GHOST RYDER
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 1,025
- 475
Ijumaa ya Fat-wah Mwanza; RC na RPC Si siku ya Kukaa Ofisini leo
Bahati mbaya sana hata wachangiaji waliochangia thread hiyo wengi waligubigwa na hamaki za imani za kidini badala ya kuzingatia mkondo wa sheria na kupeana mawazo chanya yatakayokomesha matabaka ya kidini na kuchanganywa siasa na Dini. (Thanks kwa invisible kutumia hekima kuifunga thread hiyo, hata hii ikipinda leo; Mkuu ifunge pia)
Tusisukumwe sana na ushabiki wa kidini na kusahau shaeria za Nchi na kutaka kuamua mambo kwa hamaki na kudhihakiana imani za kila mmoja tuweke umoja na utaifa mbele ili kuhakikisha tunajenga kuheshimiana kila mtu katika kuabudu kwake hata kama kuabudu huku ni kule kwa mapangoni.
Napoandika thread hii na utangulizi huo ambao sitapenda kabisa ufungamanishwe na ushabiki wa kidini ndugu yangu Mkuu wa Mkoa mpya EVARIST WELLE NDIKILO na Kamanda wa Jsehi la Polisi Mwanza leo si siku ya ninyi kukaa Ofisini wala kujipanga na weekend. Fat-wah kubwa inayotarajiwa kufanyika Mwanza leo ni hatari kama hekima haitatumika mapema kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Inawezekana kabisa Viongozi wa Dini ya Kiislam wakawafuata leo kushauriana katika hili au wasifuate kabisa kutokana na presha kubwa iliyopo kwa baadhi ya waumini wasiokuwa wasikivu kutokana na kadhia ya kuchomwa moto kwa Quran hapo majuzi.
Jana kucheleweshwa kwa maamuzi na ufinyu wa taarifa za kiintelijensia ulitoa mwanya kwa baadhi ya kundi la watu wasiojulikana kuchoma moto kanisa ambalo wanadaiwa kutoa waumini waliochoma moto Quran.
Ni bahati nzuri kuwa uharibifu na moto vilidhibitiwa mapema, bahati mbaya ni kwamaba mamlaka husika ziliteleza kuchukua udhibiti wa tukio zima toka hadhari ya mapema hapa JF ambayo tunajua mnasoma na mnatambua kuwa tunafanya hivi si kwa uchochezi bali kuwapa nyongeza katika intelijensia iliyofeli na matokeo yake tunaishia kulaumiana katika maafa.
Kwa moyo wa kujishusha kabisa watafuteni viongozi wa Dini ya Kiisalam Mwanza, Sheikh wa Mkoa Salum Fereji na wasaidizi wake wawaweke pamoja maimam na kuhahakikisha hii fat-wah inayokusudiwa kufanyiak leo Jijini Mwanza baada ya sala ya Ijumaa haifanyiki na ibada ziendelee kama kawaida huku sheria ikichukua mkondo kwa waliochoma Quran na waliochoma kanisa kwa pamoja.
Kalam na fikara zangu zimenituma kuyasema haya baada ya kupata taarifa muda si mrefu kutoka Mwanza kuwa hali si ya kuridhisha juu ya suala hili. Hofu na mashaka ni mazito na madhara yatakuwa makubwa kama hekima haitatumika mapema.
ADIOS
UPDATES:
Kikao kati ya RC, Sheikh wa Mkoa, Imam wa Msikiti wa Furqaan Lumala na Viongozi wengine kimefanikisha kuzima Jaribio la Fat-wah kubwa iliyotarajiwa leo Mwanza. Uamuzi wa Busara na Mazungumzo yamefanikisha hili...Kumbe inawezekana kabisa.
Misikiti mingi inaarifiwa kuhudhuriwa na waumini wachache katika sala ya Ijumaa huko Mwanza hasa katika Vitongoji vinavozunguka LUMALA, maeneo ya Kilimahewa, Pasiansi, Ilemela na Nyasaka. Inahofiwa waumini wengi walijiunga katika misikiti iliyotangaza hapo jana kufanya maandamano kwenda Lumala na wengine wengi wakisali Lumala kutegemea tamko lolote la kisasi.
Hekima na Subira vimefanikiwa.
Angalizo:
Sauti za chini zinashinikiza Polisi kukamilisha Upelelezi haraka na Mahakama kuendeshan kesi hiyo kwa uwazi na haraka ili kuepusha kadhia nyingine kwani viongozi wamewasihi waumini wao kubuta subira hadi muafaka utakapopatikana.
Source: Afisa Jeshi la Polisi Mza (Jina limehifadhiwa)
- Kanisa lachomwa Moto
- Maandamano makubwa kufanyika kuelekea eneo laTukio