Ijue stun grenade au flash bang grenade (bomu la sauti) inavyo fanya kazi

Zacht

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
1,009
2,197
m84-stun-grenade-01.jpg


Umewasha wahi kuona kwenye movie .Timu ya SWAT au kikosi chochote cha kijeshi inapovamia kwenye nyumba ya kikundi cha wahalifu. Afisa mmoja hutupa kitu ndani ya chumba, na hulipuka kinatoa mwanga mkali na kelele kubwa. Wahalifu hao waneshtushwa na kuonekana kama kuzubaa muda mwingine kuziba masikio hapo askari huwashambulia kwa urahisi .kile kifaa au bomu linaitwa flash bang grenade au stun grenade.
flashbang2_f.jpg
I

Flash bang nini?
Ni bomu la mkono(grenade) lenye mlipuko mwepesi(usio sababisha kifo kwa urahisi) ambalo linatoa mwanga mkali na kelele likilipuka, flash bang grenade au stun grenade linatoa mwanga kwa kiwango cha megacandela (Mcd) 7, wakati Mshumaa wa kawaida hutoa mwanga megacandela(Mcd) 1, pia linatoa kelele za kiwango cha 170 decibels (dB) ambayo ni kubwa kuliko mlio wa risasi wenye (dB) 140. Liligunduliwa katika miaka ya 1970 na ilitumiwa kwa mara ya kwanza na Jeshi la Uingereza.

Inavyo fanya kazi
Kutokana na tabia yake ya kutoa mwanga mkali na kelele, Kifaa hicho kikilipuka mwanga unaotoka unazidi uwezo wa seli za Photoreceptor kwenye jicho ambazo kazi yake ku-control na reduce mwanga unaoingia kwenye macho, hivyo humfanya mshambuliwa afumbe macho kwa takriban sekunde tano. pia husababisha uziwi wa muda kwa mwathirika na masikio kupata maumivu makali.

Madhara ya stun grenade
Kama ilivyo kawaida ya kila kitu kina faida yake na madhara yake, matukio kadhaa yamelipotiwa kusababishwa na stun grenade kama yafuatayo ;

1.Tarehe 14 Novemba, 2019, mwandamanaji huko Baghdad alikufa hospitalini kutokana na majeraha yaliyotokana na stun grenade ya ilyotupwa katika umati wa waandamanaji wakati wa mzozo na viongozi wa Iraqi.

2.Mnamo tarehe 3 Agosti 2014, shabiki wa Makedonia wa timu ya mpira ya miguu ya FK Vardar alijeruhiwa vibaya wakati wa mchezo wa mpira wa miguu baada ya kujaribu kutupa bomu hilo liliyotupwa na polisi wakati mapigano kati ya polisi na mashabiki yaliyotokea kwenye uwanja wa stadion Tumbe Kafe huko Bitola. Stun Grenade ililipuka mikononi mwake na kusababisha apoteze vidole viwili.

3.Mei 2003, mwanamke mmoja anayeitwa Alberta Spruill alikufa kutokana na mshtuko wa moyo baada ya timu ya polisi kutupa grenade kwenya makazi yake huko Harlem, New York .

4.Februari 2011, afisa wa polisi huko marekani ( SWAT) alijeruhiwa nyumbani kwake wakati grenade ilipo funguka kwa Bahati mbaya, Alifanyiwa upasuaji wa dharura, lakini baadaye alikufa kutokana na jeraha lake.

5.Januari 2011, Raia wa California marekani aitwae Rogelio Serrato alikufa kutokana na kuvuta moshi baada ya bomu hilo kutupwa na timu ya polisi ya SWAT na kuwasha moto nyumba yake. Mtu huyo aliaminika alikuwa amejificha kwenye chumba cha kulala wakati moto ulipotokea.
 
bongo naweza kuyapata kwa tsh ngapi
Sijui hata yanako patikana, lakin hizi ni siraha kama ilivyo mabomu ya machozi, risasi za mpira nk. Yanakuwa chini ya Serikali (kwetu bongo) kwahy hauwezi kuyapata kwa urahisi
 
kuna uwezekano yakatumika kwa wakili msomi.?

au umejiandikia tu
 
bongo naweza kuyapata kwa tsh ngapi
Ukitaka kuyapata labda uwende kwenye mtandao wa black market ndo utapata maana ni siraha ambayo utakiwi raia wa kawaida kutumia au kuwa nayo.

Mi nimeagiza kifaru kwenye mtandao wa black market, nimeambiwa mpaka mwezi wa 11 kitakuwa kimenifikia
 
Ukitaka kuyapata labda uwende kwenye mtandao wa black market ndo utapata maana ni siraha ambayo utakiwi raia wa kawaida kutumia au kuwa nayo.

Mi nimeagiza kifaru kwenye mtandao wa black market, nimeambiwa mpaka mwezi wa 11 kitakuwa kimenifikia
Safi
 
Mwaka 1983 nikiwa Vietnam tukicheza rede na watoto wenzangu, niliokota hicho kidude nikakirusha juu tugombanie kama "Sadakalawe" hadi leo mimi ndiyo nipo hai.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom