IJUE SOKA: Unawezaje kuwa mpiga danadana mzuri? Send to a friend | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IJUE SOKA: Unawezaje kuwa mpiga danadana mzuri? Send to a friend

Discussion in 'Sports' started by Dr. Chapa Kiuno, May 17, 2010.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kujifunza kupiga danadana siyo sana suala la ujuzi bali ni suala la kufanya mazoezi. Ukiwa unaweza kupiga danadana utakuwa na stamina nzuri na kuweza kuuchezea mpira vizuri unapokuwa unacheza uwanjani, pia utaweza kuugusa mpira vizuri. Kumbuka kwamba ukiwa mchezaji, watu watavutiwa na wewe kama utaweza kupiga danadana zaidi ya 100.

  Ukitaka kuweza kupiga danadana vizuri zifuatazo ni hatua unazoweza kuchukua;

  Kwanza, weka mpira chini halafu uunyanyue na mguu ambao unautumia sana. Mpira ukinyanyuka jitahidi kuupiga mpira juu usawa wa mikono kila mpira unapotua mguuni mwako, usiupige mpira kwa nguvu kwa sababu utakwenda juu sana, zoezi hilo inabidi ulirudie rudie mpaka uzoee kupiga mpira ufike eneo usawa wa tumbo. Ukiweza kupiga danadana kwa mguu mmoja, jifunze pia kupiga danadana kwa kutumia mguu mwingine ambapo zoezi hili ni gumu. Jitahidi kuelewa hatua moja kabla haujaenda katika hatua nyingine.

  Hatua ya pili ya kujifunza kupiga danadana ni kuongeza idadi ya danadana. Unapopiga danadana jitahidi mpira usianguke chini na hata mpira ukianguka usiuokote kwa mikono ila unatakiwa uunyanyue kwa mguu. Jitahidi kupiga danadana nyingi kwa muda mrefu kwa kutumia mguu mmoja.

  Hatua ya tatu ni kubadilisha mguu. Baada ya kuweza kupiga danadana kwa kutumia mguu ambao unautumia sana jitahidi kujifunza kupiga danadana kwa kutumia mguu mwingine ambao hauutumii sana.
  Ukishaweza ufanya hivyo, sasa unaweza kupiga danadana kwa kutumia miguu yote kwa kuchanganya, unapiga danadana moja kwa mguu wa kulia na moja kwa mguu wa kushoto hivyo hivyo unaendelea. Mwanzo utakuwa unahama hama wakati unapiga danadana hizo, lakini ukishaweza utakuwa unatulia sehemu moja na kupiga danadana kwa kutumia miguu yote miwili.

  Hatua ya nne ni kujifunza kunyanyua mpira. unapotaka kujua kupiga danadana vizuri ni muhimu ukajua pia kunyanyua mpira kwa kutumia miguu yako. zipo njia nyingi za kunyanyua mpira ukiacha kubetua.

  Mambo ya kuzingatia unapopiga danadana ni kwamba usivae bukta ndefu ambayo itakuzuia kupiga danadana vizuri, vaa bukta fupi. Pia jitahidi kutulia unapokuwa unapiga danadana.
  IJUE SOKA: Unawezaje kuwa mpiga danadana mzuri?
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,050
  Trophy Points: 280
  Mi nataka unifundishe kupiga tikitaka
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  umenikumbusha tulivyokuwa wadogo mashindano ya danadana si mchezo mambo ya kulipana sio ha ha ha.raha sana ilikuwa.
   
Loading...