Ijue Siri: Kwanini Njia ya Kigoma - Dar haina mabasi mengi ya ( luxury )

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Njia ya Dar-Kigoma, Dar-Sumbawanga Ni miongoni mwa njia chache Sana ambazo ukiomba kibari Cha njia (TLB ) Kutoka SUMATRA hutasumbuka hata kidogo!

Hii inatokana na dhana ya uhaba wa mabasi kwenda maeneo hayo!

Swali hapa je, kwanini Ni machache?

  • Wengi wanadhani uhaba wa mabasi unachangiwa na Miondombinu (barabara)
  • Wengi wanadhani uhaba wa mabasi unachangiwa na uchache wa abiria.
  • wengi wanadhani uhaba wa mabasi unachangiwa na uwepo wa Gari Moshi!
UKWELI NI KWAMBA hivyo vyote si sababu ya msingi kwa wafanya biashara kupeleka mabasi Kigoma na Rukwa!
kwasababu;
  • Kama ni ishu ya barabara, Njia ya zamani ya kuzunguka RUNZEWE haitumiki tena, Sahivi Kuna lami mpya kutokea Manyoni hadi Tabora (shortcut) na kutoka Tabora hadi Kigoma
  • Kama ni Abiria toka kigoma wapo wa kutosha tena wengine kutoka Rwanda na Burundi
  • Kama ni Gari Moshi, Ukweli Ni kwamba, Abiria wa mabasi na wale wa treni hawafungamani, hii ni sawa na abiria wa tax na wa bodaboda wasivyofungamana, Kila usafiri una abiria wake!
SIRI YA NJIA HIZO KUWA NA MABASI MACHACHE NI USHIRIKINA

Yes! Bila kuweka Natural Capastor! Njia ya kigoma Basi jipya Halitoboi hata siku moja! Akijitahidi Sana Atakwenda ruti moja ya pili hageuki!

Wababe wa njia Saratoga, adventure wamedumu kwenye njia hizi kwasababu ya Natural Capacitor!

Mwenye Basi jipya akithubutu njia hizo bila kufunga capacitor ajiandae na mapigo Kama;
  1. kwanza kabisa Basi jipya likianza Safari njia hizo hata ukitumia dreva mwenyeji- Ni pigo la kupotea njia ( yaani utaondoka Dar vizuri lakini huko mtauliza Sana njia kwa kupotea potea!
  2. Pigo la pili Ni GIA Kugoma kuingia; Yaani Gari utaifanyia service fresh kabisa utapeleka stendi tayari kwa safari kubeba abiria lakini ukishatoka nje ya mji tu, Gia zinaanza kumiss na zinapotea! Utaita fundi kutengeneza hadi zipatikane inakuwa tayari ishakua mchana na abiria washachoka!
  3. pigo la tatu ni kupigwa cheti au faini huko njiani; Yaani Askari wakiliona gari lako tu hasira zinawajaa bila sababu (kimavi) Utapigwa faini usipoangalia na gari lako utalikuta kituoni hata sababu ya msingi ya kukamatwa haitakuwa ya maana..
  4. Ukiruka hizo tatu zote bila kuweka capacitor....Namba nne Itakuwa Ni..............
  5. Namba tano Utakomaa Sana kufuatilia bima! na Ikitokea ukilipwa lazima utangaze kwenda Kuanza biashara ya kilimo Ambako nako huko Wafugaji wanakusubili!
Mwisho: Ingawa siyo mwisho kwa umuhimu; UKIJUA KUOMBA HAKIKISHA UNAJUA KUKILINDA PIA!
Kama Imani yako ni haba FUNGA capacitor kwenye kila jambo!

Kila njia Ina Barrier (BERIA) ya kishirikina kila mkoa kwa wafanya biashara hususani maroli na mabasi; Mfano BERIA ya MTO WAMI :
kibaha na mlandizi kwa mkoa wa pwani etc

Na kwasababu wazungu wanalijua Hilo!
Wengi wamefungwa na password hii"
" Amelaaniwa Amtegemeae Binadam na kumfanya Kinga yake"

Je; Hujawahi kuta Basi limeacha njia Wakati nyuma limeandikwa "IN G*D WE TRUST"?
 
kigoma majungu mengi sana. Na majungu yamezaa uchawi sema uchawi una raha yake kwa watu kama mimi.
 
Ni ulemavu wa fikra na akili kutawaliwa na mawazo hayo katika zama hizi za sayansi na teknolojia!

Hata kwa macho tu ya kawaida hali ya uchumi wa mkoa wa kigoma inakupa jawabu la maswali yako yote!

Mtoa mada jitoe kwenye huo utumwa wa fikra na uitumie akili yako inavyotakikana!
 
Ni ulemavu wa fikra na akili kutawaliwa na mawazo hayo katika zama hizi za sayansi na teknolojia!

Hata kwa macho tu ya kawaida hali ya uchumi wa mkoa wa kigoma inakupa jawabu la maswali yako yote!

Mtoa mada jitoe kwenye huo utumwa wa fikra na uitumie akili yako inavyotakikana!
Ulemavu upi mkuu
 
Biashara ya mabas lazma ujipange Sio yakukurupukia. Kamuulize ZUBERI ndio anajua kilicho mkuta huko.

Hata njia ya mwanza - musoma kuna kijiji kipo katikat hapo kabla ujafika magu ukiwa unatoka musoma, pale bas uwa aitakiwi kusimama ila kama kwenye bas kuna abiria anashukia hapo inabid mkubari kumshushia hapo las hvyo hamtafika mnapoenda yan pale ukigonga ata kuku shuka umtafte mwenye nayo umuombe samahan mbali na hapo utofika unapo enda salama.

Yan kama upo stend alaf ukamwambia konda unaenda kwenye hcho kijiji unaweza usipate ticket kabsa maana wanapaeshim mno kwa uchawi
 
Biashara ya mabas lazma ujipange Sio yakukurupukia. Kamuulize ZUBERI ndio anajua kilicho mkuta huko.

Hata njia ya mwanza - musoma kuna kijiji kipo katikat hapo kabla ujafika magu ukiwa unatoka musoma, pale bas uwa aitakiwi kusimama ila kama kwenye bas kuna abiria wa anashukia hapo inabid mkubari kumshushia hapo las hvyo mtafika mnapoenda yan pale ukigonga ata kuku shuka umtafte mwenyewe nayo umuombe samahan mbali na hapo utofika unapo enda, yan kama upo stend alaf ukamwambia konda unaenda kwenye hcho kijiji unaweza usipate ticket kabsa maana wanapaeshim mno kwa uchawi
:D :D :D :D :D :D :D :D
 
Unataka kuniambia uchawi upo kigoma na sumbawanga tu? Hapo unaelezea mawazo yako nawala si uhalisia. Waambie waloge na train basi!

Saratoga mwenyewe ameanza kufulia yutong zote hana amerudia macheses ya malori. Hivi bado watu wenye mawazo mfu Kama wewe mpo tu?
 
Unataka kuniambia uchawi upo kigoma na sumbawanga tu? Hapo unaelezea mawazo yako nawala si uhalisia. Waambie waloge na train basi! Saratoga mwenyewe ameanza kufulia yutong zote hana amerudia macheses ya malori. Hivi bado watu wenye mawazo mfu Kama wewe mpo tu?
Hilo treni Ni miongoni mwa hirizi tano za Taifa! ipo siku nitakuwekea list na vile zinavyofanya kazi!
Nakushaa unavyowaza kuiroga hirizi
 
Namba 4 umenifurahisha, wakulima noma Masai Wasukuma wakiona mimea ya mazao wameona nyasi.
Utasikia wanakwambia IACHE ILE.....ole wako uwafukuze ng'ombe mshale utakuhusu! hapo ndipo utaelewa kazi ya capacitor ilivyomhimu
 
ishu ni Uchawi tu!!
kwani mbona Saratoga ana basi mpya?
kuhusu kupotea njia unaajiri dereva wa kigoma

njoo na hoja ya maana.
Barabara ya kahama - nyakanazi - kakonko - kibondo - kasulu - Kigoma unapoteaje??
mi nimeenda kgm mara moja na nauhakika sipotei
 
Hana hamu,lipo mtoni Hadi leo
Anasema ana iman! Imani unaweza ukawa nayo lakini je kwenye matendo imo? gari unaimwagia maji ya baraka na maombi lukuki lakini ukikamatwa njiani Unatoa Rushwa ili mzigo ufike.

Kama rushwa Ni dhambi Ni Mungu gani atakurindia Mali yako! hapo ndipo Washirikina WANAPITA NA ROLI LAKO HIVI o_Oo_Oo_O
Bila capacitor biashara utajisikia tu
 
ishu ni Uchawi tu!!
kwani mbona Saratoga ana basi mpya?
kuhusu kupotea njia unaajiri dereva wa kigoma

njoo na hoja ya maana.
Barabara ya kahama - nyakanazi - kakonko - kibondo - kasulu - Kigoma unapoteaje??
mi nimeenda kgm mara moja na nauhakika sipotei
WAHA MNAPENDA UBISHI SANA, Brother kwani hapa tunabishana au! JIULIZE Kwanini mabasi Ni MACHACHE kigoma! kwanini hakuna luxury bus kigoma! ACHENI TABIA ZENU ZA UBISHI, Kwanza WABUNGE WANAOGOMBEA KIGOMA.

ITISHENI KIKAO CHA KIMILA ILI MUWAELIMISHE WASHIRIKINA UMHIMU WA MAENDELEO WA WATU NA VITU IKIWEMO MABASI NA MIUNDOMBINU...ili wasiroge
 
Back
Top Bottom