Ijue taaluma ya Kuchakachua kura

JohnShao

Member
May 6, 2010
18
3
Wizi wa kura una historia ndefu na umeshatumika katika nchi kadhaa duniani. Kwa hiyo mbinu zake zinajulikana nazo ni pretty standard ijapokuwa kuna wataalamu wa uchakachuaji wanaozungukia serikali ambazo zimepoteza imani ya wananchi na kuzishauri, kwa malipo ya bei mbaya, namna ya kuchakachua kura ili waendelee kutawala licha ya kwamba hawana ridhaa ya wananchi wengi. Wa-tz, baada ya vituko vya uchaguzi uliopita, inabidi tujifunze swala la uchakachuaji wa kura kwa marefu na mapana yake, mbinu zinazotumika na kinachobidi kufanyika illi kuuthibiti. La sivyo hali itajirudia kesho, kesho kutwa na hata mtondo. Anza na makala hii hapa.

View attachment Uchakachuaji wa Kura by Wiki.docx
 
Wizi wa kura una historia ndefu na umeshatumika katika nchi kadhaa duniani. Kwa hiyo mbinu zake zinajulikana nazo ni pretty standard ijapokuwa kuna wataalamu wa uchakachuaji wanaozungukia serikali ambazo zimepoteza imani ya wananchi na kuzishauri, kwa malipo ya bei mbaya, namna ya kuchakachua kura ili waendelee kutawala licha ya kwamba hawana ridhaa ya wananchi wengi. Wa-tz, baada ya vituko vya uchaguzi uliopita, inabidi tujifunze swala la uchakachuaji wa kura kwa marefu na mapana yake, mbinu zinazotumika na kinachobidi kufanyika illi kuuthibiti. La sivyo hali itajirudia kesho, kesho kutwa na hata mtondo. Anza na makala hii hapa.

View attachment 17748

Hii nimeipenda nitaisoma kikamilifu kama vile nasoma DESSA baada ya kushikwa.
 
Electoral fraud by Wikipedia
http://en.wikipedia.org/wiki/Electoral_fraud

  • It's not the votes that count. It's who counts the votes.
  • You won the election, but I won the count.
Electoral fraud is illegal interference with the process of an election. Acts of fraud affect vote counts to bring about an election result, whether by increasing the vote share of the favored candidate, depressing the vote share of the rival candidates or both. Also called voter fraud, the mechanisms involved include illegal voter registration, intimidation at polls and improper vote counting.

Hii ni Tafsiri yangu yangu ruksa kukosoa.

Techniques

Vote fraud in legislature- Hapa wanachakachua kwa kutumia sheria


Destruction or invalidation of ballots- Hapa unaamua tu kuharibu kura za wapinzania na kuzifanya zako ziwe nyingi


Misuse of proxy votes- Utaratibu huu mtu anajaza form kwamba hataweza kupiga kura kisha form hiyo kubadirishwa na mtu mwingine kuitumia kupiga kura. Sijui kama Bongo tuna utaratibu hui.


Misrecording of votes- Hii Jamaa wameitumia, HataMH Kikwete mwenyewe siku akihojiwa nyumbani kwake kule kwa wachoma mkaa alikiri kwamba misrecording ni kitu cha kawaida.Badala ya kuandika 29,700 unaandika 3000 kwa makusudi. Hii ni pamoja na kupotosha chagua la Wasio ona na wale wasio jua kusoma na kuandika.


Ballot stuffing Mtu mmoja kupiga zaidi ya kura moja, kupiga kura zaidi ya kituo kimoja, kupiga kura kwa kutumia jina mtu mwingine, kupiga kura kwa kutumia majina ya marehemu,kumpiga mcheche mpiga kura akiwa ndani ya chumba cha kupigia kura kiharamia ili achague mtu fulani. CCM waliitumia hii. Unakumbuka kule Mwanza watu walikamatwa wakiwa na Hati za kupigia kura?


Misleading or confusing ballot papers Kuchapisha hati za kupiga kura katika namna inayochanganya watu ili mtu fulani apigiwe kura.Kuweka wagombea wa chama na majina yenye kufanana ili mradi kutia kiwingu wapiga kura.


Misinformation Kutoa taarifa rasmi zisizo kweli/za uongo kupitia vyombo vya habari vya kiserikali ili kupotosha kwa makusudi. Kufanya kampeni za maji taka na za kupakaziana mambo yasiyo ya kweli.
(KM Dr Slaa kaiba Mke wa Mtu wakati jamaa mwenyewe anayepakaziwa kuwa ni mwenye mke hana habari pia hajaona ndani kwa kipindi kisichopungua miaka 3 hiii hiii)

Vote buyingHii ni ile ya kununua hati kutoka kwa mpiga kura ili siku ikifika aipige kura

Intimidation- Kupigwa mkwara au Jamba^2


-Violence or the threat of violence- Kufanyia fujo na vurugu au kutishiwa kufanyiwa vurugu

-Attacks on polling places- Kupiga mtu siku ya kupiga kura vituoni

-Legal threats kutishiwa kuchukuliwa hatua za kisheria bila mpango

-Economic threats- Kutishiwa kufungiwa biashara au kunyimwa leseni au mali kutaifishwa au kupakaziwa kwamba utajiri wako ni haramu .kutishiwa Kuhusishwa na mambo haramu. kupigwa mkwara na majiri.


Disenfranchisement- kutunga sheria inayozuia watu fulani kupiga kura. Pia, kuweka mazingira ambayo watu fulani watajiona hawako huru kwenda kupiga kura. watu wengi wanafanya shughuli zao huku wakikwaruzana na polisi kuweka polisi wengi vituoni kunaweza wanyima uhuru watu kadhaa kwenda kupiga kura


Manipulation of demography- Mtu iko 15,000 serikali inadai kuna mtu 45,000. Mtu iko 50,000 serikali inadai kuna mtu 12,000 tu. Hii ni pamoja na kuruhusu wakimbizi kupiga kura na kuwanyima haki raia ili kuleta ushindi


Gerrymandering- Huu ni mchezo wa kugawa majimbo na kuweka mipaka ya majimbo kinyemela ili mtu fulani ashindwe na mwingine ashinde.


Electorate manipulation
Hii ndo baba lao ambayo NEC walitumia kuchakachua kura.
Most electoral fraud takes place during or immediately after election campaigns, by interfering with the voting process or the counting of votes.
 
Mkuu hapa umetuelimisha sana. Kumbe 'uchachuaji' ni kozi kabisa!!!! Duuuuuu, ama kweli duniani kuna mambo. Thread hii ni muhimu sana kwa chadema itabidi watakafari kwa kina mbinu moja baada ya nyingine na kuzitafutia mbinu za kupambana nazo ili zisiwaletee mafisadi matunda wanayoyatarajia. Mbinu zote hizo zikidhibitiwa kwenye chaguzi za majimbo lazima chama fulani bungeni ndicho kitakuwa cha upinzani kwa kuwa na wabunge wachache na hapo ndipo mchakato wa kuunda katiba mpya utakapoanza.
 
Thanks Madela wa Madilu kwa bidii yako ya kutafsiri faster angalao sehemu ya makala ya Taaluma ya Uchakachuaji wa kura kwa faida ya wasomaji wengi zaidi. Bidii za namna hii kwa wingi ndiyo zitakazoleta mabadiliko.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom