungu sana. Rais Mh. Kikwete, Kheri mie Mwanachama wa chama chako ninaye weza ona kilicho mbele yetu na nikakisema kuliko yule mwingine ambaye naye kakiona hakisemei na au badala yake tunaanza kuingiza siasa na kujaribu kudilute utapeli huu (a scandal) eti in the pretext of the continued possible utility or 'innocence' of Dowans power supply generators or irresponsible statements such as 'we just want to have uninterrupted power supply! Whatever! Kweli? Hata kama mtu atatokea na kutuambia kuwa yuko tayari kusambaza nishati ya uhakika nchi nzima isipokuwa tuwe tayari kumpa chochote atakachotaka kama ahadi kwa Binti Herodia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom