Ijue sheria ya vyama vya siasa nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ijue sheria ya vyama vya siasa nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Mar 31, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Sheria ya vyama vya siasa nchini


  Na Allan Kajembe

  BAADA ya mfumo wa vyama vingi kuridhiwa na Watanzania, sheria ya kuratibu mambo yote yanayohusiana na vyama vya siasa ikatungwa hapa nchini.

  Lengo likiwa ni kuyachukua masuala yote yanayohitajika kufanywa katika shughuli ya vyama vya siasa nchini.

  Hii ni sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992. Kwa mujibu wa sura ya utangulizi ya sheria hii, madhumuni ya sheria hii ni kuelekeza taratibu, vigezo na masharti yote yanayohusu kusajili vyama pamoja na mambo mengine yanayoendana na hayo.

  Chini ya kifungu cha 2 cha sheria hii, chama cha siasa kimetambuliwa kama muungano maalum wa watu wenye lengo la kuunda serikali kuu kwa kutumia njia ya uchaguzi au kumunga mkono yeoyote katika uchaguzi huo.

  Sheria hii inatumika katika pande zote za nchi yetu, yaani Tanzania Bara na Zanzibar.

  Kwa chama cha siasa kutambuliwa kama chama cha siasa, kinatakiwa kwanza kitimize masharti yaliyowekwa katika kifungu cha (7) kinachokitaka chama chochote kabla hakijaanza kufanya kazi lazima kiombe na kipate usajili toka kwa msajili wa vyama vya siasa, ambaye amepewa mamlaka hayo na sheria hii, na kwamba chama chochote ambacho hakijapata usajili toka kwa msajili kimepigwa marufuku kufanya shughuli zake.

  Kwa mujibu wa kifungu cha nane cha sheria hii, chama chochote cha siasa ni lazima kwanza kisajiliwe kwa muda na kupewa cheti cha usajili wa muda na kwamba ni lazima kimalize na kutimiza masharti yoyote yaliyo katika kila hatua ya usajili wa muda na hatua ya pili ya usajili wa kudumu.

  Chama kilichosajiliwa kwa muda kinatakiwa ndani ya siku 130 kipewe usajili wa kudumu baada ya kutimiza masharti yanayopatikana katika kifungu cha tisa na kumi cha sheria hii.

  Masharti haya ni pamoja na waanzilishi wake waende kufanya usajili wa chama kwa msajili, maombi haya yawe yameambatana na katiba ya chama hicho kitarajiwa na kwamba upatikanaji wa wanachama wa chama hicho ni huru bila kushurutishwa na kwa ajili ya wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano bila kubagua dini, jinsia, kabila, uwezo wa elimu (taaluma), wala kazi ya mtu.

  Kwa msingi wa kifungu cha 9(2) cha sheria hii, chama cha siasa kimekatazwa kufanya mambo niliyoyaorodhesha hapo juu, lakini pia hakitasajiliwa kama kitakuwa kina sera zinazotetea kuvunjika kwa muungano wa Tanzania au matumizi ya nguvu katika kupata wanachama na kufanikisha malengo yake ya kisiasa au kama chama hicho hakina mfumo wa kuchagua viongozi wake kila baada ya muda fulani.

  Vilevile chama cha siasa hakitasajiliwa kama chama hicho kinafanya kazi katika upande mmoja tu wa Jamhuri ya Muungano.

  Kwa kuongezea masharti hayo ya sheria, sheria hii chini ya kifungu cha kumi kimetoa masharti mengine ya ziada kwa vyama vya siasa kupata usajili, ambapo chama kitatakiwa kuwa na wanachama wenye vigezo vya kuandikishwa kama wapiga kura katika chaguzi mbalimbali si chini ya 200 waliopaikana katika mikoa isiyopungua kumi ya Jamhuri ya Muungano, miwili kati ya hiyo iwe imetoka Zanzibar ( Pemba mmoja na Unguja mmoja).

  Chama hicho pia kitatakiwa kiwe kimewasilisha majina ya viongozi wake ambao ni lazima wawe wametoka katika pande zote mbili za muungano, na pia kimepeleka taarifa ya wapi makao yake makuu yalipo (ndani ya Jamhuri ya Muungano).

  Baada ya kusajiliwa chama cha siasa kitakuwa na haki na upendeleo kama zilivyoainishwa katika kifungu cha 11(1) cha sheria hii ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya hadhara katika eneo lolote lile ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa sharti kwamba kiwe kimepata kibali kutoka kwa mkuu wa wilaya wa eneo hilo.

  Pia chama cha siasa kina haki ya kupata ulinzi wa polisi kwa minajili ya kuendesha kwa usalama shughuli zao.

  Hata hivyo chama chenye usajili wa muda hakitaruhusiwa kusimamisha mgombea katika nafasi yoyote katika uchaguzi wa Serikali Kuu, wa serikali za mitaa, haki ambayo vimepewa vyama vilivyo na usajili wa kudumu pekee.

  Kitu kingine katika sheria hii ni katazo linalotolewa katika kifungu cha 12(1) cha sheria hii ambapo chama chochote kilichokuwa kimeundwa katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano kabla ya Februari 5, 1977, hakitaruhusiwa kufufuliwa na kupata usajili na wala kifupisho chake hakitaruhusiwa kutumiwa na chama chochote kinachotakiwa kupata usajili kwa muktadha wa sheria hii.

  Sheria hii pia imekataza kuundwa kwa tawi au kikundi chochote cha wanawake au vijana kinachohusiana na chama chochote cha siasa katika maeneo yoyote ya kujisomea kama shule au vyuo.
   
 2. Mandla Jr.

  Mandla Jr. JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2014
  Joined: Dec 15, 2013
  Messages: 3,101
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wanabodi,
  Naomba kujua, sheria zinaruhusu vyama vya siasa kuungana katika kupata jambo lolote?? Lakini vyama vyote vyenye usajili Tanzania zina Katiba zao, je hili la kuungana limo katika katiba zao??

  Msajili wa vyama vya siasa katika hili anayo mamlaka ya kuvunja muungano wa vyama vya siasa??

  Mandla.
   
 3. m

  maalim john New Member

  #3
  Jan 22, 2017
  Joined: Nov 19, 2016
  Messages: 2
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
Loading...