Ijue Sheria ya Ardhi: Taratibu za utatuzi wa migogoro ya ardhi

Je mtu mwenye miliki ya ardhi ya kijiji ilio chini ya hatimiliki ya kimila anaweza kupokonywa kwa kosa la kutoiendeleza .... Kma jibu ni ndio ni ndan ya muda gani mtu yampasa aendeleze na kw baada ya muda gani atapokonywa asipoendeleza.....NAOMBA MSAADA WAKUU

Kupokonywa ardhi kunatokea pale ambapo utakuwa umekwenda kinyume cha masharti yaliyowekwa kwenye hati husika.Masharti haya huwa yamewekwa wazi sio swala la kusema to hujaendeleza.

Kuendeleza sio lazima kujenga hata kulima. Dhana ya kuendeleza inategemeana na matumizi yaliyokubaliwa.

Hata hivyo kwa ardhi za vijijini hati za kimila nyingi nilizoona hazina hayo masharti hayo. Hivyo si rahisi kupokonywa.
 
Mkuu nakuhitaji PM
 
Habari za majukumu wana jamii foroum. Kuna issue moja inanisumbua nataka kufahamu kisheria imekaaje. Kuna eneo tumenunua mimi na wenzangu na pia yumeshaanza kujenga, aliyetuuzia ni mmiliki halali wa eneo ila kuna issue kwamba lile eneo lilipimwa na kuna plani ya shule ya sekondari ya private. Ila wanazengo wanasema yale mapimo sio halali kwani hawakuwashirikisha wanazengo wa lile eneo na Mwenyekiti wa kijiji nae pia hajashirikishwa na wanasema mapimo ya lile eneo sio halali ukienda ardhi wanakuonyesha plani kua ni eneo la shule na kunajamaa anakuja anasema ni lakwake na documents zake zinaonesha ni za kitapeli. So kisheria imekaaje hii ama kwa mnaofahamu sheria mnaweza kutusaidia apa.
Sehemu unapoweza kujua kama document ni halali au la ni ofisi za ardhi za mamlaka serikali ya mtaa (halmashauri) na pia kwa msajili wa nyaraka..sasa nendeni huko mkajiridhishe kama document ni halali au la..
2. Kama wakati mnanunua eneo lilikuwa limekwishapimwa (japo wananchi hawajaukubali upimaji huo) ilikuwa ni wajibu wenu kupita ofisi za serikali (halmashauri) ili kujua matumizi yaliyopangwa katika maeneo yenu hayo..

3. Ukipata majibu ya vitu hivyo (upimaji ulifanyika lini, nyie mlinunua lini na huyo mtu mwenye shule alinunua lini, pia kama muuzaji wenu alistahili kupewa fidia je alipewa fidia, yalete hapa tutashauriana
 
Mkuu kama kuna jambo gumu katika ardhi ni hili. Kiuhalisia iwapo hao jamaa ni kweli wanamiliki eneo kihalali, nyinyi ni wavamizi na hamstahili kuwepo mahala hapo.

Japo kwa kuwa mmekaa muda mrefu natumaini mpo wananchi wengi. Kama mpo wengi nadhani ninaweza kuwashauri njia ya kufanya.

Pili je mmeendeleza hilo eneo? Kama ndio nawashauri kucheki status ya hao wanaodai wanamiliki (inawezekana milki yao kisheria ishaisha kwani miaka 30 ni mingi) iwapo itakuwa imeshaisha fanyeni mpango fasta wa nyie kupewa milki halali.

Kwa kuongeza, kama walivamia eneo na wakakaa miaka zaidi ya 12 bila bugudha..watakuwa wamethibitisha adverse possession hivyo wanastahili kumiliki eneo hilo
 
Kwa kuongeza, kama walivamia eneo na wakakaa miaka zaidi ya 12 bila bugudha..watakuwa wamethibitisha adverse possession hivyo wanastahili kumiliki eneo hilo
Mkuu adverse possession ina apply kwenye ardhi iliyo na hati na si vinginevyo...
 
Habari za majukumu wana jamii foroum. Kuna issue moja inanisumbua nataka kufahamu kisheria imekaaje. Kuna eneo tumenunua mimi na wenzangu na pia yumeshaanza kujenga, aliyetuuzia ni mmiliki halali wa eneo ila kuna issue kwamba lile eneo lilipimwa na kuna plani ya shule ya sekondari ya private. Ila wanazengo wanasema yale mapimo sio halali kwani hawakuwashirikisha wanazengo wa lile eneo na Mwenyekiti wa kijiji nae pia hajashirikishwa na wanasema mapimo ya lile eneo sio halali ukienda ardhi wanakuonyesha plani kua ni eneo la shule na kunajamaa anakuja anasema ni lakwake na documents zake zinaonesha ni za kitapeli. So kisheria imekaaje hii ama kwa mnaofahamu sheria mnaweza kutusaidia apa.
Kwa uelewa wangu ni kwamba kulingana na mgawanyiko wa ardhi makundi yote matatu ya ardhi yana taratibu tofauti ya usimamiaji

tukiongelea hili kundi la ardhi ya kijiji ambapo ndipo shauri lako lilipo ni kwamba hakuna barua ya toleo inayotolewa kwenye kundi hili (leter of offer) hadi ardhi hii ihaulishwe na kuwa ardhi ya kawaida hivyo kwenye ardhi ya kijiji kunatolewa hati miliki za kimila ambazo utaratibu wa kuzipata alishaeleza hapo juu mwanasheria msomi

Sasa kimsingi ili kijiji kiweze kupata hati miliki za kimila ni lazma kijiji hicho kiwe na mpango wa matumizi bora ya ardhi

Mpango wa matumizi bora ya ardhi unaainisha maeneo tofauti tofauti kijiji kulingana na ardhi iliyopo na uhitaji pia

Matumizi haya hupangwa na halmashauri ya kijiji na kupata baraka ya mkutano mkuu wa kijiji ili kukweba double alocation

Katika mpango huu kunaainishwa maeneo ya huduma za jamii kama vile shule, zahanati,maeneo ya makanisa, misikiti, makaburi na nk. Pia hutenga eneo la makazi na maeneo ya mashamba yaani kimsingi kwenye kipindi cha mpango kila eneo hutambuliwa kwa hiyo hakuna hati yeyote itakayotoka kabla ya mpango katika ardhi ya kijiji ikawa halali hivyo hizo document ambazo hao wengine wanazo hujatuambia kuwa ni document za namna gani au ni ile mikataba ya kienyeji ya mauziano?

Na kama hao wanaosema ni eneo lao la shule ya private kama watakuwa wana hati ya kamishina (yaani hilo eneo lilisha badilishwa kutoka ardhi ya kijij kuwa ardhi ya kawaida) lazma aoneshe mchakato jinsi alivyopata ikiwa na maana kuwa lazma awe na mhtasari wa halmashauri ya kijiji na ule wa wa mkutano mkuu sasa kama mwenyekiti naye hajui kuna maswali ya kujiliza hapa?

Na nyie mlinunua hilo eneo kutoka kwa nani je mliwashirikisha viongozi wa kijiji kama ushahidi wakati mnanunua?
Ni eneo lenye ukubwa gani?
Ili tuweze kujua mamlaka na taratibu za upatikanaji wa eneo hili lazma pia tujue ukubwa wa eneo

Karbu kujibu hayo hapo juu then tutaendelea pia mwanasheria msomi anaweza kuongezea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu adverse possession ina apply kwenye ardhi iliyo na hati na si vinginevyo...
Aisee, hebu naomba unielekeze kidogo kuhusu hii with authority ikibidi maana kuna watu wengi tu wamepoteza ardhi hata ambayo haijapimwa kwa base hiyo ya mtu kutumia zaidi ya miaka 12 with no disturbance..
Kama ni kwa maeneo yenye hati tu naomba nielekeze vizuri mzee
 
Je iwapo baraza zima la ardhi la kijiji limekiuka maadili, mfano kula rushwa. Lina adhibiwa na nani na kwasheria ipi? Nauliza hivi kwa sababu mabaraza mengi yamekuwa yakijihusisha na vitendo vya rushwa na kuhukumu kesi vibaya kinyume cha sheria. Ni nani mwenye mamlaka ya kulisimamisha au kulifuta baraza la kijiji?
nafikiria kupitia mkutano mkuu wa kijiji wananchi wakiibua hoja , wahusika wanawezwa itwa na kuadhibiwa
 
nafikiria kupitia mkutano mkuu wa kijiji wananchi wakiibua hoja , wahusika wanawezwa itwa na kuadhibiwa
Naraza la ardhi la kijiji linasimamiwa na halmashauri ya kijiji, kama ambavyo baraza la kata linavyosimamiwa na kamati ya maendeleo ya kata (WDC).. Kama baraza la kijiji linatoa usuluhishi (maana lenyewe halina nguvu ya kutoa maamuzi- uwezo wake ni kusuluhisha tu mgogoro) basi halmashauri ya kijiji inaweza kulivunja lakini ushauri kama baraza hili linasumbua ni bora mtu mwenye malalamiko kwenda katika baraza la kata ambalo lina mamlaka ya kutoa uamuzi na uamuzi huo kuwa na nguvu ya kisheria.
 
Back
Top Bottom